PreGE2025 Devota Minja mkutanoni CHAUMMA, asema hakuna nchi iliyowahi kuzuia uchaguzi labda kuwe na vita

PreGE2025 Devota Minja mkutanoni CHAUMMA, asema hakuna nchi iliyowahi kuzuia uchaguzi labda kuwe na vita

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nchi ambazo uchaguzi umewahi kusogezwa mbele kwa sababu ya kushindikana reforms za uchaguzi au maandamano ni pamoja na Thailand(2014), DRC(2016), Iraq(2018), Sudan Kusini(2022)
 
Suala siyo hawaruhusiwi kushambulia chama kingine cha siasa, suala ni DHAMIRA.

Kwa madeleka kuhamia ACT nionyeshe kauli ya CHADEMA inayoashiria kulia waliyoitoa? Kwani alikuwa na impact gani CHADEMA au kwenye siasa za Tanzania? Hizo ni fallacy zako.

Kwenye hali hii ya kisiasa ambapo kiongozi mkuu wa upinzani anayetambuliwa hivyo siyo Tanzania tu bali hata nje ya Tanzania kupewa kesi ya kisiasa, wanachadema kutekwa, kuuliwa kupotezwa kwa sababu ya msimamo wao wa kisiasa unaowatikisa watawala dhalimu, ukurupuke kuja kuwapinga lazima uonekane chizi tu.

Unawakamata raia wa kigeni wakati wakazi wa East Africa tuna free movement. Ujinga juu ya ujinga unaofanywa na serikali halafu kitokee chama kiwe na sera za kukupinga siyo CCM, kitakuwa ni cha majuha
Mambo ya dhamira unaweza kuya judge kivipi?

Unaweza kuingia kichwani mwa mtu na kujua dhamira yake ni ipi?

Madeleka watu Twitter na Clubhouse jana nzima watu wamempiga mawe kwa sababu katumia haki yake ya kikatiba na kidemokrasia kuondoka CHADEMA. Ni wewe tu hufuatilii.

CHAUMMA wana haki ya kumpinga yeyote wanyetaka, ni haki yao ya kidemokrasia na kikatiba. Ukipinga hiki hujaelewa demokrasia ni nini.

Demokrasia si kika ntu awe CHADEMA.

Hamuelewi wapi?

Mtu anaweza kupinga utekaji na udhalimu wa CCM halafu akapinga CHADEMA pia, kwa nini mnaweka false dichotomy fallacy ya kukazinisha either or?
 
Sasa kama changamoto za wananchi ni pamoja na mapungufu ya vyama vya siasa visivyo madarakani utasemaje mapungufu ya chama chochote kisicho madarakani hayahusiani na changamoto za wananchi?

Pia, huwezi kufanya fikra dhahania kuona kuwa siasa ni pamoja na mijadala ya hoja, na ya vyama tofauti vya upinzani vinaweza kukinzana kihoja na kujadili hizo tofauti za hoja ili wananchi wajue misimamo ya vyama tofauti vya upinzani ikoje ili kujua vizuri wajiunge na chama gani?
Wewe mzee unapenda sana mabishano yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Ni ya wajinga wachache wanaojiona Wana akili kumbe Bure. Hao ndio g55

Huna unachochambua kwa kina hapa, nini cha kuchambuliwa kwa kina kuhusu CHAUMA? Yaani katika wapuuzi utakuwa ni mmojawapo maana haihitaji sayansi ya nuklia wala kutumia terminologies za kishamba ili kujenga hoja sahihi hapa. Unashambulia watanzania ukifikiri ni malimbukeni hawajifahamu kumbe wewe ndio mapungufu na terminologies zako. Tuonyeshe simple story kwenye current geopolitical climate hapa nchini?
Tuonyeshe false dichotomies
Tuonyeshe contradiction kwenye hili la hawa wapuuzi unaowatetea dhidi ya CHADEMA.

Usiwe mpuuzi kwa kuleta hoja ambazo haziakisi hali halisi ya kisiasa nchini,hakuna hoja yeyote ambayo unaweza kutetea CHAUMA kushambulia CHADEMA na kutaka kuwabagaza watanzania, wewe ndio dhaifu na hao unaowatetea, siasa za vikumbo na upumbavu wote unazotaka kuwaita watanzania ni upumbavu wako wewe mama watanzania siyo wajinga kama unavyojitahidi kutuita bali wewe pandikizi na wajinga wenzio.

Hivi watanzania hawaoni wanavyotekwa, kuuliwa, kupotezwa na ubabe mkubwa unaofanywa na polisi halafu unasema wamezoea siasa za kugombea daladala? Unajitambua kweli? Una matatizo kichwani
Kwanza kabisa sichambui CHAUMMA wala CHADEMA.

Nachambua hoja ya kidhahania ya chama cha upinzani kuwa na haki ya kupingana na vyama vingine vya upinzani.

Tatizo lako huwezi kufanya mjadala huo wa kidhahania, umeishia kuchambua vita vya CHAUMMA na CHADEMA.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Kwa nini umeweka false dichotomy?

Kwani CHAUMMA hawana haki ya kuona CHADEMA na CCM wote wana mapungufu, na hiyo ndiyo sababu kukawa na CHAUMMA, kama CHAUMMA wangeona CHADEMA haina mapungufu kungekuwa na haja gani ya kuwa na CHAUMMA?
Kwa hiyo CHAUMA manifesto yao ni mapungufu ya CHADEMA? Maana siku yao ya kwanza kufanya mkutano wao ni kushambulia CHADEMA?

Sababu kuua ya kuwepo kwa CHAUMA ni kupumguza nguvu ya CHADEMA kwa watawala ili CCM ipumue kidogo na CHAUMA ni diversion ya kupumguza mvuto na kukubalika kwa CHADEMA kwa wananchi na nje ya nchi?

Kama uko SAWA niambie umepata points zipi za maana kwa ujio mpya wa CHAUMA kiasi utukane watanzania?
 
Chadema hawajazuia wala hawana uwezo wa kuzuia uchaguzi kufanyika, hakuna uchaguzi kwa maana sheria zinazosimamia huo uchaguzi haziko fair, na kama haziko fair, uchaguzi huru na haki hakuna, bali unaegemea upande mmoja, Chadema wao wamesusa mpaka pale yatakapofanyika mabadiliko ya hizo sheria za uchaguzi wanasema Bila mabadiliko hakuna uchaguzi, yaani kwa tafsiri nzuri ni kwamba, Bila mabadiliko ya mifumo ya sheria za uchaguzi ukifanyika hautakuwa huru na haki, ndio maana hawasemi usifanyike, bali hakuna uchaguzi, kusema sio kuzuia bali ni kauli mbiu tu cha kushangaza waiopenda haki ndio wanatafuta huruma kwa kuihukumu Chadema, wanaosema hayo ni CCM waliokwenda Chaumma na wameenda kutafuta fursa ya kugombea, watashindaje na sheria hizo mbovu?.

Basi Kuelewa Kauli za wanasiasa ni ngumu sana, na inawezekana ndio maana kuna mgawanyiko ndani ya Chama.

Maana ulichosema hapa ni tofauti Kabisa na Kinachosemwa Majukwaani

Mfano.

"Hatutasusia uchaguzi bali tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya umma,tutawaalika Watanzania wahakikishe haufanyiki"- Tundu Lissu

Hii ni tofauti Kabisa na Ufafanuzi ulioutoa.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kwa hiyo CHAUMA manifesto yao ni mapungufu ya CHADEMA? Maana siku yao ya kwanza kufanya mkutano wao ni kushambulia CHADEMA?

Sababu kuua ya kuwepo kwa CHAUMA ni kupumguza nguvu ya CHADEMA kwa watawala ili CCM ipumue kidogo na CHAUMA ni diversion ya kupumguza mvuto na kukubalika kwa CHADEMA kwa wananchi na nje ya nchi?

Kama uko SAWA niambie umepata points zipi za maana kwa ujio mpya wa CHAUMA kiasi utukane watanzania?
Siongelei CHAUMMA na CHADEMA.

Naongelea kanuni kubwa zaidi za uhuru, katiba na demokrasia.

Huelewi wapi?
 
Basi Kuelewa Kauli za wanasiasa ni ngumu sana, na inawezekana ndio maana kuna mgawanyiko ndani ya Chama.

Maana ulichosema hapa ni tofauti Kabisa na Kinachosemwa Majukwaani

Mfano.

"Hatutasusia uchaguzi bali tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya umma,tutawaalika Watanzania wahakikishe haufanyiki"- Tundu Lissu

Hii ni tofauti Kabisa na Ufafanuzi ulioutoa.
Kuna watu wengi wanakuja hapa kuandika mambo mengi kwa hisia tu wakati hawana taarifa za msingi kabisa kama hii.

Nilimueleza hivyo hivyo bila ya kuwa na hiyo nukuu mahsusi.

Shukurani kwa kuweka nukuu inayohusika.
 
Kwanza kabisa sichambui CHAUMMA wala CHADEMA.

Nachambua hoja ya kidhahania ya chama cha upinzani kuwa na haki ya kupingana na vyama vingine vya upinzani.

Tatizo lako huwezi kufanya mjadala huo wa kidhahania, umeishia kuchambua vita vya CHAUMMA na CHADEMA.
Kuchambua dhana ya chama kimoja cha siasa kupingana na chama kingine cha siasa Iko sawa, ila kukataa kuwa CHAUMA ni pandikizi na haikuwa sawa siku ya kwanza ya mkutano wao mkuu kushambulia CHADEMA ndio hoja kuua ya mjadala wa mtoa post.

Kwa hali ya kisiasa nchini wanachofanya CHAUMA ni kuisaidia CCM, dhana zako za kufirika endelea nazo lakini ukizi apply kwa CHAUMA umekosea utaonekana pandikizi kama hao.

Rejea toka uchaguzi wa CHADEMA hadi uwepo wao CHAUMA na upuuzi waliozungumza unganisha dotes utawajua ni mapandikizi
 
Siongelei CHAUMMA na CHADEMA.

Naongelea kanuni kubwa zaidi za uhuru, katiba na demokrasia.

Huelewi wapi?
Huongelei CHAUMA na CHADEMA bali case study yako imeanzia CHAUMA na CHADEMA.

Nini huelewi?
 
Hatimaye CHADEMA wamepata chama cha upinzani, hawa Wafuasi watiifu a k a nyumbu wa Mwenyekiti ni watu hatari kuliko hata CCM yenyewe,wamecheza na akili zetu miaka kibao nasi tukaamini ni Wapinzani kweli.
 
Kuchambua dhana ya chama kimoja cha siasa kupingana na chama kingine cha siasa Iko sawa, ila kukataa kuwa CHAUMA ni pandikizi na haikuwa sawa siku ya kwanza ya mkutano wao mkuu kushambulia CHADEMA ndio hoja kuua ya mjadala wa mtoa post.

Kwa hali ya kisiasa nchini wanachofanya CHAUMA ni kuisaidia CCM, dhana zako za kufirika endelea nazo lakini ukizi apply kwa CHAUMA umekosea utaonekana pandikizi kama hao.

Rejea toka uchaguzi wa CHADEMA hadi uwepo wao CHAUMA na upuuzi waliozungumza unganisha dotes utawajua ni mapandikizi
Hakuna popote niliposema CHAUMMA ni pandikizi au si pandikizi.

That logical fallacy is called strawman argument.

It is also a logical non sequitur fallacy.

Whether CHAUMMA ni pandikizi au si pandikizi is immaterial.

CHAUMMA wana haki ya kikatiba na kidemokrasia kuipinga CHADEMA, whether CHAUMMA ni pandikizi au si pandikizi.

Wapingeni CHAUMMA kwa hoja, msitake kuwanyamazisha wasiiseme CHADEMA na kuwapangia waiseme CCM.
 
Huongelei CHAUMA na CHADEMA bali case study yako imeanzia CHAUMA na CHADEMA.

Nini huelewi?
Sielewi inakuwaje wafuasi na watetezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wanaingilia uhuru wa kikatiba na kidemokrasia wa CHAUMMA kujiamulia wanataka kupinga nini. Wanataka kuipangia CHAUMMA isiiseme CHADEMA.

Hawa watu inaonekana hawaelewi demokrasia ni nini, licha ya hicho chama wanachokitetea kuitwa cha Demokrasia.
 
Kwanza kabisa sichambui CHAUMMA wala CHADEMA.

Nachambua hoja ya kidhahania ya chama cha upinzani kuwa na haki ya kupingana na vyama vingine vya upinzani.

Tatizo lako huwezi kufanya mjadala huo wa kidhahania, umeishia kuchambua vita vya CHAUMMA na CHADEMA.
Mkuu hoja ilipoanzia ni mkutano wa CHAUMA na jinsi walivyojikita kwenye kushambulia CHADEMA, na wewe in the first place ulikuwa unatubananga kwa materminology ya kilatini ili kutuintimidate.

Kwanza nakubaliana na dhana ya chama cha upinzani kupingana na chama kingine cha upinzani kwamba ni demokrasia na ni uhuru, suala dhamira ndio ubishi ulipoanzia na utetezi wako kuwa wako right, je kwenye current geopolitical climate nchini CHADEMA kwa mpenda demokrasia inafaa kupigwa vita au kuungwa mkono?

Hapo ndipo kwenye difference's yetu
 
Sielewi inakuwaje wafuasi na watetezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wanaingilia uhuru wa kikatiba na kidemokrasia wa CHAUMMA kujiamulia wanataka kupinga nini. Wanataka kuIpangia CHAUMMA isiiseme CHADEMA.

Hawa watu inaonekana hawaelewi demokrasia ni nini, licha ya hicho chama wanachokitetea kuitwa cha Demokrasia.
Unapotosha kusema CHADEMA wanaingilia CHAUMA, Kwa siasa za Tanzania CHADEMA haiwezi kuingilia CHAUMA ila CHAUMA inaweza kuingilia CHADEMA kama mmoja wa makada wake alivyoshirikiana na msajili kutengua wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.
 
Sielewi inakuwaje wafuasi na watetezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wanaingilia uhuru wa kikatiba na kidemokrasia wa CHAUMMA kujiamulia wanataka kupinga nini. Wanataka kuipangia CHAUMMA isiiseme CHADEMA.

Hawa watu inaonekana hawaelewi demokrasia ni nini, licha ya hicho chama wanachokitetea kuitwa cha Demokrasia.
Huwezi kuelewa kwa sababu hutaki kuelewa, hawapingi haki ya CHAUMA kuipinga CHADEMA, that's their rights. Ila tunakushangaa wewe CHADEMA wanapojibu hoja zao CHAUMA na sababu za kupingwa nao wewe hutaki, je kwa akili yako CHADEMA hawaruhusiwi kujitetea?

Tatizo lako nini hapa?
 
Mkuu hoja ilipoanzia ni mkutano wa CHAUMA na jinsi walivyojikita kwenye kushambulia CHADEMA, na wewe in the first place ulikuwa unatubananga kwa materminology ya kilatini ili kutuintimidate.

Kwanza nakubaliana na dhana ya chama cha upinzani kupingana na chama kingine cha upinzani kwamba ni demokrasia na ni uhuru, suala dhamira ndio ubishi ulipoanzia na utetezi wako kuwa wako right, je kwenye current geopolitical climate nchini CHADEMA kwa mpenda demokrasia inafaa kupigwa vita au kuungwa mkono?

Hapo ndipo kwenye difference's yetu
Kwanza kabisa tumalize mjadala mmoja kabla ya kuurujia mwingine.

Umekubali kimsingi kwamba CHAUMMA wana haki ya kuipinga CHADEMA? Kuwa hii ni haki yao ya kidemokrasia na kikatiba? Kuwa chama cha upinzani hakitakiwi kupangiwa kipinge nini?
 
Back
Top Bottom