Ni mawazo mabovu kupinga visions za mtu. Mtu ana maono ya kuifanya Tanzania iwe kama Ulaya, na Ulaya imekuwa vile kutokana na wazee wao kujitoa mhanga, kufanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu wakati mwingine wakijitoa maisha yao kwenda kutafuta makoloni nje ya Ulaya. Leo hii watoto na wajukuu na vitukuu vyao vinavuna matunda ya jitihada za mababu zao.
Usidhani wazungu wanawaponda viongozi wao wenye maono ya kuifanya Ulaya izidi kuwa Ulaya kwa kigezo cha demokarsia. Ndani ya Magufuli tuna kiongozi aliyerejesha pride ya mtanzania. Watanzania kwa fikra za kujiamini, kufanya kazi kwa malengo, na kwa uaminifu wa kitaifa na uzalendo tunaweza kujiletea maendeleo na nchi inaweza kupiga hatua zenye mwelekeo sahihi wa maendeleo.
Nipe kiongozi kama Magufuli anayeamini kuwa Tanzania inaweza kuwa kama Ulaya, kuliko unipe kiongozi mwingine yeyote mwenye fikra za kitumwa kuendekeza ukoloni mamboleo.