Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Dkt. Modestus Francis Kipilimba: Wasifu wake

Mkuu umeonaa!watu wanataka mtu aliyeshapitia mafunzo ya kijeda,ashapigana,vita,ser n'a blak belt,ashaenda sana kwenye course cuba,Israël,marekani,north korea....awe ngangali......Kama putinnn

Ova
Ila hta uyo putin kwao hajawahi kua secret service agent
 
Mbona sioni course ya U-TISS?Au iko kwenye mabano,duh,TISS bwana.Mimi walinitaka nilipokuwa JKT nikagoma.Najuta kweli bwana,ningekuwa mbali kweli sasa kama ningekuwa sijafa.
WASIFU MFUPI (CV) WA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA, TANZANIA (TISS), DKT MODESTUS KIPILIMBA

Jina kamili ni Modestus Francis Kipilimba

Dini ni Mkristo

Ni mzaliwa wa Morogoro, Tanzania

Alifunga ndoa mwaka 1988, na ana watoto watatu.

Kuanzia Januari mwaka 1973 hadi Novemba mwana 1976 amesoma Shule ya Sekondari Kingonsera iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Kidato cha 5 na 6 amesoma Mkwawa High School iliyopo mkoani Iringa. Shahada ya kwanza amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Kompyuta.

Shahada ya Uzamili (Masters Degree) alisoma nchini Uingereza katika chuo Salford, Manchester ambapo alisomea masuala la Kompyuta tangu Septemba 1992 hadi Novemba 1994.

Shahada ya Uzamivu (PhD) alisoma katika chuo hicho hicho cha Salford kilichopo Manchester Uingereza, kutoka Februari 2002 hadi Septemba 2005.

Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Tarehe 15 Februari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Dkt. Kipilimba alijaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dickson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Tarehe 24 Agosti, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Chanzo: Swahili Times
 
Hahaha, yaani hili jukwaa burudani kwelikweli! By thevway inakuwaje bosi usalama wa taifa hana mafunzo ya kijeshi, na kiusalsma kwa ubobezi kabisa? Au kuwa na utaalamu wa usalama wa computer dystems inatosha?
AMEMALIZA SEKONDARI 1976, Alikuwa wapi?
 
Mkuu umeonaa!watu wanataka mtu aliyeshapitia mafunzo ya kijeda,ashapigana,vita,ser n'a blak belt,ashaenda sana kwenye course cuba,Israël,marekani,north korea....awe ngangali......Kama putinnn

Ova
Umbea haufai, ukishajua itakusaidia nini? Tosheka na hiyo iloyopo
 
Mbona mleta Thread hujesema alikuwa katika kitengo cha TEHAMA NEC mwaka jana au siyo huyu??(.................)
 
Nijuavyo directory wa intelijesia anakuwa amebukua maswala ya intelijesia, na ushushushu.
Nchi za wenzetu huwa wanaweka kwenye cm zao.
 
Mbona sijaona uzoefu wake WA KI TISS TISS? au nitaitwa mchochezi? ACHA niishie Hapo nisije nikazolewa hapa nyuma ya kibodi, upepo umesha chafuka

Wanaanzaga mbali hao iyo kazi,sometimes mtu yupo chuo wakati uho huo anakuwa tayari ni mtu wa Idara nasikia
 
Mkuu, uliwahi kuona mtu anaelezwa wasifu wake wa ki TISS TISS? Binafsi sijawahi kuona hata siku moja. Hata huyu aliyemaliza muda wake naye sikuona wakati anateuliwa kushika wadhifa huo

Kwan uliwah kuona wanatangaza nafasi za kazi za TISS? na kama jibu ni hapana inamana huwa hakuna waajiriwa wapya? mind u kiusalama hilo la CV huwez kuliskia

Bosi wa usalama anapsswa kuwa mwanajeshi aliyebobes kwenye mbinu mbalimbali za medani na usalama wa nchi!

Ni kweli usemayo lakini kwa upeo wangu mdogo alifaa ateuliwe miongoni mwa waliokaa kwenye idara hiyo na waliokubuhu ktk masuala ya upelelezi hasa ktk nyanja za kimataifa
 
Back
Top Bottom