Sioni kama ni ajabu, wala ubaya. Ukitafakari, kuna madokta wangapi, tena wengine udaktari hauna mchango wowote hata kwenye mtaa.
Mwigulu doctor, Musukuma docta, Dotto dokta, sasa hawa utawalinganisha na Samia? Kama ingekuwepo nyingine juu kidogo, Samia alistahili kupewa hiyo. Maana, hii ya sasa itamweka kwenye kundi moja na akina Musukuma na Mwigulu.
Japo kwa kweli kuna mengi bado ambayo yamekosekana kutoka kwa viongozi wetu:
1) bado hatujampata kiongozi mwenye dhamira safi ya kujenga demokrasia ya kweli, utawala wa haki na sheria.
2) bado hatujapata viongozi walionyoka kwa kauli na matendo, na wakweli wa nafsi.
3) bado hatujapata viongozi wanaoweza kuthamini uwezo wa watu na kuwapa majukumu ya kulisaidia taifa letu bila ya kuweka uchama kama ndiyo sifa kuu ya kwanza. Jambo hili limesababisha baadhi ya watu kuwa wanafiki na kuwa chawa wa watawala
4) bado hatujawapa viongozi wenye macho ya kumulika kuwatambua watu wenye uwezo wa kutoa mchamgo mkubwa kwa Taifa, ambao hawana habari na siasa za vyama. Viongozi wetu, uwezo wao wa kuona unaishia kwenye wigo za CCM.
Hongera Rais Samia, lakini heshima hiyo ingekuwa na nguvu sana na ya kukumbukwa kama ungefanya jambo tofauti, jambo ambalo watangulizi wako walishindwa, KATIBA NZURI MPYA.