Mauzauza yapo barabarani,ilikuwa ni ghafla sana nilishutukia kitu kama Mbwa anakatiza barabara,sikutaka kumkwepa kwani umbali ulikuwa ni mdogo sana na ni usiku,nikamgonga na ngao ikapasuka nikasikia kabisa imedondoka na vipande vimepasuka kwa chini,Nikasimama kama mita 300 kuangalia nikakuta kweli imepasuka,nikasema ngoja nirudi labda naweza kuokoa baadhi ya vitu vilivyo dondoka,siku ona Mbwa,wala kilichoangauka,wala damu.Yani barabara ni nyeupe kama hakuna kilichotokea,kesho yake nikapita mchana ili niangalie vizuri sikuona chochote,ukichukulia kuwa pamenyooka kabisa.Nikaulizia wanaopafahamu wakaniambia hapa hivyo vitu vya kawaida sana.Wanaojua njia ya Babati Arusha karibu na daraja la Kiongozi...