Fukuza wazinzi weka waadilifu just as simple as that !!
Hii nchi imekuwa ya kujadili matukio na sio sera za nchi na maendeleo ?

Inashangaza nchi nzima vijana kwa wazee kumjadili mzinzi na sio maendeleo tuache Upumbavu wa kujadili watu na hii ni kampeni inayoratibiwa na Ccm chini ya wazee wa propaganda doesn't make sense sisi 24/7 tukawa tunajadili Uzinzi na wazinzi mara Simba na Yanga this is shit.
 
Usitegemee maendeleo kuletwa na watu wenye tabia mbaya mbaya waliokabidhiwa ofisi kubwa za Umma !! Ndio maana Nchi zilizoendelea wapo strict sana na tabia za watendaji wao ! Boris Johnson alilazimishwa kujiuzulu Uwaziri mkuu wa 🇬🇧 UK kwa sababu ya kuvunja tu kanuni ya lockdown ya Corona !!
 
Endapo tukipata ukweli je sisi wananchi wa kawaida itatusaidia Nini?
Swali lako unadhani linatusaidia nini sisi wananchi wa kawaida.Haustahili kuwepo kwenye ulimwengu wa watu wastaaarabu.Yawezekana ukifiwa unaweza kuhamua marehemu umzike peke yako na ukawauliza waliokuja kuzika je mgezika ingewasaidia nini nyie ambao sio ndugu? Nakushauri uwahi milembe.
 
4.Mpenzi wa Naibu Waziri bado hakujulikana, bodoboda waliofika eneo la ajali waliona maiti ya mwanamke.

What if huo mwili ni wa mtu aliyekuwa akitembea kando kando ya bara bara?

hapa yabidi mke wa Naibu waziri ahojiwe,
Marafiki wa mwanafunzi nao wana umbea kidogo

Huku kote twazunguka zunguka tuu .... master mind ndo mwenye jibu kamili
 
Tatizo kubwa ni kuwa Tanzania hatuna media bali waganga njaa waliofeli maisha wakaigiza ni waandishi wa habari. Hili jambo ni rahisi mno mno kupata ukweli wake tena na ushahidi usio na shaka kama mwandishi wa habari akiamua kufuatilia. Kina Pascal Mayalla kazi kuganga njaa tu.
 
Muachieni Paskali jamani🤣
 
Roho wa ukweli aliye ndani yako na akulinde.
Ukweli ni roho asiyeweza kifichwa.
 
Nyie ndo mnataka watu wapigwe ban kwa kuwatukana....
Akili yako imejaa m@vi na ubongo ulishaukunya siku nyingi
 
Ndugu Ndugange ,alikuwa daktari au MD pale Simiyu mpaka Mwaka 2020 alipojaribu kugombea ubunge Jimbo la Wagong'ombe na kushika nafasi ya tatu kupitia CCM.Walioongoza wawili kwa kuwa walikuwa na upinzani mkubwa sana ,ikabidi CCM impitishe yeye.Yaan akaokota dodo na kuwa mgombea ubunge katika hilo Jimbo la Wagong'ombe .Kumbe aliendelea kuokota dodo na kuwa naibu wazir.Oh !!Ndugu yetu amepatwa na mkosi upi tena?Tumuombee.
 
Nyie ndo mnataka watu wapigwe ban kwa kuwatukana....
Akili yako imejaa m@vi na ubongo ulishaukunya siku nyingi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hili swala limejaa akili na sura ya fumanizi zaidi kuliko tukio la ajali yenyewe hivyo pole kama utakua umenielewa vibaya
 
If true kama Taifa we are LOST !!

Ninapokutana na tamko la kijinga kama hili, nabaki tu nimeduwaa! Yaani pamoja na yote yanayotokea kila leo, tukio hili moja (ambalo hata hivyo bado una mashaka kama ni kweli) hujui kuwa as a nation we are lost!

Ni miaka mingapi toka marehemu Kolimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM atamke kuwa kama taifa tumepoteza dira? Je unakumbuka jibu alilopata baada ya kukiri ukweli huo?

WE LOST OUR WAY A LONG TIME BACK na ukweli ni kuwa kama taifa tumepotea, CCM imetupofusha macho na kutudumiza akili, hatuoni wala kuhisi hatari iliyo mbele yetu!
 
Ni sahihi waziri kutumia gari la unma kwenda kufanya zinaa?

Ni sahihi mtu kufa kifo cha utata na kusiwe na uwajibikaji wowote ?

Vipi angekuwa dada yako ndiyo kakutana na kadhia hiyo ungekuwa na mtazamo huu ulionao ?
Swali lako la kwanza, ni kweli si sahihi kutumia gari ya serikali kwenye harakati binafsi haswa kama anazotuhumiwa nazo

Swali la pili, si sawa ni lazima uwajibikaji na majibu yapatikane ila ishu niliyonayo mimi kwenye kutaka kuelewa ni kwanini huyo dada kahusishwa moja moja na hii ajali na si mtu mwingine!!? As if kuna watu wana uhakika wa moja kwa moja, je huyo muheshimiwa kama alikua na mwanamke mwingine kwenye gari na si huyo dada kama wanavyo shutumu!!?

Sijui kwanini wa cover ila najaribu kutomuhusisha huyo dada na hiyo ajali labda mpaka uchunguzi ufanyike ila sio kuhukumu moja kwa moja

Bahati mbaya wengi hawajanielewa tangu awali, ni hisia zangu zisizo na ushabiki wowote kama watu walivyo egemea kwenye fumanizi zaidi na kuwaunganisha hawa watu moja kwa moja.

Kweli kuna huyo dada wa chuo kapotea na kupatikana akiwa hana uhai bila taaharifa za kina ila sizani kama ni sawa kumuhusisha moja kwa moja na ajali hiyo, pengine hakuwemo humo kwenye ajali
 
Hakuna jeshi linaloyumbishwa na wanasiasa kama Polisi! Sijui nani atawasaidia Polisi waweze kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na sio maagizo kutoka juu.

Mbona JWTZ kuna adabu? Why makamanda wa polisi msiweke heshima ya jeshi hili? Waambieni hao mawaziri watoe amri isiyo halali kwa kamanda wa JWTZ muone!

Hili sakata limeyumba sababu ya maagizo maagizo kama kawaida. Hizi spinning mnataka kumuokoa nani? Kwanini hii aibu isiondoke na chain yote ya command huko Dodoma kuanzia Mkuu wa Mkoa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa?

Mambo madogo mnapoteza nayo muda wakati mnakazi nyingi za kupambania umma. Raia mmoja kisa waziri mnakimbizana utafikiri ni Rais!
 
Katiba mpya ni muhimu !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…