Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Msifanye makosa kuchagua kiongozi kwa kujaribu, mtapoteza miaka mitano bure!

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Msifanye makosa kuchagua kiongozi kwa kujaribu, mtapoteza miaka mitano bure!

Kama hampo tayari kumweka madarakani kiongozi tofauti basi fuateni masharti.
 
View attachment 1560349

Nachojua mimi huu ni muda wa kuuza sera na sio kutisha wapiga kura na kutumia mabavu. Ni muda wa kushawishi. Kama hali ni mbaya basi ashauriwe kupimzika kidogo ajitafakari na kutuliza mawazo

Hizi kampeni zitaweka wazi tabia halisi ya Magufuli, hata kwa wale waliokuwa hawaamini tusemayo dhidi yake. Na iwapo wapinzani watasimamia mshindi halali kutangazwa, mauaji ni lazima.
 
CCM kama hawafikirii vizuri ,wanasema tuwape miaka mitano tena watuletee maendeleo as if kuanzia 2015 kurudi nyuma mpaka 1961 walikuwa wanatawala wakoloni au upinzani ,tumewapa miaka karibia 59 hakuna la maana walilofanya ,je hiyo mitano kuna jipya wataleta? Kama wamepewa 59 bado hapa DSM baadhi ya sehemu hakuna umeme wala maji,kipindi cha mvua tu barabara hazipitiki mawasiliano yanakatika wa huku wa huku wa huko wa huko.
 
Hii mitano iliyopita tumepoteza, hatukubali kupoteza tena kwa kumchagua. Huyu mzee akapumzike.
 
"Hatuchagui Mtu wala sura, hata sura yangu ni mbaya, tunachagua Vyama , huwezi kuchanganya mambo Rais awe CCM wengine Vyama vingine, Mimi sifichagi nawaeleza ukweli fanyeni makosa mtajuta, nileteeni Mbunge na Diwani wa CCM, mkiniletea mwingine itaniuzi"

Jamaa libaguzi sana hili!
Halafu linasema nye nyeee "maenyeleo hayanya cnyamha@
 
Kwani tuliyoipoteza kwake ni midogo?
Au yeye hajui kuwa ametupotezea miaka 5?
 
Huko Magu, Magufuli amesikia alitoa vitisho kwa wananchi baada ya kumkataa mgombea wa Udiwani kuwa akichaguliwa anawatelekeza wananchi

Magufuli amewaambia hawatishi, anawaambia ukweli kuwa wasipomchagua watajuta
kisha akaendelea kuongea Kisukuma

Mheshimiwa itampasa azindue mbio za mwenge, na awe anambatana nao kwenye kampeni zake za uchaguzi wa mwaka huu. Pengine akili yake inaweza kuwa "recharged" kwa kupitia nuru yake.

Badala ya kuwanyenyekea na kuwomba kura wapigakura yeye anawakea kibezi cha matisho! Mh! Kweli kutokuwepo kwa marehemu Ben Mkapa kunampeleka nje ya reli. Hivyo vitisho aje pia kuvileta mkoa wa Mbeya.
 
Ndo yale yale ya Savimbi wakati wa kampeni za Angola alipowaambia wananchi wasipomychagua atarudi tena msituni , hataacha vita
 
Ivi ndio katiba yetu inasema ukichagua chama tofauti na kinachoongoza dola ni halamu kupelekewa huduma za kijamii na maendeleo? Na usipolipa kodi katika maeneo hayo unakuwa muhaini?

Yaani ulipe kodi ila maendeleo kwako hayaji na vyombo vya sheria vuko kimya?
 
Yeye ameshatugharimu 5 years inatosha. Apumzike tu.
 
Back
Top Bottom