Dkt. Mwakyembe Kuongoza Uchunguzi Malalamiko ya Mtihani wa Law School

Dkt. Mwakyembe Kuongoza Uchunguzi Malalamiko ya Mtihani wa Law School

Acha kuongea uongo hapa mwnyw nimepita LST nilikamatwa but nikazichomoa second sitting! Hayo masuala ya kusema wanafunzi hawasomi ni uongo! Hakuna lecturer yoyote wa LST hapa atakayekiri madudu yanayofanyika pale....nasema hivyo kwa sababu nimepita hapo na nina uzoefu wa kutosha. Kama una hoja za msingi lete hapa tujadili........
VIjana hamtaki kupikwa mkapikika jmn
 
Mambo. LST ni chuo cha law sasa lazima kufurahisha wote waliochaguliwa ni wanasheria. Hata huyo aliepita hapo sio mwanafunzi tena. Ni muhimu kuwa na uwakilishi wa wanafunzi. Wangeweka at least 2, mkaka na mdada.
Pili ni vizuri wangekua pia na mjuzi mambo ya elimu hasa curriculum, assessment na evalution.
Ingependeza pia kuweka mtu mmoja ambae si mwanasheria lakini ana elimu ya kutosha na amebobea kwenye utafiti ( anaweza kuchimba mambo). Hapa tungekuwa na balance nzuri.
Kwa hyo hUyo mhitimu hamna imani naye??, Naye si anajua msoto wa LST
 
Muendelezo wa siasa katika mambo ya kitaalam.

Waziri yule yule aliyezua taharuki Ngorongoro ndio huyu huyu anayetaka kuimaliza tasnia ya sheria hapa nchini.

Kwaheri taaluma karibu siasa.
 
Na hili ombwe la vyuo vingne kutoa degree ya Sheria Miaka mitatu, vingne Miaka minne, ni vizur hili ombwe liondolewe, iwe Miaka SAWA vyuo vyote. Mbna Kwenye digrii zingne hili ombwe hatulion?Kamati waliangalie na hili
 
Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la ajabu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.



Credit: Malcom Lumumba
Mkuu Aikambee; umechambua vizuri sana! [emoji120]
 
Mwakyembe haaminiki , hata matokeo ya uchunguzi wa kamati yake hayataaminika na jamii .

Kwa mfano , alipokuwa Mbunge wa Kyela aliwahi kuwaaminisha wananchi wa Jimbo hilo kwamba ATAWATAFUTIA SOKO LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI , lakini hadi anapigwa chini hakuwahi kutimiza ahadi hiyo
Nakubaliana nawe. Kibatala aliwahi kusema hivi, namnukuu, "Dr. Mwakyembe ni non practising Lawyer", mwisho wa kunukuu.
 
Nashangaa serikali kuunda kamati ya watu saba kuchunguza matokeo ya Law school of Tanzania.

Hichi kizazi cha malaptop huku kichwani hamna kitu?

Angalia hata wakihitimu wanavyokuwa weupe vichwani. Sasa wanafeli kihalali wanabaki kulalama.

Huu ni upuuzi
Kuna wanafunzi form six mwaka wa Jana,hawawezi kuandika hata sentensi moja ya kiingereza eti nao walifaulu.Janga linaanzia NECTA.
 
SABABU KUU ZA TATIZO:

1. Vyakula hovyo/vya kisasa, Watoto hawanyonyeshwi zaidi ya miaka miwili ili kukomaza afya ya ubongo na kinga + makuku mataira + miyai yao + mipiza, mibaga, michipsi mfano ubongo wa samaki + viini vya mahindi yasiyokobolewa + ufuta + parachichi + ndizi hupelekea kujenga akili nzuri sana kwa kumbukumbu na uelewa mpana.

2. Maadili mabovu tokana na malezi hovyo ya house maids sababu wazazi wako bize kutafuta pesa 24 hrs kwa wiki tokana na motives ya "HAKI SAWA" hivyo hupelekea wazazi kutojua Watoto wameshindaje kiafya, kimichezo na huenda hata wamenyanyaswa kijinsi (kubakwa + kulawitiwa + vitisho vya uhai).

3. Utandawazi, nyimbo hazina maadili kusikiliza hata kuzitazama videos zake + simu janja kuachiwa watoto + makundi mabaya ya urafiki + mazingira ya malezi mabovu.

4. Malezi ya mzazi upande mmoja (single mothers & fathers) mtoto hukosa kujiamini kisaikolojia kwa kutopata upendo wa wazazi wote wawili akijilinganisha na Watoto wenzake wa malezi ya pande 2 + sumu toka kwa single mothers.

5. Uzungu mwingi, watoto waliozaliwa miaka ya 60 - 89 wamestaarabika sana sababu ya "sticks and carrots caring systems" yani Mtoto akikosea anadhibiwa papo hapo na akifanya vizuri anatunukiwa zawadi/pongezi, siku hizi huu mfumo tumebakiwa nao wahenga pekee.

6. Kukosa uchaji wa Mungu(nguvu za kiroho) Bila maombi ya kiroho na nguvu za Mungu malezi ya watoto ni changamoto kubwa sana kwa wazazi, ijulikane shetani yupo kazini 24 hrs akitumia mawakala wake(Watu wasiomcha Mungu) kurushia Watoto mapepo wachafu.

Ndiyomaana unawezakuta Mtoto yuko vizuri sana shuleni kiakili ghafla akakataa shule hataki kabisa kusoma, au akapofuka macho kimiujiza.

7. Kukosekana kwa Mazoezi mashuleni, mazoezi huchangamsha ubongo kuwa hai kiutendaji wa akili wakati wowote, mfano enzi zetu tulikuwa tunakimbia mchaka mchaka shuleni na tukirudi home tukishamaliza kazi ni michezo lakini muda wa twisheni uko pale pale.

MAISHA NI WEWE NA KUPANGA NI KUCHAGUA.
Barikiwa mtu wa Mungu. Uko sawia kwa 100%
 
Nashangaa serikali kuunda kamati ya watu saba kuchunguza matokeo ya Law school of Tanzania.

Hichi kizazi cha malaptop huku kichwani hamna kitu?

Angalia hata wakihitimu wanavyokuwa weupe vichwani. Sasa wanafeli kihalali wanabaki kulalama.

Huu ni upuuzi
Mleta uzi inaoneka haujawahi kuoita elimu ya juu, ndio maana unashadadi. Na kushangilia
 
Ni ujinga tu kuamini kufaulu wachache ndio kigezo cha kufaulu kihalali.
 
Hapa una maaana Gani. Hyo mwamba hastahili kusomea uanasheria au?? Au kufeli Kwake ni kwasababu ya kuwa mwl shule ya msing
Issue hapa siyo kufundisha shule ya msingi bali ni ile hali ya kustruggle kwa miaka 7 anatafuta digrii ya sheria halafu eti aje kuwa na ufaulu LST itakuwa ni kichekesho
 
Msingi mkubwa wa tatizo ni siasa kuwa ndio kuwa kipaumbele katika nchi hii kwa kwa ccm kuwekeza kwenye ujinga.

Sio huko tu kwenye matatizo, fani zoooote hali ni mbaya. MD anasoma miaka mitano na mmoja wa intership jumla miaka 6, akienda kazini hata kupasua jipu hawezi. Nenda kwa mainjinia hali ni hiyo, nenda ualimu hali ni hiyo.
Hilo ni tatizo la kitaifa kwa fani zote.
Matokeo yake hata profesa anaenda kugombea u diwani, u wenyekiti wa ccm wa wilaya, ubunge, n.k

Hakuna msingi mzuri kwenye shule za msingi kama neno lenyewe linavyomaanisha. Mtoto anachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hata jina lake kuandika ni mtihani, huko mbele ataweza nini?

Bado tuna safari ndefu hadi tutakapojitambua.
 
Kwa hyo hUyo mhitimu hamna imani naye??, Naye si anajua msoto wa LST
Mhitimu siyo mwanafunzi kimantiki hawezi kuwakilisha kundi la wanafunzi. Sijasema hafai kuwemo kwenye jopo bali si mwanafunzi.
 
Hapa una maaana Gani. Hyo mwamba hastahili kusomea uanasheria au?? Au kufeli Kwake ni kwasababu ya kuwa mwl shule ya msing
Ana maana kwamba shule ya huyo mtu ni ya kuungaunga mno, hivyo siyo rahisi kufanya vizuri hapo Law school ambapo vipimo vyake vimekaza sana.

Sir robby
 
Back
Top Bottom