Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Na itakuwaje kwa wale wasio mwamini Yesu e.g. Dini nyingine; Wapagani na hata wale wasioamini uwepo wa Mungu?
Ipo hivi Mkuu,ukiaoa au ukiolewa na mtu ambaye nafsi yake haijakombolewa na Kristo Yesu jiandae kwa lolote wakati wowote!. Hata kama awe ni kiongozi wa dini. Hata kama awe anakesha makanisani. Hata kama awe mshika dini wa dini zote zilizopo hapa duniani. Narudia tena oa au olewa nae at your own risk!. Huyu ni ticking bomb. Kulipuka ni obvious!

Mtu ambaye hajakombolewa ugonjwa unaoitwa "ubinafsi" umetanda moyoni mwake hivyo uwe na uhakika with time na life circumstances lazima sumu yake itakukaanga tu. Lazima!

Yesu ndiye pekee mwenye uwezo wa kuifix nafsi ya mtu ili awe mwenye kuwapenda wengine kama anavyojipenda yeye!. Sio Elimu,sio Maarifa,sio fedha,sio cheo wala chochote kinachoweza kufanya jukumu hili isipokuwa ni Kristo Yesu peke yake. Mkuu Mungu amekupa utashi ukiweza tenga muda wako kisha chunguza kwa makini kabisa nakuhakikishia utakuja kuubaini ukweli wa hiki nilichokiandika hapa!


Mkuu haya mambo yanasumbua dunia nzima na yataendelea kusumbua sana tu kwa sababu majority ni watumwa wa dhambi. Nafsi zao hazijakombolewa!.

WARUMI 7
14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.

17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
 
Dini/imani na mwanadamu ni kipi/yupi mkuu kuliko kingine?
Wokovu watoka wapi?
 
Dini/imani na mwanadamu ni kipi/yupi mkuu kuliko kingine?

Wokovu watoka wapi?
Wokovu unatoka kwa Mwokozi Yesu:

YOHANA 8
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.

ISAYA 61
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
 
Unachokizungumza sio cha kizazi hiki uwanaume na ukike ulikuwa zamani.
Hii ni zama wa 50/50 kwa lugha rahisi wanaita zama ya usawa .
Wakati wewe unataka kusimama kama mwanaume mwenzio anaona unaenda kinyume na zama,anataka usimame kwa haki sawa na sio kwa ujinsia.

Zama za hovyo wakati wewe unapambana uwalee wanao kwa mfumo wa kiume na kime ulimwengu unamfunza katika usawa.
Mambo yaliyokuwa ya kike ulimwengu wa sasa unamfunza hata mwanaume kuwa ni sawa hata yeye kuwa kama mwanamke kupelekea ushoga usagaji nk.
Makelele kujibishana baina ya wanandoa kwa kigezo cha usawa.
 
Asilaumiwe mwanafunzi; mwalimu atimize wajibu wake.
 
Ishi nao kwa akili
 
Mwalimu akishafundisha(habarisha) na mwanafunzi akaelewa basi wajibu wake unakuwa umeishia hapo.

Kuzingatia na kufanyia kazi unabaki kuwa ni wajibu wa Mwanafunzi mwenyewe!
Nakubaliana na wewe. Ila baadhi ya walimu chini ya kiwango!
 
Cheche huzaa Moto
 
Hili janga ni zaidi ya utekaji, inabidi jitihada za kimakusudi zichukuliwe kunusuru taifa.

Ni kama roho imeibuka na kusambaa ikiwapagaa wanaume kuanza kuzoea kuua na kuona ni kawaida na inawezekana.

Kwani hawa wanawake wameanza kua na inayodaiwa tamaa ya mali au tabia mbaya miaka ya hivi karibuni?

Mkishindwana si bora muachane kwa utulivu bila kuathiri mustakabali wa watoto na familia kwa ujumla!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…