Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Sasa Wapinzani wameibuka na hoja ya kudai marekebisho ya Katiba na sheria ili pawepo na Tume huru ya uchaguzi badala ya NEC.

Madai haya yangekuwa na mantinki kama Tume hiyo inalenga uchaguzi wa mwaka 2025 laki kwa uchaguzi wa October, 2020 ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.

Niwashauri tu CHADEMA kwamba mwaka huu waunge mkono juhudi hizo ndoto za Tume huru wazielekeze 2025.

Ni hayo kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!
Hata wakati wa utawala wa kitumwa ilifika mahali babu zetu wakadai uhuru. Hata sasa baada ya kuona uchaguzi wa viini macho imefika wakati wa kudai tume huru ya uchguzi.. Wewe endelea kubaki utumwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Wapinzani wameibuka na hoja ya kudai marekebisho ya Katiba na sheria ili pawepo na Tume huru ya uchaguzi badala ya NEC.

Madai haya yangekuwa na mantinki kama Tume hiyo inalenga uchaguzi wa mwaka 2025 laki kwa uchaguzi wa October, 2020 ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi.

Niwashauri tu CHADEMA kwamba mwaka huu waunge mkono juhudi hizo ndoto za Tume huru wazielekeze 2025.

Ni hayo kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!

Huu ndio muda muafaka wa kudai tume huru ya uchaguzi, ingedaiwa mapema mngesema ni muda wa kujenga nchi na sio muda wa siasa za madaraka. Wapinzani msilogwe mkaacha kuidai tume hiyo sasa. Iwapo hakuna tume huru tutautia shombo huo uchaguzi kitaifa na kimataifa. Kwa maneno marahisi ni kuwa, tume huru ni sasa.
 
Bwashee kwa sasa muda siyo rafiki labda uchaguzi usogezwe mbele hadi 2022!
 
Acha kuusogeza, hata usiwepo kabisa miaka kumi ijayo, lakini hatupo tayari kushiriki uchaguzi wa kishenzi bila tume huru ya uchaguzi. Kwenye kuidai hiyo tume huru kelele zake ni za kitaifa na kimataifa. Nadhani serikali kwa kujua kuwa Mnyika atalizungumzia hilo, kipindi chake cha leo saa 5 asubuhi kimepigwa stop kufanyika ITV.
 
Tangazo la ITV lilisema wazi kuwa watarusha live mahojiano ya Mnyika kupitia akaunti yao ya facebook siyo luningani bwashee.
 
Nyie vyama vya upinzani unganeni muwe na msimamo, mjenge hoja ya kushawishi watu tususie uchaguzi kama hakutakuwepo na tume huru.

Tamaa na ubinafsi wekeni pembeni..kwa pamoja tuirudishe demokrasia.
 
Back
Top Bottom