Dkt. Mwigulu asema Nchi haiwezi kupigwa Tsh. 30 Trilioni wakati Bajeti yetu haivuki Tsh. Trilioni 50, Mpina asema Waziri hajui lolote

Dkt. Mwigulu asema Nchi haiwezi kupigwa Tsh. 30 Trilioni wakati Bajeti yetu haivuki Tsh. Trilioni 50, Mpina asema Waziri hajui lolote

ana-1-71.png

Upigaji wa CCM unaathari kwetu sote Watanzania.
 
Mwigulu amekuwa akihenyeshwa na Mpina karibia miezi sita mfululizo, hana hamu kabisa na huyo jamaa.

Huyo Mbarawa ni sawa na mdoli tu wa Samia, hata yeye binafsi naamini anajua kabisa hastahili kuendelea kuwepo kwenye hiyo nafasi, amshukuru dada yake anayemlinda.
Kumbukumbu zangu zinaonesha mbarawa alikua Waziri wa jakaya na magufuli
 
huyu nae sjui anaumwa anaijua trilioni 280 huyu jamani..?
Namba ni tatizo kwa wengi.
Ni watu wachache sana wanaojua hesabu.
Hata hivyo, muhimu ni kuwa ukisikia kelele za mbwa, elewa kwamba kuna tatizo, chunguza na chukua hatua.
 
Mpina nimwizi katuibia wavuvi na kutuweka katika maisha magumu sana
 
Hakuna jitu jinga kama Mpina, lenyewe ndio halijui kitu. Namfahamu tangia kaiwa Mzumbe huwezi kwa namna yoyte kumlimganisha hata kwa tone na Mwigulu.

Huwa linaongeaga kwa jazba kukosa uwaziri, shida ni kwamba halina impact ktk nchi hii. Amesharudisha yale mashamba alowadhulumu wananchi kule Morogoro?
Kwanini usishambulie hoja yake?
 
Wote wezi tu ndio maana hawamchukulii serious. Ni sisi wananchi tusiokua na akili ndio tunamuona Mpina ni mzalendo!! Huyu Mpina anayetaka ripoti ya CAG iheshimike huko nyuma aliwahi sema inatumika kumchafua JPM na alikua mmojawao waliotaka CAG Assad achukuliwe hatua na bunge!! Cha ajabu leo hana uwaziri ndio anaamini ripoti za CAG?

To hell
Hoja yake vipi?

Huu upumbavu wa watz badala ya mtu ashambulie hoja anaanza kushambulia mtu alietoa hoja!
 
Mpina kasema akiwa bungeni au nje!?..aje nje ya bunge aseme hivyo,wakisema bungeni hawashitakiwi,wanaropoka tu
Ulitaka asemee wapi ? Mpuuzi ww!! Au unanufaika na wezi?[emoji706][emoji706]
 
Mbunge Mpina asema hii nchi inapigwa kila kona na zaidi ya Tsh. 30 Trilioni zimepigwa na nyingine zimesafirishwa/ kutoroshwa nje ya nchi.

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba PhD amesema anachosema Mpina hakiwezekani kwa sababu Bajeti ya nchi haizidi tsh 50 trilioni.

Mpina ameomba Waziri Dr Mwigullu PhD na Prof. Mbarawa Wakamatwe na kufungwa kwa Uhujumu Uchumi.

----
Hivi ndivyo ilivyokuwa ndani ya Bunge, leo Novemba 3, 2023 wakati Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina alipokuwa akichangia hoja kisha kujibiwa na Mbunge na Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba kuhusu upigaji wa zaidi ya Tsh. Trilioni 30.
Kwani fedha na Mali za serikali zinazaanza kuhesabiwa kwenye bajeti ??
Je Kama zinaibiwa kabla ya kufika Hazina kupitia ?
Je rasilimali zingine zinazoibiwa ambazo haziko kwenye bajeto
 
Hoja yake vipi?

Huu upumbavu wa watz badala ya mtu ashambulie hoja anaanza kushambulia mtu alietoa hoja!
Hatutaki unafiki wenu kama alishasemaga ripoti za CAG ni za kumchafua JPM basi aendelee kuamini hivyo sio kisa kakosa uwaziri ndio anajifanya kumtambua CAG
 
Lile jiwe la kito cha thamani lililoibukia Dubai na zile nyara za serikali zilizokamtwa Australia !!! Huo sio upigwaji?
 
Hakuna jitu jinga kama Mpina, lenyewe ndio halijui kitu. Namfahamu tangia kaiwa Mzumbe huwezi kwa namna yoyte kumlimganisha hata kwa tone na Mwigulu.

Huwa linaongeaga kwa jazba kukosa uwaziri, shida ni kwamba halina impact ktk nchi hii. Amesharudisha yale mashamba alowadhulumu wananchi kule Morogoro?
Wewe una chuki kwa Mpina, ujinga wake ni upi? Ungetuletea ushahidi kuwa hakuna pesa inayoibiwa watu tungekuelewa, lakini hii ya kumshambulia bila sababu ni chuki binafsi, je CAG aliyetoa report juu ya upotevu wa fedha ya serikali nae hana akili?. Unamtetea Mwigulu, una uhakika gani kuwa haibi? Hiyo ya Mpina kutokuwa na akili umesema ulisoma nae, je Mwigulu unaedai ana akili, je, nae ulisoma nae? Mpina angewezaje kusoma na kumaliza Mzumbe kama hakuwa na akili?
 
Wote wezi tu ndio maana hawamchukulii serious. Ni sisi wananchi tusiokua na akili ndio tunamuona Mpina ni mzalendo!! Huyu Mpina anayetaka ripoti ya CAG iheshimike huko nyuma aliwahi sema inatumika kumchafua JPM na alikua mmojawao waliotaka CAG Assad achukuliwe hatua na bunge!! Cha ajabu leo hana uwaziri ndio anaamini ripoti za CAG?

To hell
Two wrong don't make a right
 
Back
Top Bottom