Dereva Halima aliyekatika mkono asema 'Niliona mtu ninayemjua akivuka barabara kabla ya ajali'

Dereva Halima aliyekatika mkono asema 'Niliona mtu ninayemjua akivuka barabara kabla ya ajali'

Still ataendelea kutimiza ndoto yake apate mkono wa bandia ila sijui kama sheria za udereva zinaruhusu, kuendesha kwa mkono bandia
 
New Force tena si Bora Tavavile. Sasa hivi nimekuwa muoga kusikia hizi habari za Superfeo ndiyo gari yangu Pendwa
New force Wachina sidhani kama Wana mambo hizi,Mimi najiuliza mbona madereva wa kichina wao walikuwa awapati ajali walipokuwa wakiziendesha
 
New force Wachina sidhani kama Wana mambo hizi,Mimi najiuliza mbona madereva wa kichina wao walikuwa awapati ajali walipokuwa wakiziendesha
New Force ilikuwa hivyo zamani kidogo ...sasa hivi sijui sema naogopa tu. Ila mimi naongelea kuhusu ajali nadhani sbb ya speed.
 
Akubali tu alishindwa kulimudu gari kwenye kona kutokana na kuwa katika mwendo mkali. Hayo mambo ya kumkwepa mtu anaye mfahamu, na kushindwa kulimudu gari na kupinduka; ni utetezi wa kufikirika.

Yaani ni sawa na mtu afanye kitendo cha ubakaji, halafu ajitete eti Shetani alinipitia! Alikupitia kwenda wapi!

All in all, pole nyingi kwake. Hata mimi niliyaona yale mahojiano yake na yule mwandishi wa Azam Media.

Kuna baadhi wa madereva gari liko kwenye mwendo na haswa hawa wa mabasi wanatoa mikono nje akiwa anapisha na mwenzake kumpa ishara ya kuwepo kwa traffic police uwa kinanisikitisha sana, sababu ikitokea hatari yoyote wakati wanapishana kama tairi kupasuka sijui huo mkono kama utasalimika.
 
Mkono nje ya gari unafanya nini alafu analiendesha gari
Ukifanya utafiti kidogo utagundua madereva wa safari ndefu hususani mabasi na malori mara nyingi huwa wanatoa mkono nje ya dirisha wakati wakiendesha chombo. Nadhani sababu ni kuwasaidia kuondoa uchovu na usingizi kwa kupigwa na upepo..Mtizamo
 
Msigwa huyo akaweka kiini macho ili dereva aangushe gari, abiria wafe yeye apate kafara, huyu baba atatuua wangoni wote khaaah.

Tutamchoka na tutamfurusha km mwenzie Ottawa. Msieeew zake.
Msigwa gani tena?....
 
😂 huyu dada tulianza kumuonea huruma ila sasa anaanza kutuletea mapicha picha yake stori za kuamini ushirikina... Hayo ni mambo ya kawaida tu it depends labda sababu ya uchovu, mawazo, stress za maisha, umeamkaje siku hiyo, mshituko n.k
Namshaur akae kimya amewatoa watu ktk hali ya kumsaidia sasa wanajadili imani yake... Anyways
 
Daah kitu kama hii niliiona Sukamahela pale Singida bibi mmoja yuko katikati ya barabara na yuko umbali wa mita chini ya 5, eeee buana weeee ile kuhamaki na kutoa macho pamoja na kushika kichwa akili ikiwa imehama mtu anaonekana nyuma akikatisha barabara kulia kwenda kushoto ukitokea Dodoma.

Hapo ndio nikajua kuna mambo japo ile picha kichwani huwa haileweki (ninachoona ndicho au naota)

We gonga tu. Fanya kama umeona Zombie.
 
New force Wachina sidhani kama Wana mambo hizi,Mimi najiuliza mbona madereva wa kichina wao walikuwa awapati ajali walipokuwa wakiziendesha

New force jaribu kufanya uchunguzi kuna kitambaa chekundu kimefungwa nyuma ya gari upande wa chini kabisa,na ni kwa kila gari.hawa wenye magari wana mambo mengi sana hatari kwa maisha ya watu
 
Msigwa gani tena?....

SuperFeo aka Omary M.Msigwa.jamaa ana mambo ya kishirikina kiasi hata mke wake wa kwanza alikataa kufunga nae ndoa na wameachana licha ya kuwa na watoto.kwa sasa inasemekana ameoa mwanamke mwingine mwenye asili ya kizungu na ndoa walifungia dar es salaam.nb mke wa kwanza ni mlokole
 
Ndumba zipo..nilishuhudia sehemu jamaa wanafanya uchawi barabarani mchana wa jua kali..tena barabara kubwa highway..cha ajabu tunaona magari kwa mbali ila hayafiki mpaka walipomaliza gari zikapita..na sio kwamba zilikua zimesimama.
 
Nimewahi kutana na hiyo hali na ilibaki kidogo tufe mimi, baba, mama, mjomba, watu kama 7 hivi

Niko speed 150kmph ghafla mbibi anatokeza mbele akiongea na simu, afu macho yakapoteza visibility, ghafla niliyekuwa naye akashika steering akitaka kumpisha nisimgonge, hapo nishapanic honi nabonyeza hailiii....
Nikasema liwalo na liwe, nikapita pale pale, mshangao yule bibi sikumgonga...

Ningempisha hata kidogo nisingekuwa hapa leo
 
Back
Top Bottom