Dereva Halima aliyekatika mkono asema 'Niliona mtu ninayemjua akivuka barabara kabla ya ajali'

Dereva Halima aliyekatika mkono asema 'Niliona mtu ninayemjua akivuka barabara kabla ya ajali'

Siku chache baada ya tukio la kukatika mkono wa kulia, Halima Mbwana aliyepata ajali wakati akiendesha basi la Super Feo lilipokuwa likitokea Songea kwenda Dar es Salaam, ameelezea kilichotokea sikunde chache kabla ya tukio.

Kwa sasa Halima anaendelea na matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya St. Benedict iliyopo Ndanda Mtwara baada ya ajali hiyo iliyotokea Mei 22, 2022.

“Wakati natokea Songea kwenda Dar es Salaam kupitia Lindi, sehemu zote hatarishi nilikuwa nimeshazivuka, kuna sehemu ina kona ya kawaida sana, nikaona kuna mtu anavuka kutoka kulia kwenda kushoto na nina mfahamu, ilikuwa ghafla sana.

“Nilishtuka sana, nikawa namkwepa, kushtuka gari likawa limeshalalia upande mmoja, lakini baadaye nilibaini kuwa hakukuwa na huyo mtu, ni miujiza tu ya barabarani, hivyo vitu vipo.

“Wakati gari linalala mkono wangu ulikuwa nje, lilivyoanguka mkono wangu ulikatika palepale nauona, nikakumbuka kuwa gari bado linawaka na inaweza kulipuka, nikatumia mkono wangu wa kushoto kulizima kwa usalama wa kuondoa moto.

“Namshukuru Mungu, nilihudumiwa vizuri hospitali, ndoto yangu ilikuwa kuendesha gari zaidi ili baadaye nisomee urubani, lakini sijakata tamaa kuwa maisha yangu yameishia hapa,” – Halima.


Source: Azam TV

Pia soma: Basi la Super Feo Songea-Dar via Lindi limepata ajali. Dereva mwanamke avunjika mkono
Ngoja kwanza nicheke
 
Kashasema mkono mmoja ulikua nje means alikua karelax anapiga mashine kwa mkono moja...na ndio maana hiyo kona aloona ya kawaida akashindwa kuimudu... Huhitaji akili ya ziada kung'amua hili. Pole dada yetu..kuendesha gari mkono mmoja mwisho speed 40..na ni marufuku kuning'iniza mkono nje..hata askari mwenye uelewa lazima akuzingue
 
Nimewahi kutana na hiyo hali na ilibaki kidogo tufe mimi, baba, mama, mjomba, watu kama 7 hivi

Niko speed 150kmph ghafla mbibi anatokeza mbele akiongea na simu, afu macho yakapoteza visibility, ghafla niliyekuwa naye akashika steering akitaka kumpisha nisimgonge, hapo nishapanic honi nabonyeza hailiii....
Nikasema liwalo na liwe, nikapita pale pale, mshangao yule bibi sikumgonga...

Ningempisha hata kidogo nisingekuwa hapa leo
Ipo hii!

Na, Inaletwa na uchovu!
 
Afrika ulozi upo sana tu..sema wafia dini za wazungu na waarabu watabisha.

Chamsingi omba yasikukute.

#MaendeleoHayanaChama
Waarabu unamaanisha uislam? Sisi waislamu tunaamini uchawi upo, labda Kama una lingine
 
Hahah...

Hapana aliendelea na mishe zake, mimi nikaendelea kuchapa lapa kuwahi niendako...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka sana lol.
 
SuperFeo aka Omary M.Msigwa.jamaa ana mambo ya kishirikina kiasi hata mke wake wa kwanza alikataa kufunga nae ndoa na wameachana licha ya kuwa na watoto.kwa sasa inasemekana ameoa mwanamke mwingine mwenye asili ya kizungu na ndoa walifungia dar es salaam.nb mke wa kwanza ni mlokole
Akikataa kutoa kafara mtoto wao, na huyo mwanamke ni mndendeule wa Namtumbo, katoa siri nje. Na sahivi ananunuq kafara kwa watu. Huyu msigwa tutamchoka wallah.
 
Back
Top Bottom