Kweli kabisa, kuna wajinga hata kulima hamna, eti wanasubiri reform, reform ni ya kumuingiza Lissu madarakani tu aanze kula hela. Watu wa jimbo la Singida mashariki wamekuwa na Lissu kama mbunge kwa miaka mingapi lakini jimbo halina maendeleo. Kama Lissu ni mtu wa mipango mbona jimboni kwake majalala tu.
Mfano, je Diamond angesema asijiingize katika fani ya muziki akisubiri kwanza nchi iwe na katiba mpya ingekuwa ni upuuzi.
Babu zetu enzi ya mkoloni walilima na kufuga na kutembea kwa miguu kufanya biashara, hapakuwa na reform wala katiba mpya, lakini kwa jitihada zao walilea familia na kusomesha wazazi wetu.
Katiba hata ikibadilishwa leo, serikali haitakulipia mahari, haitakuletea ugali nyumbani, haitakupa hela ya bia. Kimsingi hata Lissu anapigania reforms za uchaguzi tu aingie madarakani, ale hela za umma, hakuna mahali amepigania wewe upate ugali