Hili liko wazi sote tunalijua, wengi wa machawa wa serikali ya ccm wamelazimika kuwa machawa hili mambo yao yaende bila bugudha.Kwa mazingira yaliyopo ya kibiashara., kikazi ni ngumu kukua na kuwa multimillionaire Kama hauwezi kukubali kushirikiana na Serikali ya ccm na viongozi wake .
Kuna watu wapo ccm ili Ku-secure biashara zao , na sio mapenzi na hicho chama.
Ila alichokosea huyo mmanyema ni kutoa maneno ya kashifa na matusi kwa watanzania wasioridhishwa na uongozi mbovu wa ccm.
Kitendo cha kuwaita watanzania ni wavivu eti hawafanyi kazi na wakati hao hao watanzania ndio kila siku wanamuingizia hela kwa kustream nyimbo zake kwenye platforms mbali mbali kinamuonesha Diamond ni jinsi gani alivyokuwa na fikra finyu ambazo ni matokeo ya yeye kukosa shule.
Halafu mbaya zaidi anawatukana mpaka CHADEMA kwamba ni waongo wanadanganya watu kila mwaka, kwa hiyo moja kwa moja hapo anawatukana mashabiki wa mziki wake ambao ni wafuasi wa CHADEMA kuwa ni wajinga kila mwaka wanadanganywa, jambo ambalo huwezi kuona wanamuziki wenye akili walioenda shule wanafanya.
Diamond kafanya upumbavu sana bila kujua, na ana bahati sana anaishi nchi ya watu wasiojielewa, kwa nchi nyingine hata hapo jirani tu sasa hivi angekutana na massive cancellation kutoka kwa mashabiki mpaka angejuta.
Wapo machawa kibao wa ccm wengine ni ndugu zetu, ila hawana dharau za kipuuz namna hii.