Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Hivi ilitokea Dr kibarua chake kimeota nyasi atarudi chuoni kufundisha? Labda hivi vitoto vya siku hizi vinakwenda chuo kikuu vinajua zaidi mapenzi kuliko upeo wa akili zao vinaweza kukubali kusikiliza lecture yake otherwise wenye akili timamu akiingia kwenye lecture yake wangetoka.

Dr hanatofauti na yule Dr aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutumbuliwa na JPM akaanza kulia lia kuomba msamahi Eti " Mimi ni yatima". Imagine elimu ya Tz level ya PHD hajui tafasiri ya yatima.
 
Dr. Bashiru; katika jambo ambalo mmekurupuka kama chama ni hili la elimu bure.Hamkujiandaa nalo bali mlilivamia tu kiajaliajali kama mtaji wenu kisiasa.Mpaka leo bado mnaendelea 'kuchezea'elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ukishaingia kijani na njano elimu na akili HUVIA.
huyu Mwalimu Wangu tangu amekalia hicho kiti na Akili imehama kabisa mungu amsaidie kwa kweli, Mkate wa Kila siku unapokuwa unapatikana bila taabu hata akili huwa inagoma kufikiri, huyu kwenye midahalo pale Nkuruma ndio alikuwa anazungumzia haya mambo ya Demokrasia, Haki na Tume huru leo gafla hata haoni maana ya Tume kisa amepewa shavu, Eeeh Mungu Tunusuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa wa CCM.

Maneno aliyo yaongea na elimu aliyo nayo sidhani kama vinaendana.

HOTUBA YA DR. BASHIRU KWA UFUPI

CCM inatoa salamu za mwaka mpya 2020, niwahakikishie watanzania kuwa tutaongoza siasa safi,ni mwaka wa kuheshimu maoni na uamuzi wa Umma, na tutashinda kwa kishindo kwa kuwa wananchi walihitaji huduma ya maji, elimu bure, afya na sasa wanapata huduma hizo,wananchi sio wanafiki.

CCM inapingana na udhalilishaji unaojitokeza ktk chaguzi, Wanawake kabla ya kugombea wanaitwa majembe, wakichukua fomu za kugombea wanaanza kuchimbwa na kupewa kashfa,wanajazwa hofu na wanaogopa, awamu hii CCM haitakubali wanawake wadhalilishwe na haki ni lazima itendeke kwa wote.

Wapo wanaolilia tume huru iwasaidie kupata ushindi, tume haipigi kura bali inasimamia uchaguzi, chama kisicho na wapigakura kisitegemee tume iwape ushindi, CCM imetafuta wapigakura kwa kutoa elimu bure, afya, maji na barabara, wao waseme wapiga kura wamewapataje.

Wenyeviti wa vijiji na mitaa, ninyi ni wajumbe wa vikao vya CCM kwenye Matawi na Kata, mtusaidie kupata wagombea bora, ikiwa mnaona kuna watu wanawazidi nguvu na kupendekeza wagombea wasio na sifa kwa maslahi yao, leteni taarifa haraka kusaidia Chama.

Swali fikirishi nani anayeweza kuiba kura kati ya watu hawa wawili anaye ratibu upigaji wa kura na anayepiga kura
 
Wewe Bashiru, mmeleta maji,elimu bure Je mateso ambayo wastaafu wanayapata kwa kutolipwa mafao yao kwa wakati mbona huyasemi, kuondoa fao la kujitoa, na yapo mambo mengi tu ya kukera ya kufanya watu waichukie ccm.Unajidanganya tu eti mnawapiga kura.
 
Huyo mpuuzi anajiita Bashiru anajifanya hajui kuwa tume ndiyo hupindua matakwa ya wananchi miaka yote. Huko Zanzibar Ni mfano dhahiri kabisa. Hizi degree zao uchwara Ni za kujaza matumbo tu wapate kwenda chooni. Ila haishangazi kwani Naye Ni zao la mule jalalani.
 
Ni kweli kuni ndizo zinazopika chakula,lakini chakula kikiungua kuni halaumiwi kwa kuunguza chakula,lawama zote kwa mipishi/Mtu.hawa viongozi wa sasa midomo huwa inawasiliana na ubongo wanapolopoka?
 
Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa
Kwa akili yako ndogo huwezi kumuelewa dk Bashiru
Mwaka 2015 Zanzibar kulikua na tume huru,lakini cafu hawakupata walichokitaka licha yao wenyewe kuwemo kwenye hiyo tume
Kenya kuna tume inaitwa huru,mpaka leo wapinzani hawajachukua nchi
 
Elimu ya Tanzania ni bora sana, ona Dr aka PHD holder and the former lecture from UDSM anavyomwaga point za maana. Huu ni mfano wa wasomi wetu walivyo bora kabisa, Hongera Dr Bashiru kwa kuitendea haki PHD yako..
 
Hivi chama gani kina ongoza Kenya? Ninacho jua KANU ndiyo iliyo pigania uhuru lkn sasa hivi KANU ilishajifia kitambo.
Kwa akili yako ndogo huwezi kumuelewa dk Bashiru
Mwaka 2015 Zanzibar kulikua na tume huru,lakini cafu hawakupata walichokitaka licha yao wenyewe kuwemo kwenye hiyo tume
Kenya kuna tume inaitwa huru,mpaka leo wapinzani hawajachukua nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema kuidhalilisha
Elimu ya Tanzania ni bora sana, ona Dr aka PHD holder and the former lecture from UDSM anavyomwaga point za maana. Huu ni mfano wa wasomi wetu walivyo bora kabisa, Hongera Dr Bashiru kwa kuitendea haki PHD yako..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Wapinzani wameibuka na hoja ya kudai marekebisho ya Katiba na sheria ili pawepo na Tume huru ya uchaguzi badala ya NEC.

Madai haya yangekuwa na mantinki kama Tume hiyo inalenga uchaguzi wa mwaka 2025 laki kwa uchaguzi wa October, 2020 ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.

Niwashauri tu CHADEMA kwamba mwaka huu waunge mkono juhudi hizo ndoto za Tume huru wazielekeze 2025.

Ni hayo kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!
 
hakuna kitu kinaitwa too late - Wana Sera mbadala - huu sasa ni wakati muafaka hasa wa kuibana Serikali kwenye jambo hili, cha msingi unganeni pamoja na muwe na sauti moja.

Sauti ya wengi ina nguvu na hata mwenyezi Mungu ataisikia.
 
Kukumbatia dharau, ufedhuli na kejeli za 99% ni sawa kuweka reheni umoja na ustawi wa taifa letu. Bora tudai tume huru sasa, wakatae tupate sababu na hoja watu kudai haki yao kwa njia mbadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakuna kitu kinaitwa too late - Wana Sera mbadala - huu sasa ni wakati muafaka haswa wa kuibana Serikali kwenye jambo hili, cha msingi unganeni pamoja na muwe na sauti moja.

Sauti ya wengi ina nguvu na hata mwenyezi Mungu ataisikia.
Waungane akina nani bwashee?!
 
Hakuna cha Shuka wala Blanketi mkuu kwanza wanaodai ni wao kwani wamekutuma wewe?
 
Back
Top Bottom