Wapo Waislam wenye wake zaidi ya mmoja na wanazini kama kawaida,ni upuuzi kulihusisha tukio hili na dini ya mtu.
Iko hivi SHERIA ya kuoa mke mmoja imepokelewa juu juu na Waovu Kwa Nia ovu. Na ikatangazwa na Waovu Kwa Nia ovu.
Ukristo ni Daraja la juu saa la Imani.
Ukristo ni umasihi. Ni juu ya ufalme. Wakristo halisi sio Hawa tunaowaona ambao ni wafuasi wa shetani waliojivika Vazi la Ukristo.
Ukristo halisi ni Imani ngumu sana . Ukristo halisi ni kujikana na kuutiisha mwili na dhambi muda wote . Ukristo halisi hauwezi kushindwa na mwili mana Roho Mtakatifu anakua ndani ya mtu hivyo anakua ameufisha mwili na tamaa zake .
Mkristo halisi ni yule anayeweza kuuambia mwili wake acha hiki na mwili ukatii. Zaidi ya hapo ni watu waopaswa kuwa Chini ya SHERIA kama Ile ya Musa ambayo inawaongoza Waislam Leo na wengi watagaulu Kwa kufuata SHERIA iliyoko kwenye Korani na Tourati ya Musa.
Huwezi kuwa Mkristo kamili basi simama katika Sharia .
Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu ili awapate watakatifu watakaotawala pamoja naye kule Mbinguni . Hawa watakua kama Malaika kwani hawataoa Wala kuolewa kule Mbinguni . Wataamza hapa Duniani Kwa ama kuoa mke mmoja TU kama Adamu wa kwanza alivyokuwa au kutooa kabisa bila kufanya uzinzi. Leo Kuna makristo wa uongo hawajaoa au kuolewa lakini ni wazinzi wa kutupwa. Hao nafasi yao ni katika Lile zizi liwakalo moto na Kiberiti.
Wale wakristo wa kweli Hawapaswi kamwe kujihusisha na mambo ya uzinzi mana watatakiwa kwenda Kukaa Mbinguni karibu na Mfalme na Mbinguni hawatakiwa kamwe kuingia viumbe vyenye hulka ya usaliti na kukosa utii . Kusema una ndoa ya mke mmoja na mume mmoja Kisha ukaanza kujihusisha na uchepukaji ni kwamba huna sifa kamwe ya kuingia Mbinguni hata kama unatoa sadaka na kusali sana . Hapo utakachopata ni kwenda Peponi kama matendo yako yatakua mema na ukawa umetubu mazambi yako.
Waislam kamwe hawawezi kuingia Mbinguni kutawala poja na Kristo mana hawakumpokea Yesu Kristo katika Imani na kupokea Roho Mtakatifu. Ila Waislam wenye matendo mema wataishi Peponi na kupata maisha ambayo ni Bora kuliko haya ya Duniani . Kule wataruhusiwa kuoa Wanawake sabini . Watakua ni raia wa Peponi .
Na pia Kuna baadhi ya wakristo waliomwamini Kristo na kutubu madhambi yao watakaa nje ya hema la Mbinguni wakiwa kama Chawa wa Wakristo watakaokuwa wanatawala pamoja na Mfalme Yesu Kristo . Watakua ni wapambe wa Ufalme .
Mkristo halisi hata umshikie panga kamwe hawezi kuikana Imani ya Kristo sembuse kuendeleza zinaa . Hawa wanaojifanya Wana mke au mume mmoja halafu Wana michepuko . Hao ni mawakala wa shetani na uzao wa uharibifu unatoka kwao. Ni kizazi Cha nyoka . Na mara nyingi hata wakiwa ni viongozi wa dini hua hawakemei dhambi Kwa kumaanisha na kuihubiri habari ya toba na kuwaombea watu Roho Mtakatifu ili waishinde dhambi.