Kuwaweka wanafunzi makambi na kurudi hiyo saa 12 ni kupoteza muda.....

Tufanye wanafunzi wakeshe kwa ajira gani?

Sisi tulikesha sana, mwisho wa siku tupo wapi?......

Kunamaisha nje ya elimu, mtoto arudi hiyo saa 9, ajifunze vitu vya ziada kama kupaka rangi, kutengeneza bustani, kujifunza ufundi wa baiskeli na magari, kujifunza ufundi uwashi.....

utamtoa saa 12 baada ya miaka 8 (form 1 - chuo) anakuwa anasjinda chumbani na laptop kusubiria ajira, hajui hata kutengeneza tuta.....

Tutengeneze mazingira mazuri ya mtoto kuwa serious na elimu kwa muda stahili na pia kupata muda wa kujifunza stadi za maisha...

Kuna mafundi wazuri wa tv, kuna graphic designers, kuna wakulima wazuri walijifunza mda wa ziada.....
 
Mkuu wa mkoa yuko sahihi, Ndalicho, Dr Dorothy Gwajima,Dr mollel, RAS shinyanya, RAS mwanza,RAS Geita, RC manyara,DED same, Kaimu DED Moshi manispaa, Hawa ni viongozi mzigo awamu ya SITA.
Mkuu umetumia vigezo vipi kuwaona hao ni mizigo? TUELIMISHE.
 
Jitahidi kutofautisha mambo
Nani kakataa watoto wasiende likizo?.

elimu hata ya chuo kikuu baada ya lecture lazima ujisomee binafsi ama kama kikundi

kuna shida gani mwanafunzi wa Sekondari kujisomea binafsi au kama vikundi mara baada ya masomo ya kawaida?

past paper mtasolve muda wa vipindi vya kawaida?homework huwa inafanywa sa ngapi?

sioni kama Elimu ina shida kiasi hicho ila wasilazimishwe kutoka sa 9 kama watu wanaridhia kuweka kambi muda wa ziada wasome
 
Kwa hiyo watoto wa Mtaka wenyewe wako shule za kata na Wana mazingira sawa na wa anaowahutubia 😁!

Ni heri hao wananchi wakawapuuza wote,Waziri pamoja na Mtaka then wawasikilize viongozi wao wa mitaa na vijiji ambao wanaishi miongoni mwao.

Uwasilishaji mbovu sana,sitoshangaa Bimkubwa akimpiga chini.

BTW:Waziri kawaambia nini wanaDodoma kuhusu saa Tisa?
 
Tatizo mawaziri wanapenda kuingiza siasa kwenye kila kitu
 
Hivi debate ama clubs za masomo nk ni kitu cha kila siku?

mbona tulijisomea extra hours na michezo tulicheza siku za michezo na usafi tulifanya kila siku na debate na clubs pia zilifanyika kwa siku husika
Ratiba za watoto zipangwe kuaccomodate na kujua activities zote
Inawezekana...ila kikubwa zaidi wapate maarifa ya shule
 
Sio privatezote ni shule za bweni, au unamaanisha hadi shule za kutwa(day) nazo wanasoma hadi usiku?
Sasa hawa wa day hawasomi shule usiku bado unataka watoke sa 9 ili?.

ndo mana on average shule za boarding wanafaulu kuliko day
Muda mwingi ni kusoma.,ratiba binafsi kidogo na michezo
 
Hat shule wanazofundisha vizuri watoto wanasoma mchana na usiku juu

ama mnadhani wanafaulu kimiujiza?
Hakuna miujiza kazi yao ni kufundishwa na kujisomea over
 
Na huo ndo ukweli huyu kazoea makambi ya KISABATO ndo anataka wanafuzi wakae makambini yani nchi nzima kila mkoa makambi? Nini maana ya madarasa. Hapa cha msingi serkali iboreshe mazingira ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na kuboesha masrahi ya walimu.

Haya mambo ya kuhangaisha watoto kwenye makambi bado ni temporary solution, Watu wenye akili kubwa hiyo haiwezi kuwa mwafaka wa elimu yetu kwangu mimi binafsi naamini mtotot akifundisha vizuri masaa 9 yanatosha, pia wakumbuke shule sio kusoma tu pia kuna suala la vipaji vya watoto kuendelezwa kama mpira,uigizaji na talent zingine pia.

Inamaana mkuu wa mkoa anataka watu wote wawe na division one na two ili kufurahisha wazazi wakati product yake bado ni sifuri kutokana na ukosefu wa ajira.

Tatizo la elimu yetu ni kukariri ndo maana tunalazimisha watoto wasome mpaka usiku wa manne kukariri makaratasi.
 
Umeandika vizuri.
Elimu yetu ina matatizo makubwa.
Nakubali.
Mwenye jukumu la kuyatatua haya matatizo makubwa ni Waziri wa Elimu.
Asaidiwe namna ya kuyatatua.
Mahali pazuri pa kuanzia, ni kuwasikiliza Viongozi wenzake wenye uchungu na Elimu, wakiongozwa na Anthony Mtaka.
Badala ya Waziri kutoa matamko hadharani ambayo nayo pia yanajibiwa hadharani, alitakiwa akutane na Wadau, wazungumze, asikilize kwa nini zinawekwa Kambi za kujisomea, kisha akirudi Ofisini kwa PhD wenzake, wachakate walichokipata ili kutatua matatizo.
Matatizo ya Elimu hayawezi kutatuliwa kwa amri za Kipolisi za kufuata sheria pasipo shurti.
 
Naona staili ile ile ya Dialo ya kutema nyongo. Nahisi kuna kitu hakipo sawa baina ya viongozi hawa na kauli hizi. Kuna haja ya kutoa miongozo juu ya nani wa kusemea mambo yanayogusa maslahi makubwa ya wananchi kama hili la elimu na si kupingana hadharani hivi.
 
Kama nimeelewa vizuri ELIMU ya Tanzania inamatatizo haiko sawa kwamba tayari kuna tofauti ya elimu anayopata mtoto maisha bora na mtoto maisha duni/kawaida. Kikawaida mfumo wa elimu unategemea muda, mazingira, rasilimali na nyenzo zingine. Je hivyo vyote vipo au vinatosheleza kwenye utoaji wa elimu Tanzania?, Hao watoto wa mawaziri, maRC sijui wakurugenzi au hata watu wenye uwezo wananafasi kubwa kupewa elimu nzuri kutokana na uwekezaji kwenye vitu hivyo muhimu. Serikali ya Tanzania ingekua kweli ina uchungu na kizazi cha watoto wa Tanzania wangewekeza zaidi kwenye elimu kuliko mambo kama sijui mwenge, maslahi makubwa kwa viongonzi wa kisiasa, uchaguzi usio huru na haki yaani ikiwezekana waacha kununua magari ya kifahari pesa wapeleke kwenye ELIMU ELIMU ELIMU
 
Mimi napenda sana viongozi wanaothubutu ku challenge status quo. napenda sana.
 
Amesema ukweli bila kupepesa macho. Bravo Honourable Mtaka. The best RC in Tanzania
 
Waziri yupo sahihi,

Muda wa kazi wa Serikali ni saa tisa na nusu.

Waziri kafuata sheria ya kazi ilivyo.

Kinyume na hapo ni fujo.

RC amemkosea heshima Waziri.

Hakupaswa ajibu.Angepiga kimya na akaendelea na mipango yake kimya kimya tu.
Wewe umesoma shule za kina Junior ndio maana tuulize sisi tuliosoma Kayumba tukusimulie ugumu wa hii elimu ya huku kwetu.
 
Hapa nimekukubali mkongwe. BTW ameomba radhi kiungwana. Tusahau tusonge mbele. Ni mtu mwema na mchapakazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…