Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Sasa kitu gani kinazuia tusiwape hiyo tume huru wanayoidai,maana kama ni wapiga kura wapo upande wetu
Hebu nisaidie ili hiyo tume iwe huru inatakiwa iweje? Au unaimba tu Tume Huru lakini hata huelewi mfumo wa nchi hii mkuu.
 
Hebu nisaidie ili hiyo tume iwe huru inatakiwa iweje? Au unaimba tu Tume Huru lakini hata huelewi mfumo wa nchi hii mkuu.
Tunaweza kucopy na kupaste toka nchi nyingine kama tulivyofanya kwa BRN na mengine,mbona nchi nyingi tu zina tume huru za uchaguzi,si lazima tuanzishe formula yetu mkuu kwenye jambo hilo
 
huyu Mwalimu Wangu tangu amekalia hicho kiti na Akili imehama kabisa mungu amsaidie kwa kweli, Mkate wa Kila siku unapokuwa unapatikana bila taabu hata akili huwa inagoma kufikiri, huyu kwenye midahalo pale Nkuruma ndio alikuwa anazungumzia haya mambo ya Demokrasia, Haki na Tume huru leo gafla hata haoni maana ya Tume kisa amepewa shavu, Eeeh Mungu Tunusuru

Katika vitu napongeza awamu ya tano ni kutuonyesha dhahiri tabia za wanaojiita wasomi! Kumbe wana tamaa, njaa na tamaa ya vyeo kiasi vimemeza usomi na ufikiri wao kabisa!

Taifa hili tusitarajie wasomi kuliokoa, wameshafeli kabisa!
 
Ana maanisha watanzania huwa wanaipigia kura CCM kwa kura za kutosha na kwamba tume iliyopo na zilizopita zimekuwa fair kabisa.

Hivyo basi, hata ije tume kutoka mbinguni kutakatifu CCM itaendelea kushinda.

Kwamba hakuna haja ya tume huru. Lakini uzuri wa kauli yake ni kuwa amekiri bila kugundua kuwa kuna walakini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wana jiamini wana wapiga kura wa kutosha mbona wana tumia polisi kupata ushindi? /kwanini hawa taki tume huru? Ma prof wa Tz Mungu awarehemu

Sent using Jamii Forums mobile app
Naamini siku akitoka ndani ya ccm akawa huru atajilaumu sana kwa kuidhalilisha hiyo PhD yake.

Maana hayo maneno anayo yaongea hayastahili kutoka kinywani kwa mtu aliyesota darasani miaka kibao kuitafuta hiyo PhD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom