Dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika

Mawazo ya mkoloni bado yanaishi kwenye kichwa chako
 
duuu! Aisee kumbe dini ni mawazo ya mkoloni pole Sana kwakua bado hujui hata dini ni Nini?. Nakusema tumefichwa toka utotoni. Si dhani Kama kunamazuri makubwa ambayo yalikuwepo kwenye dini ya sisi waafrika ambayo tumefichwa. Wakati masalia ya hii dini bado yapo na tunayaona na kuyasikia pia. Hivi labda nikuulize unavyoona albino wanauwawa watoto wanatolewa Sehemu za Siri, watu wanarogana, watu wanalala makaburini, watu wanakosana, magonjwa yanapuziwa kwa imani potofu,. Mimi ni kwambie tu huna mawazo yoyote kwenye hili swala zaidi ya kupotosha jamii.


Wewe na mtoa maada hamjui dini ya mwafrika wala dini inayomuhusu mungu Kama mnajua moja wapo Basi ni lazima iwe dini ya waafrika ambayo ilikua ni chukizo mbeleni mwa macho ya mbwana na Kama upo huko kweli Basi toka haraka kabla gazabu ahijakuwakia
 
nadhani hujanielewa hapa naongelea dini ilivyochangia kudumaza ufahamu wa mwafrika.

kwani kwenye hiyo list kuna mwafrika hata mmoja?

au kuna mwafrika yoyote mkristo aliyeugundua chochote chenye faida afrika?
kama wapo wataje hapa.
 
Blah blah hizi,ujinga na umasikini wenu unautupia kwenye dini. Kuna watu wanaamini ushirikina kama waafrika? afrika kuna watu badala ya kwenda hospitali wanaenda kwa waganga na kuzidisha maradhi yao na hadi kufa halafu ujinga kama huo wa waafrika unaenda kutupia lawama dini? Waarabu wameshika dini kweli kweli kuliko sie hata hatuwafikii ila bado wanatuzidi uwezo.
 
Blah blah hizi,ujinga na umasikini wenu unautupia kwenye dini.
Soma kwa makini hakuna sehemu nimeandika ujinga na umasikini nimeutupia kwenye dini bali nimeandika dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika.

Maana yake mwafrika alikuwa na ufahamu duni kabla ya dini.
Kuna watu wanaamini ushirikina kama waafrika?
Ndio maana nimesema dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika.
afrika kuna watu badala ya kwenda hospitali wanaenda kwa waganga na kuzidisha maradhi yao na hadi kufa halafu ujinga kama huo wa waafrika unaenda kutupia lawama dini?
Kwa hiyo unataka kuniambia hakuna waafrika wanaokwenda kwa mashekhe na wachungaji ili waombewe ila hawaponi na mwisho wake wanakufa?
halafu ujinga kama huo wa waafrika unaenda kutupia lawama dini?
Kwenda msikitini au kanisani kuombewa ili uwe tajiri na upone HIV huo sio ujinga?
Waarabu wameshika dini kweli kweli kuliko sie hata hatuwafikii ila bado wanatuzidi uwezo.
Hapa kwa asilimia 90% naongelea waafrika weusi Sasa wale sio waafrika weusi.
 
nadhani hujanielewa hapa naongelea dini ilivyochangia kudumaza ufahamu wa mwafrika.

kwani kwenye hiyo list kuna mwafrika hata mmoja?

au kuna mwafrika yoyote mkristo aliyeugundua chochote chenye faida afrika?
kama wapo wataje hapa.
Na ukikuta yupo utafanya nini?
 
nadhani hujanielewa hapa naongelea dini ilivyochangia kudumaza ufahamu wa mwafrika.

kwani kwenye hiyo list kuna mwafrika hata mmoja?

au kuna mwafrika yoyote mkristo aliyeugundua chochote chenye faida afrika?
kama wapo wataje hapa.
Kuna hii list ya wanasayansi na educationists Waafrika (bofya hapa List of African educators, scientists and scholars - Wikipedia). Ina mchanganyiko ya wanasayansi na educationists wenye imani ya dini na wengine hapana. Sijui utasemaje kwa hawa!
 
Wee jamaa unjikutaga great thinker kumbe huna lolote. Nilikuwaga nakudhania hivyo zamani lkn nilipokugundua nikakudharau mazima
Ukunidharau haipunguzi chochote kwangu ujue, sana utapata vidonda tumbo tu. If yako ndio naion hapa leo
 
Daahhh kwanini nilichelewa kuyaona maneno haya matukufu .... Binafsi mimi nilishajitoa kabisa katika ujinga wakuamini katika dini yoyote ile siingii kanisani wala msikitini nasitakagi kuusikia huo ujinga
 
Unachekewa kazini eti alikuwa anapiga maombi!! Kila kitu unamuachia Mungu! Ukipigwa shavu la kulia mgeuzie na shavu la kulia! Ndio mzungu!!! maisha ni haya : ukipigwa shavu la kulia rudisha katika shavu hilohilo mpaka meno yote yadondoke. Atashika adabu na maisha yanaendelea. Usiwe mtumwa wa dini!
 
Daahhh kwanini nilichelewa kuyaona maneno haya matukufu .... Binafsi mimi nilishajitoa kabisa katika ujinga wakuamini katika dini yoyote ile siingii kanisani wala msikitini nasitakagi kuusikia huo ujinga
Umenifurahisha sana ulivyosema matukufu.

Ila yana ukweli mwingi sana ndani yake ingawa wafia dini watabisha kama alivyosema Xi
 
Umenifurahisha sana ulivyosema matukufu.

Ila yana ukweli mwingi sana ndani yake ingawa wafia dini watabisha kama alivyosema Xi
Walk brainwashed wanapaswa kuhurumiwa .... Ila dini ni ulevi 1 mbaya sana 😂
 
Du lakini inafikirisha. Kwanini rangi nyeusi iwakilishe jambo baya, msiba, uzamani, uovu, hata orodha ya wabaya wanaita black list. Je giza au weusi ni kiwakilishi cha ubaya? Rangi yetu sie weusi kweli ina maanisha laana au ubaya? Inafikirisha ujue!
 
NAITOSHE KUSEMA MTOA MADA UPO SAHIHI NA ASANTE SANA KWA KULETA HII TOPIC,

According to history hizi dini kubwa mbili hapa Africa zimeletwa na watu kutoka western/ European countries(ukristo) na Middle East countries (uislamu). Hawa watu kwa nyakati tofauti walitutawala na kuchukua rasilimali zetu kwa faida zao binafsi wali watesa sana Babu zetu walifanya kila wawezalo kutu kandamiza na kutu nyanyasa tukiwa katika ardhi yetu na machoni kwao mtu mweusi hakua mtu alikua ni kiumbe kisicho na samani kabisa na hii mpaka leo tunaiona.

Swali la kujiuliza kwa mapenzi gani walio nayo kwetu sisi weusi na huruma ipi walio nayo kwetu mpaka watufundishe mambo mazuri kumuhusu mungu ambae hatumuoni???? Hivi kweli Quran na Bible vingekua na thamani kiasi hicho kwa walivyo kua na roho mbaya ya kumtesa na kumuu mtu mweusi akiwa katika ardhi yao wenge tukabidhi kweli??? Hivi kweli mambo ya Heaven na aljana kama yange kua ya ukwel wangetufundisha kweli jinsi ya kwenda uko??? Kama kweli wana moyo mzuri kiasi hicho kwanini hawakuifanya hii dunia kuwa pepo kwa kuishi kwa misingi ya haki.

Ukwel mchungu lakini haina budi kuusema kwa yeyeto mtu mweusi anae usoma ujumbe huu naomba utambue yakua White people and Arabians wengi wao hawatupendi sisi weusi hakuna ethnicity yeyeto ambayo ina mapenzi ya kweli ma mtu mweusi hata wachina au wahindi na kama hawatupendi na mifano iko wazi leo inakuaje watueleze na kutufundisha mambo mazuri ya mungu kiukwe hii haingii akilini hata kidogo yani kwa mfano unaishi na mtu ambae humpedi na unatafuta kila njia ya kumuibia na kumkandimza kiuchumi alafu una mwambia usiangalie sana ya dunia duniani tunpita fanya mema uende kweny uzima wa milele [emoji15][emoji15][emoji15] shame on us black people.

Nimalizie kwa kusema hizi DINI zimeletwa na walio zileta walizieleta kwa sabau zao na faida zao wao wenyewe, kama wewe ni muislamu unamuita mkristo kafiri my brother/ sister wewe ni mpuuzi namba moja au kama wewe ni mkristo unamuita muislmu mtu wa dunia na wewe pia ni mpuuzi kwa sababu kabla ya wageni kuja na kuzileta hizi dini mlikua mnaishi vzr kwa amani na upendo bila kuitana hayo majina. WAKE UP AFRICANS
 
Maneno kuntu hayo
 
Habari,

Binafsi nakushukuru kwa kuleta mada fikirishi kama hii, umeandika mambo mengi kwa kadiri ya uwezo wako wa kuchambua ulipofikia na kwangu mimi naona siyo jambo baya. Watu wengi hawajui hasa nini maana ya dini na nini lengo la dini miongoni mwetu sisi wanadamu ndiyo maana wengine wanapinga, wanalaumu na wengine wanaunga mkono lakini bado hawajatoa suluhu hasa ya nini matatizo yetu au dini imetusaidia nini. Binafsi nitajitahidi kadiri ya nilivyojaliwa kuelezea mawazo yangu machache.

Kwa kadri ninavyofahamu ni kuwa Dini ni njia ya Mwanadamu kumtafuta na kumuabudu MUNGU (Tafsiri yangu), hivyo basi dini ni ya Mwanadamu maana MUNGU hana dini kwa kuwa yeye anaabudiwa na haabudu kiumbe chochote. Mambo mengine mengi yaliyomo ndani ya vitabu vya dini (Biblia na Quran) ni sheria, mila na tamaduni zao (hao waleta dini) kwa jinsi walivyoishi zama zao hivyo kwetu sisi hazina uzito maana hata sisi tunazo. Kama Babu zetu wangekuwa na akili kubwa wangeweza kuhoji mathalani kuhusu majina maana tumeaminishwa kuwa majina ya kizungu ndiyo ya kikristo na majina ya kiarabu ni ya kiislamu wakati kiuhalisia siyo kweli maana majina yalikuwapo kabla ya dini hizo kuja na hakuna mtume yoyote aliyekuja na majina. Pia sisi Africa tuna majina yetu hivyo kama tukifikiri kwa kina tutagundua kuwa hatukua na haja ya kutumia majina yao.

Hao wazungu na waarabu tunaoshindana kuwalaumu kuwa walituletea dini hizi hata wao hawakuwa nazo hapo awali hivyo na wao waliletewa na wakati wakiletewa dini hizo za Ukristo na Uislamu siyo kwamba wao hawakuwa na dini, zilikuwepo ila hazikuwa za kumuabudu MUNGU wa kweli bali masanamu, jua, mwezi na wengine waliabudu nyota. (Hii ikiwa na maana kuwa walikuwa na MIUNGU ila hawakuwa na MUNGU wa kweli)

Kuhusu maendeleo na ustaarabu siyo kwamba vililetwa na dini bali dini hizi mbili zilikuta jamii za wakati huo zikiwa zimestaarabika maana tayari walikuwa na mavazi, walijenga majengo na walijua kuchimba visima vya maji pia walimiliki mali na walikuwa na mifumo ya utawala yenye kueleweka, hivyo ilichofanya dini ni kunogesha ustaarabu huo kwa kuwafanya watu kumjua MUNGU wa kweli, kupendana, kuheshimiana na pia kuelimika kwa kujifunza zaidi. Hivyo ukisema dini imeleta maangamizi Afrika utakuwa unakosea.

Kwangu mimi binafsi naona ni ujinga kumlaumu mzungu au muarabu kwa umaskini wetu, inafaa tukubali kuwa sisi tuna akili ndogo na wenzetu wana akili kubwa, bila hivyo hatuwezi kupiga hatua, tutaendelea kuwalaumu viongozi wetu huku tukijua wametokana na sisi hivyo na wao wana akili ndogo kama sisi. Kama ambavyo mgonjwa akienda kwa Daktari akaambiwa kuwa homa inayomsumbua ni malaria, inatakiwa mgonjwa huyo akubali kuwa ana malaria ndipo apewe doze lakini akikataa kuwa hana malaria hata akipewa dawa hawezi kuzimeza. Sasa kama sisi hatutakubaliana kuwa tuna akili ndogo basi kujifunza na kukosoana itakuwa vigumu hivyo tutaendelea kupiga marktime.

Matatizo tuliyonayo Waafrica yametokana na tabia ya uvivu, kutopenda elimu na kujidharau/kudharauliana sisi wenyewe kwa wenyewe (KUJIENDEKEZA) na kisha kumtukuza Mzungu na Muarabu, yaani imefikia hatua kuwa Muafrika mbele ya mzungu au muarabu ni kama mmbwa mbele ya chatu.

Suluhisho ni kuwa, tukiacha kujiendekeza na kudharauliana na kisha tukachapa kazi kwa bidii na kuwa waaminifu miongoni mwetu, tutapiga hatua ya kimaendeleo na tutafika mbali, hata tusipowafikia wazungu au waarabu lakini angalau tutaweza kutatua matatizo yetu ya msingi kama vile ukosefu wa chakula bora (ardhi tunayo), elimu bora na uchumi endelevu. (Nina mengi ila nimechoka kuandika)
 
Waafrika tungekuwa wavivu kama unavosema tusingeijenga marekani na ulaya. Acha kuchukia waafrika wenzako.

Self hate ndo inatusumbua. Yani unadiriki kuandika gazeti kwa ajili ya kupinga positivity. Stop that brother.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…