Dkt. Mwakyembe Kuongoza Uchunguzi Malalamiko ya Mtihani wa Law School

Issue hapa siyo kufundisha shule ya msingi bali ni ile hali ya kustruggle kwa miaka 7 anatafuta digrii ya sheria halafu eti aje kuwa na ufaulu LST itakuwa ni kichekesho
Ndg MTU akiweka malengo anatusua tu bila shida, wapo maprofesa Leo WaLianza Kazi na cheti Cha darasa la saba B, leo hii ndo walimu wenu Huko varsity
 
Umesema jambo la maana sana ambalo wengine labda hawalijui au hawataki kulisema. Bila kutenganisha siasa na taaluma, itakuwa ngumu sana nchi hii kuondoa ujinga.

Tunachofanya sasa hivi si kuondoa ujinga bali kuufunika kwa vyeti na ufaulu usio na msingi wa maarifa ya kweli.
 
Ndg MTU akiweka malengo anatusua tu bila shida, wapo maprofesa Leo WaLianza Kazi na cheti Cha darasa la saba B, leo hii ndo walimu wenu Huko varsity
Elewa ndugu issue siyo kuanza na cheti cha LY bali umeipataje digrii? kwa sababu kuna watu ni LY lakini uwezo wao ni mkubwa sana ila tu hawakupata nafasi ya kuendelea kimasomo. Sasa huyo ticha digrii ya kuipata kwa miaka 3 anakuja kuipata kwa miaka 7, kuna mtu hapo kweli au ndo wale wa TRAB na TRAT?
 
Uvccm wanaotegemea teuzi[emoji1787][emoji1787]
Apo eka siasa pemben mkuu.. jamaa kaongea ukwel watz tunapenda kubenwa bebwa sn mpk kwmy ishu nyeti kama elimu... kama watu wamefeli means wameshindwa kufkia passmark tusilazimishe kila mtu awe na elimu ilihali hastahili kuwa nayo
 
Mkuu wasomi wa nchi hii niwa hafidhina wa ajabu Sana ambao hawa paswi kuwepo katika taasisi za umma Kuna Padre mmoja anafundisha chuo fulani aliwahi niambia kwamba shinda kubwa ya wahadhiri wengi wa chuo kikuu ni kujiona wenye akili kuzidi wengine hili naliona hapa kwetu Tanzania

Ndio maana unakutana na wakili anasema vyuo vya Sasa vinatoa product mbovu ndio maana wanafeli Sana ukimuuliza Wewe ulisoma chuo gani? Jibu linakuja ni vyuo vyetu hivi hivi Sasa una mshangaa yeye kujiona product bora na kudharau product nyingine kutoka vyuo hivyo hivyo kaitoa wapi?

Kuna mhadhiri yupo SAUT anafundisha philosophy anaitwa Komu alisha sema kwamba mhadhiri ukiona unafundisha na mwisho wanafunzi wengi wanafeli basi jifanyie tathimini au jitafakari binafsi Kuna shida.
 
-Vijana wanataka first sitting ziwe 100
-Dr zakayo lukumay alisema tatizo vyuo vile vya degree pia ni tatizo.
Shida sio chuo mkuu Kuna wahadhiri wanafundisha chuo na hao hao ni wahadhiri hapo law school Sasa mhadhiri anakutana na product yake mwenyewe aliyo izalisha toka chuo kitendo Cha kusema shida iko chuo basi nae ni sehemu ya tatizo lenyewe.
 
Na bado watakuja kutana na pepa za utumoshi na watagonga 3/100, sasa ndiyo watamlilia mwalimu ummy...
 
Kuna uwezekano tume yake ikaja,ba,majibu yalkyopangwa tayari. .mtu aliikana thesis yake mwenyewe ambayo ilikuwa inatetea serikali tatu ili tu kulinda maslahi ya kisiasa ambapo mfumo ulikuwa unatetea serikali mbili.
 
Kulingana na maelezo hapo juu yupo mwanafunzi wa LST aitwaye John Kaombwe
 
Ajabu huu ujinga hao walimu hapo LST wameshaurithisha kwa wanafunzi wao, wote wanaopita hapo nao wakiulizwa kwanini wengi wanafeli, watakujibu hawakuandaliwa vizuri kule walipotoka.

Unabaki kujiuliza, huyu ndie msomi aliyefaulu hapo alipo ikiwa analaumu kule alipotoka, hajui elimu ni muendelezo wa ngazi moja kwenda nyingine, sasa ukianza kuiponda ngazi uliyotoka maana yake wanataka isiwepo au ifanyweje?

Nagundua mwisho wa siku haya yote yanasababishwa na ubinafsi, aliyenacho hamkumbuki yule asiyenacho, anajiona yeye ndie bora zaidi yake, na hii tabia ndio inazidi kuliharibu hili taifa.

Hii precedence ya kuwaponda wahadhiri wa sheria wa vyuo vikuu ikiendelea itaharibu morali ya walimu, na hilo jibu kwangu najua ni ujanja wa walimu wa hapo LST kujikwepesha lawama, wao kazi yao ni kufelisha tu, sio kuingiza kitu kwenye ubongo wa mwanafunzi.
 
Sasa hapa tume ya mwakyembe ya kazi gani tena??! Maana hii ni ripoti tosha na imesheeni sababu zote msingi za mapungufu ya hiyo law school!
 
Unataka kumaanisha nini hapa?!
 
Issue hapa siyo kufundisha shule ya msingi bali ni ile hali ya kustruggle kwa miaka 7 anatafuta digrii ya sheria halafu eti aje kuwa na ufaulu LST itakuwa ni kichekesho
Kama wewe ni mfuatiliaji wa learning protocols utabaini kuwa huyu anashindwa mtihani ila sio uelewa! Time exposure yake kwenye kitu kilekile kwa muda huo inampa avenues nyingi za ubobezi na ukizingatia kuwa kufaulu mtihani hasa kwa Tanzania yetu ni matakwa ya msahisha mtihani mostly.
 
Ana maana kwamba shule ya huyo mtu ni ya kuungaunga mno, hivyo siyo rahisi kufanya vizuri hapo Law school ambapo vipimo vyake vimekaza sana.

Sir robby
Sio kweli, kama umekuwepo tangia Tanganyika kupata uhuru utakumbuka kwamba watendaji wengi wa Serikali ya Mwl. JKN walikuwa wa elimu ya kujiendeleza hiki unachoita kuungaunga, lakini ndio watendaji walioweka misingi mizuri ya taifa hili ambayo inabomolewa na wasomi wa sasa wa kukariri (kumeza) kwa ajili ya paper na kisha kufaulu mtihani bila kufaulu maharifa!
 
Mkaruka you're becoming too judgemental! Jitahidi kuacha kuongelea nadhalia juu ya mtu huyo mpaka umfanyie mahojiano utapata hoja nzuri za kuwasilisha jukwaani hapa.
 
Moja la vyuo na shule za siku hizi kutoa products mbaya ni sawa kwa sababu tushaona chanzo ni lugha ya kufundishia inavyotenganishwa na lugha ya taaluma fundishwa na nyongeza ni mtu aliyefeli wakati wa masomo yake kuja kuwa mwalimu wa kufundisha wengine baada ya kufaulu kwa njia zingine ambazo mmejizuia sana kuzitaja kwenye uzi huu!

Lakini pia ni kweli kuwa kufeli kwa mwanafunzi ni msiba kwa mwalimu wake, ukiona mwalimu anashangilia mwanafunzi wake kufeli ni wazi kwamba mwalimu huyo hakuwahi kufaulu kihalali wakati anasoma angetamani kuona mwanafunzi wake anajiongeza kufuata mbinu alizotumia kufaulu mwalimu huyo.
 
Mwakyembe amekaza, hataki kuachia nafasi kwenye Kamati. Sasa kamati ya Mwakyembe inapokea ushauri wa wadau, mwisho wa kutoa ushauri ni Oktoba 24,2022.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…