Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Tumshukuri Mungu kwa uponyaji na Tuendelee kumuombea. Huku kwetu uswazi MTU akiumwa sana halafu akaja kupata nafuuu lazima muwe naye karibu sana. Sijui inakuwaje!
 
..katika mazungumzo yake na waandishi wa habari Waziri wa Fedha Dr.Mpango amesema alitumia mtungi wa oksijen kwa muda wa wiki 2 kabla hajahamishiwa hospitali.

..sasa kwasababu huduma hiyo inaelekea ilikoa maisha ya Dr.Mpango, kwanini serikali isifikirie kuzipatia kaya zote mtungi wa gesi kama tahadhari dhidi ya ugonjwa wa korona?

..isije kuwa VIONGOZI wana MITUNGI YA OKSIJEN majumbani kwao halafu wanatuhamasisha wananchi tujiachie tu bila kuchukua tahadhari zozote.

 
..katika mazungumzo yake na waandishi wa habari Waziri wa Fedha Dr.Mpango amesema alitumia mtungi wa oksijen kwa muda wa wiki 2 kabla hajahamishiwa hospitali...
Kwani huyu naye alikuwa anasumbuliwa na corona?
 
Huyu Mzee bado anaumwa hata Sura yake na sauti inatia mashaka.

kama mtungi wa Gesi umepungua mwambieni akajazie tena akae standby maana muda wowote anaweza kurudi tena
 
Huyu waziri atakuwa amemkosea sana Mkuu wake. Angekaa tu Mungu amponye.

ANGALIZO:
"tusimjaribu Mungu" Askofu Ruwaichi.
 
Amevuka hizi wiki mbili mlizomzushia kifo.
Hivi kifo kinachouma ni Cha mwana CCM tu? Sisi wapinzani tukiuwawa ni Kama kafa mbwa siyo?

Ok tambueni Mungu Ni wa wote na msidanganywe na pesa na madaraka; hivyo ni vya kupita tu na mtaviacha mda mchache ujao.
 
Nilikuwa na agenda yangu siku kadhaa huko nyuma but ilipelekea kupigwa burn.
👇🏾
Vaa barakoa na unawe mikono kwa sabuni na maji tiririka pia ukae mbali na mikusanyiko.
 
Utakuwa mpumbavu kudhani utapendwa na kufurahiwa na wote. Hao waliofurahia kuugua kwake na kutaka afe ni asilimia ngapi ya watanzania?!
Embu ipigwe Kura huru utajua tu Ni asilimia ngap!
 
..Yap!!

..wananchi tunaambiwa tumetegemee MUNGU peke yake.

..wakati VIONGOZI wanategemea MITUNGI YA OKSIJEN, baada ya hapo ndio wanamlilia MUNGU.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Kwanini unaruhusu chuki kuugubika ukweli!? Hakika hiyo ni hatarii kubwa kwa afya ya akili yako.
 
Back
Top Bottom