Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Naanza kuamini sasa 90% ajali uzembe wa madereva nimefatila ripoti karibu mwaka sijasikia gari binafsi au basi la abiria limepata ajali sababu sijui tairi imepasuka sijui breki lilifeli kila saa mtu alikua anapiga blind overtake....

Mtasema miundombinu waeke double road ila ndio hakuna double road tuwe makin sasa
 
Mengine hatupaswi kumlaumu Mungu, je chombo kinafanyiwa regular services kwa wakati? Na je? Dereva anapata muda wa kupumzika? Nk nk. Tuyatazame kwanza hayo na ajali zitapingua.
Utafiti unaonyesha kuwa, tatizo la kwanza linalosababisha ajali ni uzembe/ujinga/upumbavu kwa madereva. Hili linachukua 85%. Mtu anaambiwa asiovertake kwenye kona, ambapo haoni mbele, lakini yeye anaovertake. Tatizo la pili ni ubovu wa vyombo vyenyewe (magari). Hapa shida ni kutofanyiwa service vyombo hivyo, na uchakavu wa magari. Hili linachukua 10%. Na tatizo la mwisho ni madawa ya kulevya; hapa kuna pombe, mirungi, cocaine, nk. Mtu akitumia vitu hivi kwa kiasi kikubwa, hawezi kuwa na maamuzi sahihi. Hili linachukua 5%.
 
Naanza kuamini sasa 90% ajali uzembe wa madereva nimefatila ripoti karibu mwaka sijasikia gari binafsi au basi la abiria limepata ajali sababu sijui tairi imepasuka sijui breki lilifeli kila saa mtu alikua anapiga blind overtake....

Mtasema miundombinu waeke double road ila ndio hakuna double road tuwe makin sasa
Siku hizi tairi kupasuka aileti madhara sana kutoka mwendo sio mkali sana siku hizi.shida imebaki kwenye haraka za Ku overtake
 
HIVI KWANINI ASITOKEE KIONGOZI KICHAA AKAWEKA 'LIZEGE' LIKUUUBWA KATIKATI (NJIA MBILI) ILI HUU UPUMBAVU WA HAWA MADEREVA NA BAADHI YA ABIRIA WAO UNAOSABABISHA MAJANGA YENYE KUTESA KAMA HAYA UKAISHAAA?!!!

TULE MIHOGO HATA MIAKA MITATU LAKINI HILI LINGEFANYIKA KWA KESHO BORA YA WATU. SASA HIVI KUNA WENGINE TUKISAFIRI HATUONGEI (KWA SABABU YA WASIWASI) HADI TUNAFIKA.
 
Back
Top Bottom