Amejiharibia sana huyu, hajaweza kudhibiti ulimi wake, yawezekana nia yake ni njema lakini hajatumia diplomasia kumnanga kiongozi mwenzake jukwaanni
Naamini anayo sababu ya msingi sana mpaka kufikia maamuzi ya kumlipua waziri hadharani.

Hawa mawaziri sometimes wanajikuta tu washakuwa wao ndio wanajua kila kitu
 
Mkuu wa Mkoa alichafukwa na nini, mbona katoa povu kubwa mbele ya Umma.

Alikosa kutumia lugha ya alama?? Anataja hadi cheo cha anayemkusudia tena mbele ya kadamnasi?

Ujumbe umefika in a hard way. Nlitegemea haya yasemwe na "wapinzani"

Ayway hii ndio inaitwa CALL A SPOON A SPOON
 
Naamini anayo sababu ya msingi sana mpaka kufikia maamuzi ya kumlipua waziri hadharani.

Hawa mawaziri sometimes wanajikuta tu washakuwa wao ndio wanajua kila kitu
Ni kweli Ndalichako ni wa hovyo sana, lakini Tony naye angetumia lugha ya kidiplomasia kidogo kwakuwa watz wa siku hizi wanaelewa kwa haraka.
 
Huyu mtu yuko wazi sana and he is very strong, yaani hafichi hafichi ujumbe. Awe mwangalifu tu kwamba ujumbe wake usije ukamgeuka vibaya. Maana sasa kupingana waziwazi ndani ya Serikali nadhani siyo kitu ambacho hata mamlaka za uteuzi zinaweza kukivumilia
 
wajuzi watujuze kwanza watoto wa RC mtaka wao wanasoma wapi shule gani anuai....? au kiongozi yeyote cabinet minister , RC au mtunga sera yeyote mwenye kutembelea kiyoyozi au bendera yeye watoto wake wao wanasomea wapi shule gani za kata au serikali msingi na sekondar?
 
Wengine wameajiriwa na serikali lakini sisi raia tunaambiwa tujiajiri mana serikali haina nafasi.

Nasikia Mhe. Joyce Ndalichako ana mtoto mmoja na alifeli chuo, wajuzi ni kweli hayo.?
Mkuu huyo akifeli chuo hafeli maisha maana connections zipo nyingi tu kama JESCA
 
Ndalichako alikua best student enz zake huko sekondari...yaan Tanzania one...shaur yako.
 
Syllabus ipo, Work plan ipo, huhitaji kukaa hadi saa 10.

Sheria inataka mwalimu asilazimishwe kukaa overtime na hata akikubali alipwe overtime.

Sasa umlipe overtime wakati mshahara tu mbinde.


Nchi moja mazingira ya shule yanatofautiana halafu unataka wote wafanye kama yellow buses. Mwisho wa mchezo watoto wetu wanaondoka na mayai viza. Nooooo. Big up RC
 
Wajinga hawa. Mwanafunzi anatakiwa kuelewa kwa muda wa darasani.

Ukiwazoesha waelewe kwa muda wa ziada basi chuo kikuu wataukosa na kazini wanaukosa.

Solution ni kulipa vizuri walimu wawe na moyo wa kufundisha muda wa darasani.


Mnachosha watoto kuwasomesha masaa mengi hivo
 
Achilia mbali overtime, hata salary yenyewe mbinde hadi mwalimu anakosa hela ya kiatu.


 
H
Hiyo mipango yake ndiyo iliyoipaisha simiyu. Siku wakifeli mtamlalamikia Mkuu wa Mkoa. He's right and he's my support. Go Anthony.
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Nchi hii inayumba sana kwa sababu ya kuoneana aibu. Anthony has made it. Development is integrated with difference in opinions. Na hakuna kuambiana huko ofisini. Tell it in broad day light. Joyce amemkera sana Anthony I hope. Hata mimi ningemjibu hivyo hivyo zaidi ya Anthony. Watoto wakifeli RC ndiye anasakamwa. Remember, waziri ni policy tu lakini utendaji uko TAMISEMI kwa akina Anthony. Niliwahi kusema kuwa wakuu wa mikoa watakaofanikiwa ni Anthony, Kafulila, and Queen.
 
Ndalichako ni "status quo" na mtaka ni "mlevi wa madaraka" wote wana mazuri yao na mabaya yao, nchi bdo sana hii, tuvumiliane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…