Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Msifanye makosa kuchagua kiongozi kwa kujaribu, mtapoteza miaka mitano bure!

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Msifanye makosa kuchagua kiongozi kwa kujaribu, mtapoteza miaka mitano bure!

Magufuli ni blessing in disguise. Amekuja kuua kabisa CCM, by the time anamaliza muda wake, CCM itakuwa choka mbaya. Sijawahi kuona haya mambo, mpiga kura anafokewa
 
Ndugu yangua jpm akipita hata 2024 haifiki atakuwa keshabadili ukomo wa uraisi na ziko sheria zitaletwa za kumlinda
Connect dot why ikulu mpya,why kuuwa upinzani,rejea kauli za ndugai wanahitaji 2/3 ili wamalize kazi
 
kuiondoa ccm sio kazi nyepesi kama wanavyo fikiria wafuasi wa vyama vya upinzani haswa CDM.mtaji wa kura walizo nazo ccm ni mkubwa ukilinganisha na vyama vingine.
 
Huko Magu, Magufuli amesikia alitoa vitisho kwa wananchi baada ya kumkataa mgombea wa Udiwani kuwa akichaguliwa anawatelekeza wananchi

Magufuli amewaambia hawatishi, anawaambia ukweli kuwa wasipomchagua watajuta
kisha akaendelea kuongea Kisukuma

Hivi anajielewa kweli huyu? Ananitia wasiwasi. Kama amewafuata watu kuomba kura, inakuwaje kuwalazimisha watu kumpigia kura mtu wasiye mtaka?
Mbaya zaidi anawatishia kuwa wakimzomea ataondoka, sasa si aondoke tu kwani wao ndo walimwomba aende au shida zake ndizo zilizompeleka?
 
kuiondoa ccm sio kazi nyepesi kama wanavyo fikiria wafuasi wa vyama vya upinzani haswa CDM.mtaji wa kura walizo nazo ccm ni mkubwa ukilinganisha na vyama vingine.

CCM haina mtaji wa kura ila ina mtaji wa wa polisi na tume ya uchaguzi. Ukiviondoa hivyo, ccm ni nyepesi kuliko karatasi
 
Regadless ya ninachokiona , Kauli aliyotoa ni kauli ya kujiamini kuwa anachukua tena mamlaka, sasa mpira upo kwa uma/wananchi kufuata matakwa yake ama la, yeye keshasema matakwa yake sasa ni wananchi kuamua.

Ingekuwa sio rais hapo sawa, ila tabia hizi anazifanya hata sasa akiwa rais. Hata uchaguzi wa SM uliharibiwa kwa maagizo yake.
 
hawajatishwa bali wameelezwa ukweli.....maaana ccm ndio chama kinacho tawala....hivyo mkichagua wapinzania mtakuwa mmejimaliza wenyewe.......sahau maendeleo. bali mkitaka maendeleo chagua Rais wa Ccm Mbuge wa ccm na diwani wa ccm
Ile kauli ya maendeleo hayana chama huwa anamaanisha nini?
Mataga jiheshimu hata kidgo basi
 
Niwaulize NEC na TBC kama hizi ndio lugha za kiungwana kwa mgombea kutishia wapiga kura kua wasipochagua chaguo lake watakiona. Maendeleo watayasikia kwenye bomba tu na akatoa mfano hai wa Bunda. Inasikitisha, achilia mbali mapungufu yake mengine.
 
Huko Magu, Magufuli amesikia alitoa vitisho kwa wananchi baada ya kumkataa mgombea wa Udiwani kuwa akichaguliwa anawatelekeza wananchi

Magufuli amewaambia hawatishi, anawaambia ukweli kuwa wasipomchagua watajuta
kisha akaendelea kuongea Kisukuma

Heri kupoteza miaka mitano kuliko kupoteza miaka kumi
 
hivi kweli ukifikiria haswa unadhani kweli CHADEMA inaweza kuingusha CCM ?!hizo ni ndoto za mchana wa saa sita .
hata Mbowe na Lisu wanafahamu kuwa hawawezi kuitoa ccm madarakani.
kwa kampeni inayo fanywa na ccm ni wazi ccm itashinda
ccm kushinda haiwezekani hata upinzani wamweke mtu kama wewe, sema watatangazwa washindi
 
Halafu dakika chache baadae utamsikia akisema "Maendeleo ndugu zangu hayana chama"

Kazi kweli kweli.
Nimeona Ile clip akijinadi ameshafika ulaya hata akiwa Waziri ameshawahi kwenda. Juzi kajisahau kasema hajawahi kwenda Ulaya. Kuna shida ni muongo halafu Hana kumbukumbu.
 
Maendeleo h
Huko Magu, Magufuli amesikia alitoa vitisho kwa wananchi baada ya kumkataa mgombea wa Udiwani kuwa akichaguliwa anawatelekeza wananchi

Magufuli amewaambia hawatishi, anawaambia ukweli kuwa wasipomchagua watajuta
kisha akaendelea kuongea Kisukuma

Maendeleo hayana chama .why kutishana???Mungu pekee atatuvusha hata kama wanasiasa wataacha kuwajibika
 
Oh so pesa yetu imekuwa ya ccm?
Kwa majibu haya hafai kuwa kiongozi period
 
Kama miaka mitano hii tuliyoipoteza bure, kuna ubaya Gani tukipoteza mingine tena
 
Huko Magu, Magufuli amesikia alitoa vitisho kwa wananchi baada ya kumkataa mgombea wa Udiwani kuwa akichaguliwa anawatelekeza wananchi

Magufuli amewaambia hawatishi, anawaambia ukweli kuwa wasipomchagua watajuta
kisha akaendelea kuongea Kisukuma

Alianza mzee Mkapa kutamani uchaguzi huru, akafuatia Mzee Kikwete kutueleza yale tusiyo yajua baada ya kukurupushwa, akafuatia mama Maria kugoma kuzungumza baada ya kulazimishwa akaishia kuongeza idadi ya watu na sasa wananchi nao wamegoma adi wanazomea.
Mzee wetu ameamua kuwatisha wananchi kwamba umkizomea nitaondoka. Na mbaya zaidi amekwenda mbali kwa kulazimisha makubaliano, "tukubaliane, nachukua mradi wa maji na nyinyi mnichagulie mbunge na diwani (ninae mtaka mimi) bila hivyo tusiulizane".

Ukimsikiliza kwa makini huwa haongei kama mgombea anae omba kura za wananchi bali anaongea kama raisi, kitu ambacho sio sawa katika kampeni.
Kwa upande mwingine ni kwamba mpiga kura kwake yeye hana thamani tena, hutake ama husitake ni lazima umchague yule anae mtaka yeye. Hii ni hatari sana.
Kama hata ndani ya chama anacho kiongoza kama m/kiti anawalazimisha wapiga kura anavyotaka yeye. Je kwa upinzani wategemee haki kutendeka? Bado ni kitendawili.
 
Ingekuwa sio rais hapo sawa, ila tabia hizi anazifanya hata sasa akiwa rais. Hata uchaguzi wa SM uliharibiwa kwa maagizo yake.
Mfumo unaruhusu kutawala kwa utashi wa mtawala kulingana na mazingira.
 
Back
Top Bottom