View attachment 2060577
Papa Francis akiwa mimbari
I. USULI
Kitu kinachowaunganisha wanajumuiya ni imani ya pamoja kuhusu vitu vinavyoonekana na visivyoonekana (belief), kanuni za kimaadili zenye kutamko miongozi na miiko kuhusiana na matendo binafsi na matendo ya pamoja wakati wa kutekeleza ajenda ya pamoja (norms) na tunu zinazotoa msingi wa matumani ya wanajumuiya (values).
Katika Ukristo, Imani inatamkwa katika Kanuni ya Imani ya Mitume, kanuni za maadili zinatamkwa katika Amri Kumi za Musa, na Matumani ya Wakristo yanatamkwa katika Sala ya Baba Yetu. Kwa ufupi, hicho ndicho kitako, kimo na kiegama cha itikadi asilia ya Ukristo (Christian worldview).
Kwa miaka 2000 sasa vikao mbalimbali vyamakanisa anwai ya Kikristo vimekuwa vikifanyika ili kufafanua, kutetea na kulinda mambo haya matatu. MItaguso ilitumika zamani. Lakni, siku hizo sinodi ni kikao cha aina mojawapo kwa ajili hii ndani ya Kanisa Katoliki.
Sinodi ya 16 ya Maaskofu Katoliki inaendelea tangu 10 Oktoba 2021, na itahitimishwa Oktoba 2023, huko Roma.
Tayari dodoso la kukusanya maoni ya walei na makleri limeshatolewa na kusambazwa maparokiani duniani kote. Dodoso lina maswali 51, moja likiwa swali kuu. Kwa kuzingatia ukweli huu, katika aya zifuatazo nafanya yafuatayo:
- Najadili dhamira na swali kuu la dodoso;
- Naorodhesha maswali madogo 50 ya dodoso;
- Najibu swali namba 50 katika dodo hili;
- Nadadavua dhana ya itikadi (worldview) kama zana muhimu kwa ajili ya kutusaidia kujibu dodoso kwa ufahasa;
- Natumia dhana hii kwa kufananisha na kutofautisha itikadi kuu tulizo nazo (worldview comparisons and contrasts);
- Naonyesha maeneo ya kiitikadi yapatayo 50 yenye mikanganyiko ya kimantiki (logical contradictions) na/au mikanganyiko ya kimetafizikia (metaphysical contradictions), mikanganyiko ambayo ni miongoni mwa sababu kuu za kusababisha mmomonyoko wa Kanisa Katoliki, kwa maana ya kuzalisha "Wakatoliki wastaafu"; na
- Hatimaye nahitimisha kwa kutoa mapendekezo kadhaa nikiwaalika wajibu dodoso kutumia ya dhana ya itikadi (worldview) kama nyenzo muhimu kwa ajili ya kuchuja na kutofautisha kati ya pumba za itikadi duni na mchele wa itikadi bora.
II. UTANGULIZI
Milenia mbili zilizopita ilizaliwa dini ya Ukristo, mara tu baada ya habari za ufufuko wa Yesu wa Nazareth kuenea Yerusalemu, na baadaye dunia nzima.
Na sasa dini ya Ukristo ni itikadi (worldview) inayokabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwenye itikadi mbadala kama vile Uislamu, Ubuda, Uhindu, Ukonfuchio, Ukomunisti wa Marx, Ukanamungu, Uliberali, Usekulari, na Usayansi.
Tangu wakati huo hadi leo Ukristo kupitia Madhehebu ya Katoliki umekuwa na utaratibu wa kufanya Mkutano wa Juu Kabisa wa kitaasisi uitwao Mtaguso (Council).
Ni kama ambavyo Anual General Meeting (AGM) huwa ni Mkutano wa Juu Kabisa wa Kampuni au Azaki.
Kwa mujibuwa tovuti maarufu ya Kikatoliki iitwayo New Advent, tayari mitaguso 21 ifuatayo imefanyika, miaka yake ya kufanyika ikiwa kwenye mabano hapa chini:
Nikea I (325); Konstantinopoli I(381); Efeso (431); Chalsedoni (451); Konstantinopoli II (553); Konstantinopoli III (680-681); Nikea II (787); MKonstantinopoli IV (869); Laterani I (1123); Laterani II (1139); Laterani III (1179); Laterani IV (1215); Layoni I(1245); Layoni II (1274); Vienna (1311-1313); Konstansia (1414-1418); Florensi (1431-1439); Laterani V (1512-1517); Trent (1545-1563); Vatikano I (1869-1870) na Vatikano II (1962-1965).
Kila Mtaguso ulikuwa na ajenda yake mahsusi. Kwa mfano, Mtaguso wa Trent (1545-1563) ulilenga kujibu mapigo dhidi ya Mafundisho ya Mtawa wa KIjerumani Martin Luther aliyeanzisha Kanisa Jipya la Kilutheri duniani.
Mtaguso wa II wa Vatikano ndio ulianzisha utaratibu wa Kanisa zima kukutana kwa njia ya Sinodi katika ngazi ya Kanda, Bara na hata Dunia nzima kwa ajili ya mashauriano juu ya masuala muhimu ya Kikanisa.
Tayari zimefanyika sinodi 15 tangu 1965. Na sasa Sinodi ya 16 ya Maaskofu Katoliki Duniani inaendelea tangu ilipozinduliwa na Papa Francis tangu 10 Oktoba 2021 huko Roma.
Sinodi ya 16, itakayofanyika kwa miaka mitatu mfululizo, tangu 2021 hadi 2023, inanogeshwa na kauli mbiu isemaayo “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume.”
Sinodi hii itahitimishwa Oktoba 2023 huko huko Roma, baada ya Papa atakayekuwepo wakati huo kupokea maoni ya walei, makasisi, maaskofu, makardinali, Waanglikana, Walutheri, Waislamu, na watu wengine kutoka duniani kote kupitia dodoso maalum kwa ajili hii.
Katika aya zinazofuata nafanya yafuatayo: Najadili swali kuu la dodoso; naorodhesha maswali madogo 50 ya dodoso; nadadavua dhana ya itikadi (worldview) kama zana muhimu kwa ajili ya kutusaidia kujibu dodoso kwa ufahasa; natumia dhana hii kuonyesha utitiri wa itikadi tulio nao (worldview pluralism) na migongano kati yake; kisha nahitimisha kwa mapendekezo kadhaa nikiwaalika wajibu dodoso kutumia ya itikadi (worldview) kama nyenzo muhimu kwa ajili ya kutofautisha pumba za itikadi duni na mchele wa itikadi bora .
III. SWALI KUU LA SINODI
Dhamira kuu ya Sinodi ya 16 ya Kiaskofu inabainishwa na swali la msingi katika dodoso hilo. Kwa mujibu wa dodoso husika, swali hilo ni:
- Katika kutangaza Injili, kwa njia ya Kanisa la Sinodi, waumini wanapaswa “kusafari pamoja.”
- Je, katika Kanisa mahalia la leo “safari ya pamoja” inafanyika ipasavyo?
- Je, [kama jawabu ni hapana,] ni hatua gani ambazo Roho Mtakatifu anatualika kuchukua ili tuweze [kusafiri pamoja bila kumwacha mtu yeyote nyuma na] kukua wakati wa "safari ya pamoja”?
Kwa mujibu wa swali hili, ni kama vile Papa Francis amesukumwa na Enjili ya Mwana Mpotevu. Anawaacha wale kondoo 99 na kwenda kumtafuta yule mmoja aliyepotea. Anataka kondoo wote wajiunge katika "safari ya pamoja".
Katika historia ya Kanisa, sinodi ya 16 unao upekee wa aina mbili. Kwanza, hii ni sinodi ya kwanza duniani inayoanza kwa kukusanya maoni ya waumini walei wote kwa njia ya dodoso.
Na pili, ni sinodi ya kwanza, kuwaalika watu walio nje ya Madhehebu ya Katoliki kutoa maoni yao juu ya ajenda ya Kanisa Katoliki kuhusu maboresho ya imani na matendo yake.
Yaani, Walutheri, Waanglikana, Wapagani, Wakanamungu, Waislamu na watu baki wenye manung'uniko dhidi ya itikadi Katoliki wanaalikwa kujaza dodoso na kuwasilisha mawazo yao kwa Papa Francis, kupitia viongozi wa Kanisa mahalia, ili ayafanyie kazi.
Ni jukumu la makanisa mahalia kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya maoni kutoka kwa makundi yote haya, na kisha kuyafikisha kwa Papa Francis.
Maswali madogo ya dodo nayaorodhesha mwishoni kwenye Kiambatanisho A
IV. TAFAKARI KUHUSU MASWALI YA DODOSO
Napenda sasa kufanya tafakari yangu kuhusu dodoso la sinodi ya 16 ya Maaskofu Katoliki Duniani kwa kujibu swali la 12 na swali la 50.
Swali la 12 linauliza hivi: "Je, tunayasikilizaje mazingira ya kijamii na kitamaduni yanayotuzunguka?"
Napendekeza kwamba swali hili lisomeke hivi: "Je, [tunapaswa kuyasikilizaje] mazingira ya kijamii na kitamaduni yanayotuzunguka?"
Na swali la 50 linauliza hivi: "Ni zana gani hutusaidia kusoma mienendo ya utamaduni ambamo tumezama na athari zake kwa mtindo wetu wa Kanisa?"
Swali hili nalo napendekeza lisomeke hivi:"Ni zana gani [zinapaswa kutusaidia] kusoma mienendo ya utamaduni ambamo tumezama na athari zake kwa mtindo wetu wa Kanisa?"
Machujio kwa Ajili ya Kuchambua Itiakdi za Ulimwengu
Tamaduni zinazolizinguka Kanisa Katoliki zinaweza kuangazwa vema kama tukikubaliana kwamba, kila utamaduni ni itikadi mtambuka (comprehensive worldview) kamili inayojitegemea.
Katika muktadha huu, napendekeza kwamba, zana inayopaswa kutumika kuumulika Ukristo na tamaduni zinazouzunguka ni kitu ambacho hapa nataka nikiite "Chujio Kubwa kwa Ajili ya Kuchambua Itiakdi za Ulimwengu (CHUKAKIU)," yaani "Comprehensive Worldview Analysis Toolkit (COWATO)".
Zana hii ni nyenzo mbadala kwa kitu ambacho hapa pia nataka niite "Chujio Dogo kwa Ajili ya Kuchambua Itiakdi za Ulimwengu (CHUDAKIU)," yaani "Abridged Worldview Analysis Toolkit (AWATO)," ambazo mara nyingi hutumiwa na wanazuoni, ikiwa na maswali kati ya nne na kumi:
Kwa mfano, Walsh na Middleton (1984) wanataja chujio lenye maswali manne, yaani:
(1) Human identity: Who am I ,Or, what is the nature, task and purpose of hum an beings? (2) Human location: Where am I, Or, w hat is the nature of the w orld and universe I live in? (3) Human evils: What's wrong, Or, w hat is the basic prob lem or obstacle that keeps me from attaining fulfillment or salvation? (4) Human Salvation: What is the remedy, Or, how is it possible to overcome this hindrance to my fulfillment or salvation? (p.35)
Sire (2009) anataja chujio lenye maswali saba yafuatayo:
(1) Ontology: What is prime reality? (2) Cosmology: What is the nature of the cosmos, that is, the world around us? (3) Anthropology: What is a human being? (4) Thanatology: What happens to a person at death? (5) Epistemology: Why is it possible to know anything at all? (6) Ethicology: How do we know what is right and wrong? (7) Historiology: What is the meaning of human history? (p. 22-24)
Na Noebel na Myers (2015) wanataja chujio lenye maswali kumi yafuatayo:
"(1) Theology: How did I and everything else get here? (2) Philosophy: What is real, as opposed to illusion, and how can I know it with certainty? (3) Ethics: What does it mean to live a good life? (4) Biology: What does it mean to be alive? (5) Psychology: What makes me human? (6) Sociology: How do we live in community with one another? (7) Economics: How can individuals and the community be optimally productive? (8) Law: What constitutes just and orderly governance? (9) Politics: What is the best way to organize a political community? (10) History: How did people in the past think and act on theology, philosophy, ethics, biology, psychology, sociology, politics, law, and economics?" (p.30-36).
Ni rai yangu kwamba, zana ya kuchuja itikadi mtambuka yenye kubeba maswali manne, saba, kumi, hata ishirini, haikidhi mahitaji yaliyopo kwa ajili ya kuzifananisha na kuzitofautisha itikadi mtambuko zilizopo katika dunia ya leo.
Katika ulimwengu wa leo, itikadi (worldview) inabeba mambo mengi sana, kama ambavyo mitaala ya kielimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu sehemu mbalimbali duniani inavyoshuhudia.
Kwa hiyo, kama nitakavyoonyesha hivi punde, napendekeza kwamba, tunapaswa kutumia "Chujio Mtambuka kwa Ajili ya Kuchambua Itiakdi za Ulimwengu," inayojumuisha maswali yanayogawanyika kwenye mafungu yapatayo 50 na zaidi.
Ni katika muktadha huu, natumia neno "itikadi" kumaanisha "worldview." Haya ni maneno ambao yanawakilisha dhana mahsusi kama inavyojadiliwa na watafiti maarufu, ndani na nje ya Kanisa Katoliki, kama nitakavyoonyesha.
Na maneno "Itikadi mtambuka" hapa yatamaanisha dhana ya "Comprehensive Worldview" kama inavyojadiliwa na wanazuoni kama vile John Rawls ambaye pia alipendelea kutumia maneno "comprehensive doctrines" kama kisawe (Rawls 1987)
Safari ya pamoja ni kitu gani na sio kitu gani?
Kuhusu misamiati muhimu, napenda kuongea kidogo juu ya maneno kwamba "sinodi ni safari ya pamoja."
Uhai wa Kanisa la Kisinodi unategemea uwepo wa "safari ya pamoja," safari ya pamoja inamaanisha uwepo wa "Umoja wa Kikanisa," Kanisa ni jumuiya, na Jumuiya ni kitu kimoja kinachowaunganisha watu wengi kwa kutumia "kanuni ya umoja wa vitu vingi vidogo vinavyounda kitu kimoja kikubwa zaidi" (the unity of a compound thing).
Kifalsafa, na hasa tangu enzi za kina Aristotle wa Ugriki, kanuni ya umoja wa vitu vingi inasema kwamba, umoja wa vitu viwili hutegemea uwepo wa kitu cha tatu kinachoviunganisha vitu hivyo viwili, kwamba, moja wa vitu vitatu hutegemea uwepo wa kitu cha nne kinachoviunganisha vitu hivyo vitatu, na vivyo hivyo kwa vitu vinne, vitano na kuendelea (Hoffman na Rosenkrantz 1998; Johnston 2013: 296-98; Qingyun 2015).
Kwa ujumla, umoja wa kitu kimoja chenye sehemu nyingi hutegemea uwepo wa kitu cha ziada, mbali na sehemu hizo, ambacho huziunganisha sehemu hizo pamoja hadi kuzifanya ziwe kitu kimoja.
Kwa mfano, ndoa ya mke na mume ni kitu kimoja kwa sababu mke na mume wanaunganishwa na kitu cha tatu kiitwacho tendo la ndoa, ambalo ni tendo la ngono ya jenitalia kwa jenitalia linalofanyika kwa mujibu wa kanuni ya muamala wa kubadilishana zawadi ya mwili (self-donation), na siokufanyika kwa mujibu wa kanuni ya muamala wa kibiashara ambapo mwili ni bidhaa inayopigwa bei (self-comodification).
Familia ya Baba, Mama na Watoto ni kitu kimoja, kwa sababu watoto ni zao la damu ya Baba na Mama linalopatikana kupitia tendo la ngono ya jenitalia kwa jenitalia.
Vivyo hivyo, Kanisa linapaswa kuwa kitu kimoja kwa sababu maalum. Kitu kinachowaunganisha wanakanisa ni imani (credenda) ambayo huweka msingi wa matendo (agenda) na matumaini (speranda) ya pamoja.
Kwa hiyo, pasipo "imani ya pamoja" hakuna "safari ya pamoja", na bila "safari ya pamoja" hakuna "Kanisa la Kisinodi."
Itikadi ni kitu gani na sio kitu gani?
Kama hivyo ndivyo, swali la kuongoza tafakari yangu linazuka: "imani ya pamoja" ndani ya Kanisa Katoliki, yaani imani yenye kulifanya Kanisa hili lijihesabu na kuhesabiwa kama kitu kimoja, hasa ni kitu gani na sio kitu gani?
Hapa napendekeza kwamba, imani ya kidini, kama vile imani ya Kanisa Katoliki, Imani ya Kanisa la Anglikana na Imani ya Kanisa la Kilutheri, ni itikadi (worldviews) kati ya itikadi nyingi zilizopo ulimwenguni. Ujamaa, ukomunisti wa Karl Marx, Usekulari, na Ukanamungu ni itikadi pia.
Noebel na Myers (2015) wanakubaliana na mtazamo huu. Wao wamejadili aina sita za itikadi zikiwemo itikadi za Secularism, Marxism, Postmodernism, Islam and Christianity. Wanataja fasili ifuatayo ya neno itikadi:
"A worldview is a pattern of ideas, beliefs, convictions, and habits that help us make sense of God, the world, and our relationship to God and the world" (Noebel and Myers 2015:16)
Wanaongeza maneno haya:
"Our worldview does not merely reflect what we think the world is like; it directs what we think the world should be like. In other words, our worldview not only describes reality, it prescribes how we should act and respond to every aspect of life. Because our ideas do determine how we behave, the bottom line is that our ideas do have consequences." (Noebel and Myers 2015:16)
Naye Sire (2009) ameorodhesha itikadi kama vile Theism, Deism, Naturalism, Nihilism, Existentialism, Pantheism, Postmodernism, na kuendelea.
Bila shaka Ukristo na Madhehebu yake, kwa upande mmoja, Uislamu a Madhehebu yake, kwa upande mwingine, ni dini zinazoanguka kwenye itikadi ya Theism.
Na kwa mujibu wa kanuni ya kuhesabu vitu vinavyofanana kwa kutumia vigezo vya lazima na vyenye kutosheleza mahitaji ya kutofautisha vitu hivyo (the principle of individuation based on necessary and sufficient conditions) kila dhehebu linayo itikadi kamili inayolifanya liwe kitu kimoja kamili.
Baada ya kuorodhesha itikadi hizi, Sire (2009) anasema kuwa zote zinafanana katika jambo moja kuu, kwani, kila moja ni "itikadi" ambayo kwa namna yake inatoa jawabu kwa swali lifuatalo:
Je, "anatomia ya msingi ya mti wa uhalisia" (basic constitution of reality) kuhusu Mungu, Binadamu, Jamii na Ulimwengu baki inaonyesha kwamba mti huu unayo matawi mangapi na matawi hayo yana vijitawi vingapi?
Yaani wanasema kuwa:
"A worldview is a commitment, a fundamental orientation of the heart, that can be expressed as a story or in a set of presuppositions (assumptions which may be true, partially true or entirely false) that we hold (consciously or subconsciously, consistently or inconsistently) about the basic constitution of reality, and that provides the foundation on which we live and move and have our being." (Sire 2009:20).
James Olthuis (1989:29) anasema yafuatayo kuhusu dhana ya itikadi (worldview):
"A worldview (or vision of life) is a framework or set of fundamental beliefs through which we view the world and our calling and future in it. This vision need not be fully articulated: it may be so internalized that it goes largely unquestioned; it may not be theoretically deepened into a philosophy; it may not even be codified into a creedal form; it may be greatly refined through culturalhistorical development. Nevertheless, this vision is a channel for the ultimate beliefs which give direction and meaning to life. It is the integrative and interpretive framework by which order and disorder are judged; it is the standard by which reality is managed and pursued; it is the set of hinges on which all our everyday thinking and doing turns."
Katika mazingira haya, Miaka sita baadaye, Sire (2015) aliandika tena na kufafanua itikadi saba alizozitafiti, yaani Christian theism, deism, naturalism, nihilism, exitentialism, new age spirituality na postmodernism. Anatumia maneno yafuatayo, ambayo sitaki kuyatafsiri, maana naweza kupoteza utamu:
"The bulk of [my book entitled] The Universe Next Door identified seven basic worldviews and then proceeded to explain what they were.
"I began with ...THEISM as it has been largely embodied from the seventeenth century to the present [as a belief in a supernatural being called God].
"Then I tried to show how DEISM arose as an erosion of certain key concepts of theism. Deism, as I see it, is ... what is left of theism when the personality of God is abandoned.
"NATURALISM, then, is a further erosion of deism, retaining its optimism with regard to the autonomy of human reason.
"NIHILISM is what is left of naturalism when it is realized that human reason, if autonomous, does not have the power to explain nearly as much as was first thought.
"EXISTENTIALISM—both atheistic and theistic—attempts to “go beyond nihilism,” affirming the intrinsic power of the individual self to will into being its own conception of the good, the true and the beautiful or to affirm by faith what cannot be proved by reason. Eastern pantheistic monism provides for the West a fresh start that attempts to avoid the pitfalls of Western thought.
"NEW AGE [SPIRITUALITY] thought then combines Western existentialism’s exaltation of the self with the Eastern notion of the deity of all things...
"POSTMODERNISM has taken a sociological and psychological twist to deny, on the one hand, the human ability to actually know reality in its essence and, on the other hand, to affirm the adequacy of human communities to construct reality by their language.
"One may not be able to know anything, but one can get along with this knowledge simply by constructing a language that works to get what one wants. Pragmatic knowledge is all one can have and all one needs." (Sire 2015:12). (Emphasis by capitalisation mine).
Mwandishi Sire (2015) anaigawanya itikadi ya "naturalism" kwenye sehemu mbili, yaani "secular humanism" na "Marxist humanism." Kimsingi, wafuasi wa "secular humanism" hawafungamani na upande wowote kati ya "wapingamungu" (atheists) na "wakirimungu" (theists). Kwa upande mwingine, wafuasi wa "Marxist humanism" ni aina mojawapo ya "wapingamungu" (atheists).
Kwa ufupi, anachosema Sire (2009, 2015) kuhusu itikadi kinaweza kunyumbulishwa kwa kusema kwamba:
"A worldview is a set of beliefs about the basic anatomy of reality that influence one's perceptions, thoughts and behaviours." (Mnyumbulisho wangu)
Kwa mfano, katika upande mmoja, Itikadi (worldview) ya Ukristo Asilia tangu enzi za Mitume 12 wa Yesu Mnazareti hadi leo inakumbatia mambo makubwa matatu. Mosi, Kanuni ya Imani ya Mitume, yenye kufafanua kiini cha imani. Pili, Amri Kumi za Musa, zenye kutoa miongozo na miiko maishani. Na tatu, Sala ya Baba Yetu, yenye kufafanua utume wa Yesu na wafuasi wake, kwa mujibu wa Yesu.
Mambo haya matatu yanakubalia katika sehemu kubwa ya Ukristo, yanagusa kila sehemu ya maisha ya Mkristo, yanao msingi wake katika maandiko na teolojia, na ni muhtasari bora kwa ajili udadavuzi wa kipengele kwa kipengele.
Na katika upande wa pili, itikadi (worldview) ya Uislamu inazo nguzo kuu tano. Yaani, kumkiri Allah na Muhamad kama mtume wake; kusali mara tano kwa siku; kufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani; kutoa zaka; na kufanya hija huko Maka angalau mara moja maishani.
Itikadi (worldview) hizi huokotwa kutoka vyanzo vikuu vitano. Kuna wazazi, makundi rika, viongozi wa dini, viongozi maarufu wa kisiasa na kijamii lakini wasio wazazi wetu, na walimu wetu mashuleni na vyuoni wanaotufunza kwa mujibu wa mitaala rasmi ya kiserikali.
Kwa ujumla, ni maoni yangu kwamba, imani za watu kuhusu "anatomia ya mti wa uhalisia" kuhusu Mungu, Binadamu, Jamii na Ulimwengu baki zikichambuliwa vema, zitaonyesha kuwa mti huu unayo matawi yafuatayo, kati ya mengine, yakiwa yamepangiliwa kialfabeti:
- Administrology (Utawala wa taasisi),
- Agatheology (Wema wa Mungu)
- Agathology (Wema wa ulimwengu)
- Angelology (Malaika),
- Anthropology (Ubinadamu),
- Axiology (Tunu),
- Biology (Uhai),
- Chorology (Mwanya),
- Christology (Yesu Kristo),
- Chronology (Majira),
- Clericology (Mfumo kasisi)
- Cosmology (Ulimwengu ulio nje ya mwili),
- Criminology (Jinai)
- Criteriology (logic) (Mantiki),
- Demology (Ongezeko la watu)
- Demonology (Shetani)
- Deontology (Haki na majukumu),
- Dogmatology (Imani za kibabe)
- Ecclesiology (Utawala wa Kikanisa),
- Ecology (Mazingira),
- Economiology(Economics) (Uchumi),
- Ecumenology (Uekumene)
- Embryology (Mimba)
- Epistemology (Maarifa ya kweli),
- Eschatology (Hofu na matumaini kuhusu dunia mpya).
- Ethicology (Maadili),
- Etiology (Mfumo wa sababu na matokeo),
- Harmatiology (Dhambi),
- Hedonology (Anasa za mwili),
- Historiology (Historia),
- Jurisiology (Jurisprudence) (Sheria),
- Mariology (Bikira Maria)
- Matrimoniology (Ndoa),
- Meriology (Kitu kizima na sehemu zake)
- Mythology (Visasili)
- Naratology (Masimulizi)
- Ontology (Kikonyo cha uhalisia),
- Paterology (Mungu Baba)
- Pathology (Magonjwa)
- Patriarchology (Mfumo dume)
- Personology (Utu)
- Phenomenology (fenomena)
- Physicology (physics) (fizikia),
- Pneumatology (Roho Mtakatifu),
- Politology (uongozi wa nchi)),
- Ponerology (Ubaya)
- Praxiology (Kupanga, kutekeleza, na kupima utekelezaji),
- Psychology (Mind) (King'amuzi chenye akili na utashi),
- Sacramentology (Sakramenti),
- Sexology (Ujinsia),
- Sociology (Jamii),
- Somatology (Tabia za magimba),
- Soteriology (Wokovu/Ustawi),
- Thanatology (Kifo),
- Thaumatology (miujiza)
- Theology (Mungu),
- Teliology (Lengo la msanifu)
- Trinitology (Utatu wa Mungu mmoja),
Hivyo, napendekekeza kuwa Imani Katoliki ni aina mojawapo ya itikadi (worldviews) zinazokubaliana na fasili ya Sire (2009), fasili ya Noebel and Myers (2015) na fasili ya James Olthuis (1989) kuhusu swali, "itikadi ni kitu gani na sio kitu gani?"
Lakini hapa nataka kusisitiza kwamba, itikadi zote zilizotajwa na waandishi hawa zinatofautiana katika namna zinavyofafanua kile ambacho waandishi wamekitaja kama "reality," yaani "mti wa uhalisia kuhusu Binadamu, Jamii, Mungu na Ulimwengu baki.
Tofauti hizi zinaweza kuonyeshwa kwa kutumia mfano wa kioo chenye umbo la mche pembetatu (prizimu), miale ya mwanga wa uhalisia inayotua kwenye upande mmoja wa prizimu hiyo, na miale ya mwanga wa uhalisia inayopita na kuchomoza kwenye upande wa pili wa prizimu hiyo.
Kwa kawaida mwanga mweupe ukigonga, na kisha kupita kwenye uso wa kioo cha prizimu ya aina hii, hupiga kona kidogo kwa kutengeneza pembe mchepuko (dispersion angle), kutanuka, na hivyo kuonyesha miale minane ya rangi zilizofichika ndani ya mwanga mweupe, yaani rangi za Red, Orange, Yellow, Green, Bluee, Indigo, na Violet (ROYGBIV) kama picha ifuatayo inavyoonyesha.
View attachment 2073404
Kila mwale unaochomoza upande wa pili wa prizimu unao upana wake wa mawimbi yenye kuambatana na upana wa frikwensi zake maalum kama jedwali lifuatalo linavyoonyesha, ambapo upana wa mdomo wa wimbi moja inatamkwa kutumia kipimo cha nanometa (nm), wakati upana wa frikwensi ya wimbi moja inatamkwa kwa kutumia kipimo cha teraherts (THz).
View attachment 2061555
Vivyo hivyo, miale mtuo ya mwanga wa uhalisia ukitua na kisha kupenya kwenye kioo cha prizimu ya itikadi yoyote, itazalisha miale mchomozo ya kiitikadi, kila mwale mchomozo ukiwa na upana wake wa frikwensi za uhalisia kulingana na prizimu ya kiitikadi iliyotumika kutawanya mwanga.
Mgawanyo wa itikadi katika makundi kadhaa
Kwa ujumla, itikadi zote zinaweza kugawanywa katika makundi mawili. Kwa upande mmoja, itikadi za kidini zinaunganishwa na sifa zifuatazo: zinajihusisha na mambo yasiyoweza kuthibitishwa wala kukanushwa kwa njia ya milango mitano ya fahamu (empirically untestable matters).
Pia kuna ibada; vitu vyote hugawanywa katika makundi mawili ya vitu vitakatifu na vitu visivyo vitakatifu; uendelevu; kugusa maisha yote ya watu.
Aidha itikadi hizi zina msingi wake katika hadithi za kale zilizovishwa joho la utakatifu kwa ajili ya kueleza sisi ni nani, tumetoka wapi, tuko wapi, na tunakwenda wapi.
Kadhalika, itikadi hizi hutaja wanaachopaswa kuamini watu kuhusu Mungu, ukweli, chimbuko la ulimwengu, ubinadamu, maadili, wokovu, lengo la maisha, na hatima ya ulimwengu.
Na mwisho itikadi hizi hutaja mwongozo inaowaonyesha wafuasi jinsi ya kuenenda kulingana na mapenzi ya Mungu wao.
Mifano ya itikadi za kidini ni dini za Ubuda, Ukristo, Uhindu, Uyahudi, Uislamu, Usiki, na Utao.
Kwa upande mwingine, itikadi za kidunia zinajihusisha na mambo yanayoweza kuthibitishwa au kukanushwa kwa njia ya milango mitano ya fahamu (empirically testable matters).
Hizi ni imani zilizobuniwa na wanadamu kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa ya maisha kuhusu kuhusu Mungu, Binadamu, Jamii na Ulimwengu baki.
Kwa mujibu wa itikadi hizi, kizio cha ukweli ni milango mitano ya fahamu. Mifano yake ni materialism or physicalism, humanism, naturalism, atheism , secularism na scientism/empiricism.
Mgawanyo huu wa itikadi katika itikadi za kidini na itikadi za kidunia ni kwa mujibu wa andiko la Sulaiman (2018).
Migongano kati ya itikadi pendwa
Ni rai yangu kwamba, ndani ya itikadi Katoliki, kuna mikanganyiko ya kimantiki na mikanganyiko ya kimetafizikia inayopaswa kuondolewa ili kulinusuru Kanisa dhidi ya mmomonyoko wa waumini kwa sababu hizi. Mikanganyiko hii huzalkisha mgyiko hii huzalisha migongano kati ya itikadi moja na itikadi nyingine.
Profesa George(2001), ameandika kwa kirefu kuhusu migongano ya kiitikadi inayojitokeza kutokana na maisha ya watu katika jamii zenye mseto wa itikadi nyingi.
George(2001) anapendekeza kwamba, migongano ya kiitikadi (clashes of worldviews) ndani ya Utamaduni wa Magharibi ni jambo la kawaida zaidi kuliko migongano kati ya Tamaduni za Mashariki na Tamaduni za Magharibi.
Kwa maoni yake, tayari ndani ya Utamaduni wa Kimagharibi kuna migongano ya kiitikadi kati ya itikadi zenye majina yanaoishia na kiambishi tamati cha "ism". Mfano ni feminism, communism, socialism, capitalism, liberationism, secularism, catholicism, anglicanism, lutheranism, na liberalism.
Kwa pamoja anarejea baadhi ya itikadi hizi kama "liberal secularism" au “secularist orthodoxy” kwa ajili ya kuzitofautisha na itikadi ya "Christian Orthodoxy" inayofuatwa na makundi kama vile Wayahudi, Wapentekoste, na Wahafidhina Katoliki.
Lengo la George katika kitabu hiki ni kuweka wazi msimamo kwamba, kadiri mafundisho ya kimaadili na kifalsafa kuhusu hulka na matendo ya binadamu yanavyohusika, mtazamo wa Ukristo wa Kihafidhina ni bora kuliko Ukristo wa Kiliberali.
Anadai mkwamba anatumia sababu zinazokubalika katika jukwaa la mijadala ya kirazini, na zenye kuungwa mkono na misahafu. Analitangaza lengo hili kwa maneno yafuatayo:
"I want to show that Christians and other believers are right to defend their positions on key moral issues as rationally superior to the alternatives proposed by secular liberals and those within the religious denominations who have abandoned traditional moral principles in favor of secularist morality. My criticism of secular liberal views is not that they are contrary to faith; it is that they fail the test of reason."(p.7)
George anahitimisha hoja zake kitabuni kwa kusisitiza mambo mawili. Mosi, kwamba, migongano ya kiitikadi kati ya Ukristo wa Kihafidhina na Ukristo wa Kiliberali sio mgogoro wenye sura ya uadui kati ya imani na urazini, bali mnyukano kati ya hoja bora za kirazini na hoja dhaifu za kirazini.
Na pili, kwamba, katika miogoro hii, hoja za Ukristo wa Kihafidhina ni bora kuliko hoja dhaifu za Ukristo wa Kiliberali.
Sio lengo langu hapa kuchambua hoja zake. Lakini nataka kukosoa jambo moja muhimu kusudi mjadala unaoendelea hapa uweze kutazamwa katika urefu na upana wake.
Nakosoa maneno yake kwamba, kwa sehemu kubwa, mgongano wa kiitikdi unatokea kwenye sekta za kiitikadi zinazohusu biology, sexology, matrimoniology, na politology; yaani katika masuala ya uhai, ujinsia, ndoa na nafasi ya dini katika kutunga sheria za nchi yenye dini zaidi ya moja.
Tatizo ni pana zaidi ya hapo. Kwa hakika, kuna migongano mikubwa zaidi kwenye maeneo mengine zaidi ya 50 mbali na haya maeneo manne aliyoyataja.
Ni bahati mbaya kwamba, hoja zinazohusu uhai wa mimba, uhai wa wagonjwa mahututi, ujinsia tata, na ndoa za jinsia moja, hoja ambazo mara nyingi huambatana na mihemuko, hutumiwa kama nyenzo ya kuzalisha mihemuko miongoni mwa wasikilizaji, na hivyo kuwaziba midomo wakosoaji wenye hoja mbadala na zenye mashiko.
Lakini, ukweli ni kwamba, unaweza kuwadanganya watu wote kkwa muda kitambo, na unaweza kuwadananya watu wachache muda wote, lakini huwezi kuwadanyanya watu wote muda wote.
Katika muktadha huu, maneno ya profesa George (2001) ninayoyakosoa ni haya hapa:
"First, let’s get clear what is at stake in the conflict between Christian (and Jewish and to a large extent Islamic) morality and the secularist orthodoxy. The issues immediately in play have MAINLY, though not exclusively, to do with sexuality, the transmitting and taking of human life, and the place of religion and religiously informed moral judgment in public life."(p.11) (emphasis by capitalisation mine)
Nitaeleza ukosoaji wangu kwa njia ya mifano kadhaa, kwa kuzingatia kambi mbili za kiitikadi zinazopendekezwa na George (2001), yaani, Itikadi ya Ukristo wa KIhafidhina na Itikadi ya Ukristo wa Kiliberali.
Kwa vile Itikadi ya Ukristo wa Kiliberali ni kabila lenye koo nyingi, nitatumia koo mbili kama wawakilishi, yaani ukoo wa "deism" na ukoo wa "naturalism."
Na kwa ajili hii nitafananisha na kutofautisha itikadi hizi mbili kwa kutumia maswali yafuatayo:
(1) Ontology: What is prime reality? (2) Cosmology: What is the nature of the cosmos, that is, the world around us? (3) Anthropology: What is a human being? (4) Thanatology: What happens to a person at death? (5) Epistemology: Why is it possible to know anything at all? (6) Ethicology: How do we know what is right and wrong? (7) Historiology: What is the meaning of human history? (Sire 2009: 22-24)
Kwa upande mmoja, kama mwale wa uhalisia utatua kwenye prizimu ya Itikadi ya Ukristo wa KIhafidhina (Conservative Christianity), basi upande wa pili kutatokea miale mchomozo yenye kuonyesha ukweli ufuatao:
(1) Prime reality is the infinite, personal God revealed in the Holy Scriptures. This God is triune, transcendent and immanent, omniscient, sovereign, and good. (2) External reality is the cosmos God created ex-nihilo to operate with a uniformity of cause and effect in an open system. (3) Human beings are created in the image of God and thus possess personality, self-transcendence, intelligence, morality, gregariousness and creativity. (4) Human beings can know both the world around them and God himself because God has built into them the capacity to do so and because he takes an active role in communicating with them. (5) For each person death is either the gate to life with God and his people or the gate to eternal separation from the only thing that will ultimately fulfill human aspirations. (6) Ethics is transcendent and is based on the character of God as good (holy and loving). (7) History is linear, a meaningful sequence of events leading to the fulfillment of God’s purposes for humanity. (Sire 2009:25-46)
Na kwa upande mwingine, mwale wa uhalisia ukipenya kwenye prizimu ya itikadi ya Ukristo wa Kiliberali (LIberal Christianity), kama inavyowakilishwa na ukoo wa "deism", huenda ikaonyesha miale mchomozo ifuatayo:
(1) A transcendent God, as a First Cause, created the universe but then left it to run on its own. God is thus not immanent, not triune, not fully personal, not sovereign over human affairs, not providential. (2) The cosmos God created is determined, because it is created as a uniformity of cause and effect in a closed system; no miracle is possible. (3) Human beings, though personal, are a part of the clockwork of the universe. (4) Human beings may or may not have a life beyond their physical existence. (5) Through our innate and autonomous human reason and the methods of science, we can not only know the universe but we can infer at least something of what God is like. The cosmos, this world, is understood to be in its normal state; it is not fallen or abnormal. (6) Ethics is intuitive or limited to general revelation; because the universe is normal, it reveals what is right. (7) History is linear, for the course of the cosmos was determined at creation. Still the meaning of the events of history remains to be understood by the application of human reason to the data unearthed and made available to historians. (Sire 2009: 47-65).
Ulinganisho mdogo tu huu hapa unatosha kuonyesha kwamba kuna bonde la ufa kubwa sana kati ya Itikadi ya Ukristo wa Kihafidhina na Itikadi ya Ukristo wa Kiliberali, hata kabla ya kuongelea uhai, ujinsia, ndoa na nafasi ya dini katika majukwaa ya umma.
Kwa ajili ya kuweka msisitizo kwenye mpasuko huu katika ngazi ya ontology, cosmology, anthropology, thanatology, ethicology, epistemology, na historiology, naongeza udadavuzi wa ukoo mwingine wa Itikadi ya Ukristo wa Kiliberali uitwao "naturalism."
Kama mwale wa uhalisia utapenya kwenye kioo cha prizimu ya "naturalism", huenda miale mchomozo yenye kutoa ujumbe ufuatao itatokea:
(1) Prime reality is matter. Matter exists eternally and is all there is. Neither God, gods nor spirits exist. (2) The cosmos exists as a uniformity of cause and effect in a closed system. (3) Human beings are complex machines; personality is an interrelation of chemical and physical properties we do not yet fully understand. (4) Death is extinction of personality and individuality. No life beyond the grave. (5) Through our innate and autonomous human reason, including the methods of science, we can know the universe. The cosmos, including this world, is understood to be in its normal state. (6) Ethics is related only to human beings, without any reference to God, gods or spirits. (7) History is a linear stream of events linked by cause and effect but without an overarching purpose. (Sire 2009: 66-93).
Kwa hiyo, sasa tunaweza kuelewa tamko kwamba, kukosekana kwa "Kanisa la Kisinodi" kunatokana na ukosefu wa "safari ya pamoja" kwa sababu ya ukosefu wa "imani ya pamoja," imani ambayo hapa nimeiita "itikadi."
Ndio kusema kwamba, watu walioko nje ya barabara inayotumiwa na waumini wanaotembea kama "Kanisa la Kisinodi" wako nje kwa kuwa wanayo itikadiambayo, kwa kiasi fulani, ni tofauti.
Yaani, kama tukiongelea Kanisa la Kisinodi ndani ya Kanisa Katoliki, hii maana yake ni kwamba, kwa wale walioko nje ya Kanisa hili, ama itikadi Katoliki imewakataa au wao wmeikataa au bado wanaitafakari.
Mikangayiko ya kiitikadi kama chanzo cha mmomonyoko wa Kanisa
Kwa sababu ya utitiri wa itikadi katika jamii, baadhi ya watu wanapata sababu ya kuchagua na kubagua kambi za kiitikdai. Kwa mfano, tafiti zinaonyesha kuwa kuna mmomonyoko wa wafuasi ndani ya Kanisa Katoliki (dissaffiliation) kwa sababu mbalimbali.
Kwa mfano, Kanisa Katoliki linapoteza wafuasi kila kukicha. Karibu 13% ya Wamarekani wanajitambulisha kama “Wakatoliki Wastaafu”. Kati yao, 71% wanasema waliondoka Kanisa Katoliki kwa sababu "ilitokea tu." (Manning 2018).
Lakini, kutakuwepo na sababu za msingi zaidi. Kwa hiyo, swali la kiutafiti ni hili hapa: Je, data za kitafiti zinafichua sababu gani za ukengeufu dhidi ya kanuni za imani ya Kikristo kama inavyoeleweka katika mapokeo?
Swali hili linaweza kujibiwa kwa mujibu wa nguzo nne za imani ya Kikristo. Nguzo hizo ni maarifa ya imani, maisha ya sakramenti, kushi maadili, na maisha ya sala.
Katika muundo wa maswali, mambo haya manne yanamaanisha maswali ya kitafiti yafuatayo:
- (1) Ujuzi wa imani: Je, watu wanaondoka kwenye Kanisa Katoliki kwa sababu hawaelewi imani yake?
- (2) Mkanganyiko wa kimantiki katika imani: Je watu wanaondoka kwenye Kanisa Katoliki kwa sababu imani hiyo inaambatana na mkanganyiko wa kimantiki?
- (3) Mkanganyiko wa kimetafizikia katika imani: Je watu wanaondoka kwenye Kanisa Katoliki kwa sababu imani hiyo inaambatana na mkanganyiko wa kimetafizikia?
- (4) Maisha ya sakramenti: Je, kuna upungufu wa wazi wa ubatizo, ndoa, na mahudhurio ya ibada ya kila juma?
- (5) Kuishi kwa mujibu wa imani: Je, Wakatoliki hukubali mazoea ambayo yanashutumiwa rasmi na mamlaka ya kufundisha ya Kanisa kuwa ni makosa ya kimaadili? na
- (6) Maisha ya sala: Je, idadi ya Wakatoliki wanaosali angalau mara moja kwa siku inaongezeka au la?
Kuhusu swali la kwanza, takwimu zilizopo kuhusu mabadiliko katika viwango vya maarifa kuhusu Ukatoliki, zinaonyesha kwamba, wanafunzi wa Kikatoliki wa siku hizi wana maarifa zaidi kuliko vizazi vilivyotangulia. Wakatoliki wanazidi kuongeza ujuzi siku baada ya siku. Kwa hiyo, ushahidi uliopo hautoi uhalali wa kutosha kwa hitimisho kwamba watu wanaacha imani ya Kikatoliki kwa sababu hawaielewi.
Kuhusu swali la pili, ushahidi unaonyesha kuwa, sababu kubwa inayosababisha ongezeko la "Wakatoliki Wastaafu" ni mkanyanyiko wa kimantiki na (logical contradiction) uliomo katika mafundisho mengi ambayo ni sehemu ya itikadi Katoliki.
Kimantiki, Kanuni ya Kutojipinga kwa Ukweli wa Kimantiki (Law of Logical Non-Contradiction) inasema kuwa, kauli ile ile moja haiwezi kusema ukweli na kuupinga ukweli huo wakati huo huo na katika mazingira yale yale. Branson (2014) anasema yafuatayo kuhusu dhana ya mkanyanyiko wa kimantiki ninayoiongelea hapa:
"A set of propositions is explicitly inconsistent if and only if, at least, one member of the set just is the denial or negation of, at least, one member of the set. A set of propositions is formally inconsistent if and only if an explicit contradiction can be derived from its members using only the rules of ordinary logic. A set of propositions is implicitly inconsistent if and only if adding some necessarily true proposition(s) to it yields a formally inconsistent set." (Branson 2014:10)
Kuhusu swali la tatu, ushahidi unaonyesha kuwa, sababu nyingine kubwa inayosababisha ongezeko la "Wakatoliki Wastaafu" ni mkanyanyiko wa kimetafizikia (metaphysical contradiction) uliomo katika mafundisho mengi ambayo ni sehemu ya itikadi Katoliki.
Kanuni ya Kutojipinga kwa Ukweli wa Kimetafizikia (Law of Metaphysical Non-Contradiction) inasema kuwa, kitu kile kile X hakiwezi kuwa na sifa Y na kukosa kuwa na sifa Y wakati huo huo na katika muktadha ule ule.
Yaani, mkanganyiko wa kimetafikia unahusu anatomia ya uhalisia ulioko nje ya akili za watu. Kuhusu jambo hili, Tahko (2009) anasema maneno haya:
"...the law of non-contradiction (LNC) is a metaphysical rather than a logical principle... We will, however, be better off with one of Aristotle’s many formulations of the LNC, such as, 'the same attribute cannot at the same time belong and not belong to the same subject in the same respect.' When put like this, the principle appears considerably deeper, as it clearly states a restriction that concerns things rather than just propositions. We can thus avoid a prolonged discussion about the nature of propositions... At its simplest, the metaphysical interpretation of LNC amounts to this: the entities of the mind-independent reality are plausibly governed by some sort of principles (as otherwise there would be no order in our experience of them), that is, there are some constraints as to what kind of properties a certain kind of entity can and cannot have, and further, some of these properties are mutually exclusive. For instance, a particle cannot both have and not have a charge at the same time, or an object cannot be both green and red all over at the same time. It seems that reality just is such that it conforms to the law of noncontradiction." (p.32-33)
Kwa mfano, sifa moja ya sayari ya dunia ni ukweli kwamba hii ni sayari ya tatu katika mfumo wa jua. Sayari hii haiwezi kuwa sayari ya tatu na isiwe sayari ya tatu ndani ya mfumo ule ule wa jua.
Kwa hiyo, mkanganyiko wa kimetafizikia utakuwa ni madai kwamba sayasi ya dunia ni sayari ya tatu na sio sayari ya tatu katika mfumo wa jua.
Kuhusu swali la nne hapo juu, yaani maadhimisho ya sakramenti, tafiti zinaonyesha kuwa nkuna kupungua kwa ubatizo, ndoa, na mahudhurio ya ibada ya kila Jmapili.
Kuhusiana na swali la tano, data ya uchunguzi zinadhihirisha kwamba, Wakatoliki wengi wanaidhinisha desturi zifuatazo ambazo zinashutumiwa rasmi na mamlaka ya Kanisa: adhabu ya kifo, matumizi ya kingamimba, mauaji ya huruma, talaka, ngono kabla ya ndoa, na kadhalika.
Lakini, mbali na masuala haya ya kimaadili na mambo mengine ya kuishi maisha ya imani kama vile zaka na ushiriki wa parokiani, Wakatoliki wanaonyesha dalili za kujitolea kidini katika baadhi ya maeneo lakini si mengine.
Hatimaye, kuhusu swali la sita, yaani sala, takwimu zinaonyesha kwamba, asilimia ya Wakatoliki wanaosali angalau mara moja kwa siku inaongezeka. Kwa hiyo, mabadiliko yanatokea duniani, hayawafanyi raia kuwa mbali zaidi na Mungu.
Lakini, kwa ujumla, mabadiliko katika imani na tabia za Kikatoliki zinazoonekana katika data ya sosholojia kwa hakika hufichua ukengeufu dhidi ya kanuni za imani ya Kikristo kama zinavyoeleweka kimapokeo.
Hasa hasa, kupungua kwa wazi kwa adhimisho la kisakramenti na kuongezeka uasi dhidi ya mafundisho rasmi ya kimaadili juu ya masuala fulani ya maadili kunaelezea kwa nini Ukatoliki unachukuliwa na wengine kuwa unamomonyoka.
Hata hivyo, kuongezeka kwa shughuli katika maeneo mengine, kama vile ushiriki wa parokiani, maombi, na kujiweka karibu na Mungu kwa njia ya sala binafsi, kunapingana na masimulizi ya wananadharia ya kisekulari kwamba dini inaporomoka kwa kufuata mstari ulionyooka kwa sababu ya changamoto za ulimwengu wa kisayansi.
Kwa ufupi, Wakatoliki wengi hawaoni tena maana katika sakramenti au kuona umuhimu wa baadhi ya mafundisho ya Kanisa kwa maisha yao ya kila siku. Ijapokuwa nia yao ya kuendelea kuwa na uhusiano na Mungu iko pale pale, hawa wakatoliki wastaafu, wanaachana na dini kama mfumo wa kimapokeo wa kuwaunganisha watu ambao uliwategemeza mababu zao.
Kinachohitajika hapa ni ama kubadilisha itikadi au kubadilisha mawazo ya watu walioko nje ya Kanisa Katoliki au kubadili vyote viwili kwa namna fulani.
Sababu ya Sinodi kuitishwa sasa
Ni katika mazingira haya ya mmomonyoko wa wafuasi kwa sababu za kiitikadi, Papa Francis ameandaa dodoso la Sinodi ya 16 ya Maaskofu na kuuliza swali lifuatalo, kati ya mengine:
"Ni hatua gani ambazo Roho Mtakatifu anatualika kuchukua ili tuweze [kusafiri pamoja bila kumwacha binadamu yeyote nyuma na hatimaye] kukua wakati wa 'safari ya pamoja'”?
Maneno yaliyo kwenye mabano ya mraba, yaani "kusafiri pamoja bila kumwacha mtu yeyote nyuma na hatimaye", ni yangu.
Ni kwa ajili ya kufafanua swali hili, watu kama vile Robert Wuthnow (1993) wameandika kitabu kinachojadili changamoto zinazolikabili Kanisala Karne ya 21, kwa kuzigawanya katika makundi makubwa yafuatayo: changamoto za kitaasisi, kimaadili, kiimani, kisiasa, na kiutamaduni.
Lakini, katika andiko hili nimejaribu kupanua wigo wa matatizo anayoyajadili Wuthnow (1993) ili kuonyesha kwa mpigo matawi yote ya changamoto husika ndani ya mti wa uhalisia kuhusu Mungu, Binadamu, Jamii na Ulimwengu baki.
Kwa ujumla, kuna mageuzi makubwa inabidi kufanyika ili kukamilisha ndoto ya Papa Francis aliyeanzisha mchakato huu.
Ni mageuzi ambayo yatafanyika katikati ya mseto wa itikadi anwai. Baadhi zikiwa ni itikadi za kidini wakati zingine sio itikadi za kidini, kama tulivyoona hapo awali.
V. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
Papa Francis ameanzisha utafiti mkubwa katika wakati mwafaka. Ni wakati ambapo minyukano ya kiitikadi duniani imepamba moto kwa kiwango ambacho kinalitaka Kanisa Katoliki kujitathmini kwa namna ambayo italiacha imara zaidi katika ti ya mawimbi hayo ya kiitikadi.
Yafaa Kanisa Katoliki litumie fursa hii kufanya tathmini ya itikadi yake katika maeneo yote kuhusiana na mti wa uhalisia kuhusu Mungu, Binadamu, Jamii na Ulimwengu baki.
Yaani, Kanisa lisafishe nyumba yake kwa kufagia, kudeki na kukarabati vyumba vyote vilivyomo katika zana ya COWATO kama ilivyojadiliwa hapo juu.
Na kama majawabu yatakayokusanywa yatafanyiwa kazi, yanaweza kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Kanisa Katoliki kutokana na msukumo ulioanzia ndani ya Kanisa lenyewe.
BInafsi, mapendekezo yangu yanazingatia vipengele vilivyoorodheshwa hapo juu, na ni kama ifuatavyo:
Kama mwale wa uhalisia utatua kwenye kioo cha prizimu ya Itikadi ya Ukatoliki baada ya 2023 (Post-2023 Catholicism), basi, natamani kuona kwamba upande wa pili kunatokea miale mchomozo yenye kuonyesha ukweli ufuatao kuhusu Itikadi Mpya ya Ukatoliki baada ya 2023:
1. ADMINISTROLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kanuni za kuendesha taasisi yenye muundo wa kihierakia, kama vile Kanisa Katoliki lilivyo, zinapaswa kuzingatiwa kila mara, kila wakati na kila taasisi, likiwemo Kanisa Katoliki na taasisi zake zote. Kanuni hizo ni pamoja na span of control, unity of command, vertical separation of powers, accountability, responsibility, na horizontal separation of powers. Kwa sasa, kuna tatizo la kiutawala ndani ya Kanisa Katoliki. Chini ya Papa kuna Maaskofu 5,300; na kuna viongozi 700 wa taasisi mbalimbali za kikanisa, zikiwemo taasisi za Roman Curia, wanaoripoti kwa Papa moja kwa moja. Hii maana yake ni kwamba Papa anaoy span of control ya watu 6,000. Kunahitajika ngazi moja ya kiutawala kati ya Maaskofu na Papa ili kupunguza hii span of control. Ni kwa njia hii usimamizi wa makasisi na maaskofu utaleta kasi na ufanisi wa “safari ya pamoja” ndani ya Kanisa Katoliki. (Dive 2020).
2. ANTHROPOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli, taaluma ya ubinadamu (anthropology) inagawanyika kwenye makundi mawili, ya somatolojia (somatology) na saikolojia (psychology); kwamba, somatolojia ni sayansi inayochunguza tabia za miili ya vitu vyenye uhai na visivyo na uhai; kwamba, somatolojia inagawanyika mara mbili, yaani anatomia inayochunguza muundo wa viungo vya mwili, na fiziolojia inayochunguza utendaji wa viungo vya mwili; kwamba, saikolojia huchunguza king'amuzi cha kibinadamu chenye kuhusisha hazina ya akili na utashi (human mind); kwamba, kuna saikolojia mbashara yenye kutumia mbinu za kisayansi katika utafiti na saikolojia ya kirazini kwa ajili ya kutafsiri taarifa zinazohusu utendaji wa king'amuzi cha kibinadamu; kwamba, kila binadamu amegawanyika katika sehemu kuu mbili zinazotegemeana, mwili wa kifizikia (physical body) na king'amuzi cha kiroho (spiritual mind), sehemu ambazo, kwa pamoja, hufanya kazi kama pande mbili za shilingi zisizoweza kutenganishika katika siku zote za uhai wa binadamu; kwamba kiini cha hadhi ya ubinadamu ni hazina ya akili na utashi aliyo nayo kila mmoja tangu siku mimba yake inapotungwa; kwamba, ni muhimu na lazima tunu chanya ya umoja wa mwili na roho (body-self integralism) kuheshimiwa kila mahali, kila wakati na kika mtu; na kwamba, ni muhimu na lazima tunu hasi ya utengano wa mwili na roho (body-self dualism) kuepukwa kila mahali, kila wakati na kika mtu. Ni maoni yangu kwamba, kwa sasa, sera ya useja wa makasisi na kujikana kwa watawa wa kike inakumbatia tunu hasi ya body-self dualism.
3. AXIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, zifuatazo ni tunu muhimu kwa kila binadamu: umoja wa mwili na roho, afya, elimu, uhai, ikolojia (mazingira), ofisi zenye utawala bora, uchumi unaojali maslahi ya wote, ndoa, urafiki, haki, ukweli, uwajibikaji, amani, na utajiri.
4. BIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, uhai wa binadamu kamili unayo hazina ya uwezo wa kuonyesha sifa kuu nane zifuatazo: kujongea, kujisaidia, kupumua, kuzaa, kufa, kuhisi, kupata lishe na kukua (movement, excretion, respiration, reproduction, yielding to death, irritation, nutrition and growth, yaani M.E.R.R.Y.I.N.G.); kwamba, spematozoa sio binadamu mchanga; kwamba na ovamu sio binadamu mchanga; kwamba, uhai wa binadamu kamili huanza tangu siku spermatozoa na ovamu zinapoungana katika tumbo la uzazi; Kwamba, binadamu wote ni viumbehai wenye uhai ualio na hadhi sawa tangu wakiwa tumboni mwa mama zao; Kwamba kila binadamu anayo haki ya kuishi tangu akiwa tumboni mwa mama yake; Kwamba kila binadamu asiye na madhara kwa jirani yake anayo haki ya kuwa huru dhidi ya kifo kinachoweza kusbabishwa na binadamu baki; kwamba, binadamu amevuvumka kutokana na wanyama kama vile sokwe kupitia mchakato wa “natural selection”; kwamba, viumbe hujifunza kuyamudu mazingira yao na mazingira yakajifunza kuvimudu viumbehai kupitia mchakato wa “adaptation,” ambapo kiumbe hujibadilisha taratibu ili kiweze kuhimili mikiki mikiki ya kimazingira; na kwamba, huenda michakato ya “natural selection” na “adaptation” hutokea kwa msaada wa mkono wa Mungu.
5. COSMOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, ulimwengu huu ulizaliwa mabilioni ya miaka iliyopita kwa njia ya mchakato uliohusisha mlipuko mkubwa (big bang theory), ambapo baada ya mlipuko huo mabara, bahari, milima na mabonde vilijitengeneza hatua kwa hatua; na kwamba, huenda, mchakato huu ulihusisha mkono wa Mungu. (Craig and Smith 1995).
6. CRITERIOLOGY (LOGIC): Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kila hoja iliyokamilika kimantiki yafaa iwe na sehemu zifuatazo madai, msingi wa madai, waranti ya msingi wa madai, kiegamio cha waranti, mkingamo tarajiwa, kibutuzi cha mkingamo tarajiwa, na mipaka ya ukweli unaotetewa katika hoja (claim, ground, warrant, backing, objection, rubuttals, qualifiers); kwamba, hakuna kauli inayoweza kusema ukweli na kukanusha ukweli huo wakati ule ule na katika mazingira yale yale; kwamba, kutengeneza hoja pinde (logical fallacy) kwa makusudi ni kitendo cha kumwabudu Mungu wa Umachiaveli; na kwamba, kutumia lugha yenye kuudhi, kukera na yenye kuambatana na matusi (offensive, insulting, and abusive language, yaani offinabusism) kama mbinu ya kumnyamazisha mleta hoja badala ya kujibu hoja yake, ni kitendo cha kumwabudu Mungu wa Umachiaveli; kwamba, ni kosa la kimantiki kuzalisha hitimisho linaloongelea kanuni za kimaadili kutokana na kanuni za kimaumbile pekee (No-Ought-From-Is Fallacy, yaani NOFI Fallacy). Mara kadhaa nimeshuhudia baadhi ya mapadre wakimwabudu Mungu wa Machiaveli kwa njia ya kutengeneza hoja pinde kwa makusudi; na kushiriki katika mawasiliano yanayoongozwa na itikadi ya offinabusism. Pia, maandiko kadhaa ya Kanisa yanaambatana na NOFI Fallacy pamoja na NIFO Fallacy. Kama muumini makini wa kanuni za criteriology (logic) mwenendo huu umenikwaza kwa miaka 15 sasa. Mapadre waliothibitika kushiriki katika mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya walei kwa kutumia silaha ya “offinabusism” ni Pamoja na Padre Joseph Jenkins wa Washingtom DC, Marekani; Padre Gaudensi Talemwa wa SAUT tawi la Mwanza; Padre Sigfried Ntare Rusimbya wa Seminari Kuu ya Segerea Dar es Salaam; na Padre Ivus Tindyebwa wa Rulenge-Ngara. Padre Jenkins amekuwa anatumia blogu yake kutukana watu, bloogu ambayo sasa ameifunga kwa password. Alipoambiwa kuwa "no sex act which is intrinsically open to life" majibu yake yalihusisha matusi kama vile "possessed and bonkers." Na utovu wa maadili wa kina Talemwa, Rusimbya na Ivus ulithibitika zaidi kupitia kundi la Whatsapp liitwalo KATOKE SEMINARY ALUMN mnamo tarehe 10-11 Novemba 2021. Wakijibu hoja kuhusu tatizo la mfumo-kasisis (clericalism) iliyoanzishwa na mwanakundi mmoja (Newton), walimbatiza majina mabaya zaidi ya kumi. Mara mwehu, sio mkatoliki, amepoteza mwelekeo, na majina mengine ya ajabu kama hayo, badala ya kujibu hoja iliyowekwa mezani. Baadaye admin wa kundi hilo, Evodius Anthony Kashaija, kwa kuzingaia ushauri wa Padre Talemwa ambaye pia ni admin, alimtoa Newton kwenye kundi hilo kwa sababu tu ya kusanifu hoja yenye kueleza ukweli anaouamini. (Naambatanisha kumbukumbu za mjadala wa siku hizo mbili hapa chini). Katika kitako cha ukweli, mapadre hawa wamekuwa makuwadi wa itikadi ya kimachiaveli kwa sababu, katika majadiliano, offinabusism ni mbinu ya kufukuzia lengo zuri la kufanya ushawishi kwa watu baki lakini kwa kutumia mbinu haramu ya kusigina hadhi ya ubindamu wa msemaji mmojawapo. Kama mapadre wataendekeza tabia hii ya offinabusism ni wazi kwamba waumini wengi watalikimbia Kanisa. Ikomeshwe.
7. DEONTOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, haki na majukumu ni kama pande mbili za shilingi zisizotenganishika kamwe; Kamba, haki na majukumu ya kibinadamu vinagusa sekta zote za Maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na afya, elimu, ikolojia, ofisi za utawala wa kisiasa, uchumi, jamii, ujinsia, na utamaduni. Kanisa limekuwa na utamaduni wa kuepuka kuongelea haki za kijinsia. Hata waandishi maarufu kuhusu Mitazamo ya Maaskofu wa Afrika juu ya Haki za bindamu, kama vile Padre Stanslaus Muyebe na Padre Alex Muyebe, wamekuwa wanakwepa kabisa kujadili topiki ya haki za kijinsia. Katika suala hili, ninaona kwamba, Kanisa linasumbuliwa na tatizo la mchakato wa “scotosis” anaouongelea Lonergan (1956:91). Katika mchakato huu kuna mchujo wa makusudi wa taarifa ili kuficha au kuepuka maarifa ya aina fulani kwa makusudi. Matokeo yake ni upofu fulani, tuseme “colour blindness,” kiasi kwamba Kanisa haliwezi tena kuona haki za kijinsia. Kwa mujibu wa Lonergan, hitimisho hili ni tatizo linaloitwa “scotoma”. Yafaa wanazuoi wa Kanisa tuepuke “scotosis” na “scotoma” kadiri suala la kutafiti na kujadili haki za kijinsia zinavyohusika.
8. ECCLESIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, mfumo wa maamuzi ndani ya Kanisa unapaswa kujumuisha watu wote waliobatizwa bila kujali kama mhusika analo daraja la ukasisi au ni mlei asiye na daraja hilo; kwamba uwezo wa kuamua masuala ya kikanisa hautokani na mtu kupewa daraja la upadre, bali maandalizi yanayompa mtu weledi katika sekta husika ya kimaisha, bila kujali kama ni kasisi au hapana; na kwamba, kuendelea na utaratibu wa sasa wa kuwanyima walei fursa za kufanya maamuzi ndani ya kanisa lao ni kukiuka kanuni ya usawa wa kirazini walio nao binadamu wote. Kwa sasa, ndani ya Kanisa hakuna kikao chochote cha Kikanisa ambako walei wanayo haki ya kufanya maamuzi (deliberation), zaidi ya kupewa haki ya kutoa ushauri (consultation) makasisi. Utaratibu huu wenye kuendekeza mfumo-kasisi (clericalism) unakiuka usawa wa hadhi ya ubindamu. Dosari zake ni sawa na dosari zilizomo katika mfumo-dume (patriarchy), mfumo-jike (matriarchy), na mifumo kama hiyo. Katika kikonyo cha ukweli, clericalism, patriarchy, na matriarchy ni mifumo ya kimachiaveli kwa sababu inafukuzia malengo mazuri kwa kutumia mbinu haramu ya kusigina hadhi ya ubindamu wa wale wanaobaguliwa katika mifumo hii.
9. ECOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kila binadamu ni sehemu ya mifumo ya kiikolojia iliyoko duniani, yenye kuunganishwa Pamoja kwa njia ya mizunguko ya bayojiokemia (biogeochemical cycles); kwamba, mizunguko ya bayojiokemia huunganisha uliwemngu wa viumbe hai (biotics) na ulimwengu wa viumbe visivyo hai (abiotics), katika namna ambayo huvisaidia viumbehai kupata elementi muhimu kutoka kwenye ulimwengu baki; kwamba, elementi muhimu zinazohitajika kwa ajili ya makuzi ya viumbe hai na ambazo hutoka kwenye ulimwengu wa vitu visivyo hai, kuingia na kisha kutoka kwenye miili ya viumbe hai kwa kupitia miduara ya bayojiokemia ni pamoja na kaboni, haidrojeni, oksijeni, naitrojeni, fosiforasi, chuma, salfa, ayodini, potasiam, magneziam, na Zinki; kwamba, kwa sababu ya elementi zinazobebwa na miduara ya bayojiokemia, utambuliko halisi wa miili ya binadamu unatokana na mifumo mikongwe ya kiikolojia iliyopo tangu miaka bilioni 15 iliyopita; kwamba, kupitia mfumo wa kiikolojia hapa duniani, vitu hai na visivyo hai vimefungamana na vinategemeana katika kila hatua, kubwa na ndogo; kwamba, katika mfumo huu binadamu na viumbe hai baki wanaunganishwa na asidinasaba (DNA) moja ya uhai; kwamba binadamu hawezi kuishi nje ya historia ya dunia yake wala hawezi kutengeneza maisha mapya nje ya dunia hii; na kwamba kwa ajili ya kufanikisha maendeleo endelevu lazima kila hatua tunayopiga iambatane na utekelezaji wa jukumu la kuviwekea akiba ya kimazingira vizazi vijavyo.
10. ECONOMIOLOGY (ECONOMICS): Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, uchumi ni mfumo unaojumuisha mambo makuu manne, yaani michakato ya kiuchumi, kanuni za kuratibu uchumi, tunu za kijamii, na mfumo wa haki na majukumu ya kiuchumi (economic processes, organizing principles, social values, and economic justice); kwamba, kuna michakato mikubwa mitano katika sekta ya uchumi wa mahali popote duniani, kwa maana ya uzalishaji, usambazaji, mauziano, utumiaji wa huduma na bidhaa, na uwekezaji (production, distribution, exchange, consumption and investment); kwamba, kuna kanuni kuu tatu zinazotumika kuratibu michakato ya kiuchumi, kwa maana ya ushindani, ushirikiano, na uingiliaji kati kupitia mkono wa serikali ili kusimamia utulivu wa soko (competition, cooperation, and intervention); kwamba, kanuni ya ushindani inao msingi wake katika tunu ya kijamii iitwayo uhuru (freedom), kanuni ya ushirikiano inao msingi wake katika tunu ya kijamii iitwayo mshikamano (solidarity), na kanuni ya uingiliaji kati ina msingi wake katika tunu ya usawa (equality); kwamba, tunu ya uhuru inalindwa kupitia kanuni ya usawa katika michakato (procedural justice), tunu ya mshikamano inalindwa kupitia kanuni ya haki sawa katika kuchangia kapu la kodi ya Taifa (contributive justice), na tunu ya usawa inalindwa kupitia kanuni ya haki sawa katika kugawana kilichomo katika kapu la kodi ya Taifa (distributive justice); kwamba, uhuru wa kiuchumi, katika mipaka ya sheria, huleta utengamavu na tija; kwamba, ushindani wa soko, katika mipaka ya sheria, huleta ushirikiano ndani ya jamii; kwamba, hadhi ya ubinadamu inakubaliana na mabadilishano ya bidhaa na huduma yanayofanyika kwa amani, uhuru na bila ujanja, wizi wala kuvunja mikataba; kwamba, kumiliki mali binafsi ni jambo jema; na kwamba, kila binadamu anao uwezo wa kutumia talanta zake kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuzalisha mali kwa ajili yake na majirani zake.
11. EPISTEMOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, maarifa ni sentensi yenye kiima na kiarifa, yenye kuaminiwa na mtu fulani, ambapo sentensi hiyo inataja ukweli na ukweli wake umethibitishwa kwa kiwango kinachoifanya sentensi hiyi iaminike (justified true belief); maarifa yanaweza kupatikana kwa njia kama vile milango mitano ya fahamu (empiricism), yaani kuona, kusikia, kunusa, kugusa, kulamba; udadavuzi wa kimantiki hadi kufikia hitimisho lenye kuaminika kwa kuanzia kwenye umoja kwenda kwenye wingi (inductive rationalism); udadavuzi wa kimantiki hadi kufikia hitimisho lenye kuaminika kwa kuanzia kwenye wingi kwenda kwenye umoja (deductive rationalism); ushuhuda wa mtu mwingine maarufu mwenye busara kwa sababu ya kuyajua mapokeo (authority); maarifa yanayomfikia mtu binafsi kwa njia ya uvuvio binafsi (intuition); na maarifa yanayomfikia mtu binafsi kwa njia ya ndoto (revealation); kwamba, kila mfereji wa maarifa unazo faida na hasara zake; na kwamba, kazi ya umisionari unapaswa kuhusisha mafunzo juu ya vigezo vya kutofautisha ukweli na uwongo.
12. ESCHATOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, lugha inayotumika kuongelea mwishoni wa dunia hii na ujio wa dunia mpya ni lugha ya picha; kwamba, hii lugha ya kieskatolojia hutumia mbinu mbili kwa mpigo, yaani, ufananisho na ukinzani kati ya hali mbaya ya sasa na hali nzuri ya baadaye; kwamba, wakati katika dunia ya leo kuna mateso, njaa, kiu na kifo, katika dunia mpya mambo haya hayatakuwepo; kwamba, lugha ya kiestakotolojia hutumia mifano kutokana na maisha ya kila siku ya watu ili kuwaondolea hofu na kuwapa matumaini; na kwamba, kukoma kwa mbingu na nchi ya sasa na kisha ujio wa mbingu na nchi mpya unapaswa kutafsiriwa kitamathali kimaanisha safari ya kuondoka kwenye maisha duni kwenda kwenye maisha bora.
13. ETHICOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, malengo mema yanapaswa kufukuziwa kwa kutumia mbinu njema na sio kwa kutumia mbinu haramu; kwamba, wakati sheria kongwe ya madili asilia (old natural law) inaruhusu hitimisho lenye muundo wa kanuni ya kimaadili kuzalishwa kutokana na kanuni ya kimaumbile pekee; sheria mamboleo ya madili asilia (new natural law) inakataza hitimisho lenye muundo wa kanuni ya kimaadili kuzalishwa kutokana na kanuni ya kimaumbile pekee; na kwamba, katika suala hili, mamlaka kuu ya Kanisa inaona kwamba sheria kongwe ya madili asilia inakosea wakati sheria mamboleo ya madili asilia iko sahihi. Ukimya wa sasa unaendelea kuliweka Kanisa kwenye ukanda wa mashaka ya kimaadili.
14. ETIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, katika ulimwengu wa sababu na matokeo, tukio ‘c’ litakuwa limesababisha tukio ‘e’ endapo tukio ‘c’ ni jamii ya matukio ‘C’, tukio e ni jamii ya matukio E, tukio ‘c’ limetokea kabla ya tukio ‘e’, tukio ‘c’ na tukio ‘e’ yametokea katika eneo moja, na kihistoria jamii ya matukio ‘C’ huwa yanasababisha jamii ya matukio ‘E’ (regularity definition); Kwamba, tukio ‘c’ litakuwa limesababisha tukio e endapo tukio ‘c’ limetokea kabla ya tukio ‘e’, tukio ‘c’ na tukio ‘e’ yametokea katika eneo moja, na katika mazingira yenye parammeta zinazounda seti ‘K’, yamkini ya tukio ‘c’ baada ya tukio e kujiri ni kubwa kuliko yamkini ya tukio ‘c’ bila tukio ‘e’ kujiri (probability definition); kwamba, tukio ‘c’ litakuwa limesababisha tukio ‘e’ endapo tukio ‘c’ na tukio ‘e’ ni matukio ambayo yamefungamanishwa na mnyororo wa sababu na matokeo kiasi kwamba tukio ‘c’ ni pingili ya kwanza katika mnyororo huo wakati tukio ‘e’ ni pingili ya mwisho (process definition); Kwamba, tukio ‘c’ linaweza kusababisha tukio ‘e’ endapo kama tukio ‘c’ likitokea, basi tukio ‘e’ litatokea, na endapo tukio ‘c’ halitokei, basi hata tukio ‘e’ halitatokea (counterfactual definition); na kwamba, fenomena kama vile kuomba dua, kufanya sala ya mageuzi (transubstantiation), kufanya maombi, kufanya maombezi, na kuripoti matukio ya kimiujiza ambayo hayawezi kuelezwa kwa kutumia kanuni za kietiolojia zilizojadiliwa hapa, kwa sehemu kubwa, ni fenomena za kijamii zinazoongozwa na kanuni za maigizo ya kitamthiliya (fictionalism) zaidi kuliko kanuni zinazoratibu mifumo halisi ya sababu na matokeo.
15. HISTORIOLOGY (HISTORY): Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, historia hutufundisha kuhusu tulikotoka, tulipo katika wakati wa sasa, kutuonyesha tunakokwenda, na kutuwezesha kuamua tunakopaswa kwenda, kulingana na majumuisho ya vekta za kihistoria; na kwamba, vekta za kihistoria zinaonyesha kwamba, safari ya wanadamu inaanzia kwenye matatizo kuelekea kwenye majawabu, kwa msaada wa mipango thabiti, utekelezaji wa mipango hiyo, na tathmini ya mara kwa mara ya utekelezaji huo; na kwamba, katika mchakato huu, binadamu hutumia akili na utashi kuamua juu ya hatma yake.
16. JURISIOLOGY (JURISPRUDENCE): Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, lengo la kutunga sheria ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kuishi katika jamii yenye usalama, amani na utulivu kwa kuhakikisha kwamba watu watakatifu (innocent) wanalindwa na wakosefu (guilty) wanaadhibiwa; kwamba, kuna undugu wa karibu kati ya sheria za bunge na sheria za maadili kwa sababu sheria za bunge ni kanuni zinazotokana na sheria ya maadili asilia kuhusu mema na mabaya zilizoandikwa katika moyo wa kila mtu; kwamba, sheria zote lazima zitangazwe kabla ya utekelezaji wake ili watu wajue nini kinaruhusiwa na kipi kinakatazwa; kwamba, sheria hazipaswi kutumika kuadhibu makosa yaliyotendeka kabla hazijatungwa; kwamba, sheria zinapaswa kuandikwa bila kuacha utata kwa wasomaji; kwamba, sheria zinapaswa kuandikwa katika namna inayoondoa mgongano kati yake; kwamba, sheria lazima ziwe zinaweza kufuatwa na wananchi kwa urahisi; kwamba, sheria hazipaswi kubalishwa mara kwa mara kiasi cha kuwanyima nafasi wananchi kuzielewa na kuzifuata; na kwamba, mamlaka ya nchi inapaswa kusimamia sheria zilizotungwa kihalali na Bunge.
17. MATRIMONIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kila ndoa inajumuisha, sio tunu mbili za umoja na uzazi pekee, bali tunu tatu, yaani tunu ya umoja wa mke na mume, tunu ya uzazi wa watoto na tunu ya utulivu wa kimwili na kiriho (unitive, procreative and integrative goods); Kwamba, kuzaa watoto kwa kuzingatia kasi ya uzazi (birth rate) inayoleta furaha na amani kwa watoto na wazazi ni lengo zuri kimaadili, japo mbinu za kufanikisha lengo hili zaweza kuwa halali au haramu kimaadili, kulingana na wahusika pamoja na mbinu itakayotumika kuzuia ujio wa mimba isiyotakiwa kwa mujibu wa kasi ya uzazi iliyochaguliwa na wazazi; Kwamba, ndani ya ndoa kama taasisi ya umoja na uzazi (marriage as a unitive and procreative society), kitendo cha kuzuia ujio wa mimba isiyotakiwa kwa mujibu wa kasi ya uzazi iliyochaguliwa na wazazi ni haramu kila wakati na kila mahali; Kwamba, ndani ya ndoa kama taasisi ya umoja, uzazi na utimilifu (marriage as a unitive, procreative and integrative society), kitendo cha kuzuia ujio wa mimba isiyotakiwa kwa mujibu wa kasi ya uzazi iliyochaguliwa na wazazi sio haramu kila wakati na kila mahali; Kwamba, ndani ya ndoa kama taasisi iliyozaliwa kutokana na mabadilishano ya haki za kimwili yaliyofanyika kwa mujibu wa kanuni ya zawadi, basi, kuna mahusiano yasiyoweza kutenganishika kimaadili kati ya tunu za umoja, uzazi na utimilifu, hadi kifo kinapowatenganisha wanandoa.
18. ONTOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, msingi wa kimetafizikia wa mafundisho ya Kanisa kuhusu vitu visivyoonekana wala kugusika (abstract objects) kama vile mbingu, jehanamu, Malaika, Mungu, na shetani, ni fictionalism, au conceptualism, au nominalism, lakini sio realism;
19. PHYSICOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, dunia ni ulimwengu wa kimakanika (mechanistic system) unaoongozwa na kanuni za fizikia, kemia na bayolojia pekee; Kwamba, kauli juu ya vitu vinavyoweza kuthibitishwa kwa njia ya milango ya fahamu yafaa zithibitishwe kwa njia ya utafiti badala ya kusikiliza misahafu innasemaje, kwani tayari tunajua ina dosari tangu enzi za Galileo; Kwamba, sayari, nyota na mwezi havisukumwi na Mungu kama Biblia inavyosema, na badala yake vinazunguka kwa kuongozwa na kanuni za fizikia, na hasa Kanuni ya Tatu ya Mwendo kwa mujibu wa Newton; Kwamba, Kanuni ya Tatu ya Mwendo kwa mujibu wa Newton imeweka msingi wa kutofautisha kati ya sababu za kihistoria (efficient cause) na sababu za kiteliolojia (final cause), kwani, sayansi haiwezi kubaini sababu za kiteliolojia ambazo zinaanzia kwenye kichwa cha mwamuzi asiyeweza kuonekana popote; Kwamba, sio dunia wala jua ambacho ni kitovu cha ulimwengu kwa sababu ulimwengu ni kama tufe kubwe lenye uwazi na ambalo kipenyo chake kinaongezeka kila siku, ndani mwake kukiwa na makundi nyota (galaxies) yapatayo milioni 30, ambapo sayari ya dunia ni sehemu ya kundi nyota mojawapo linaloitwa "kundi nyota lenye rangi ya maziwa" (Milky Way).
20. POLITOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli Kwamba, katika jamii za kidemokrasia, utofauti wa itikadi mtambuka zinazopatikana katika jamii husika ni jambo la kudumu; Kwamba, katika jamii za kidemokrasia utiifu wa jumla kwa fundisho moja la kidini, kifalsafa, au maadili unaweza tu kupatikana kupitia matumizi ya mabavu ya kiserikali; Kwamba, katika jamii za kidemokrasia, utawala unaodumu na ulio salama, usiogawanyika katika matabaka ya kijamii yenye uadui kwa sababu ya mafundisho yenye kupingana, lazima uungwe mkono kwa hiari na angalau idadi kubwa ya raia wake; kwamba, katika jamii za kidemokrasia, tunahitaji mwafaka wa kitaifa wenye kuunganisha itikadi mtambuka zilizopo (the overlapping consensus of reasonable comprehensive doctrines in a pluralistic society) ili mwafaka huo uwe msingi wa haki ya kijamii katika Taifa; Kwamba, katika jamii za kidemokrasia, wananchi wanaojihusisha na shughuli za kisiasa wana wajibu wa kufuata ustaarabu wa kuhalalisha maamuzi yao kuhusu masuala ya kimsingi ya kisiasa kwa kuzingatia tunu na kanuni za pamoja kuhusu mijadala ya umma; na kwamba, katika jamii za kidemokrasia, kwa sababu mbalimbali, haiwezekani kwamba mijadala ya kimantiki peke mara zote italeta mwafaka wa kitaifa juu ya masuala muhimu ya kimaadili, kidini na kifalsafa, kiasi kwamba, makubaliano hayo yanapaswa kupatikana tu kwa msaada wa matumizi ya mabavu ya kiserikali; kwamba, kazi ya serikali ni kusimamia maslahi ya pamoja katika Taifa; kwamba, njia bora ya kuendesha taifa la kidemokrasia ni kutenganisha madaraka ya Bunge, Mahakama, na Serikali, kiasi kwamba, hakuna mhimili wenye uwezo wa kuuburuza mhimili mwingine; kwamba, kanuni ya demokrasia isemayo kwamba “wengi wape, wachache wasikilize,” inapaswa kuwekewa mipaka kwa ajili ya kudhibiti uwezekano wa wingi wa wapiga kura kumeza ubora sera za kitaifa; kwamba, katika Taifa la kidemokrasia ambako kuna utitiri wa itikadi za kidini, njia salama ya kudumisha umoja wa kitaifa ni kutenganisha taasisi za kidini na shughuli za kidola, kwa kiwango ambacho kinatoa nafasi kwa Taifa kuwa na “majukwaa ya umma” (public reason squares) ambako kila mtu anaweza kuingia, akakutana na wenzake, wakiwa wanajiona na kuonekana kama watu wa Taifa moja; kwamba, “majukwaa ya umma” yanayopendekezwa ni pamoja na mashule, vyuo vya elimu ya juu, vyombo vya habari vya serikali, na maofisi yanayotumiwa na watumishi wa umma wapatao 500,000; na kwamba, katika “majukwaa ya umma” itikadi ya kitaifa, yenye msingi wake katika sheria asilia ya maadili (natural moral law), kama inavyotafsiriwa na vyombo vya dola vyenye weledi stahiki, inapaswa kufundishwa kila siku na kwa kila mtu bila kuchoka; kwamba, sare za wanafunzi wa shule za awali, msingi na sekondaru ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kujenga Utaifa miongoni mwa kizazi kichanga; kwamba, shule zinazomilikiwa na taasisi za dini kwa ajili ya kuandaa makuhani, mashehe na viongozi wengine kama hao hazipaswi kuhesabiwa kama “majukwaa ya umma,” kwani zinakuwa na malengo maalum ya kitaasisi.
21. PRAXIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kwa mujibu wa mtindo wake wa utendaji kazi, matukio kama vile ibada, kusali rozari na kukutana kwenye jumuiya ndogo ndogo za Kikristo yanapaswa kuakisi kwa ukamilifu itikadi ya Kanisa kama ilivyojadiliwa kwenye mapendekezo haya hapa; kwamba, matendo ya rozari yanapaswa kuongelea haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya, kijinsia, na kimazingira badala ya kurudia rudia sala na kujadili historia Mashariki ya Kati bila kuonyesha uhusiano wake na Kanisa mahalia; kwamba, kalenda ya masomo ya Kanisani (liturgical calendar) inapaswa kupangiliwe kwa kuzingatia mgawanyo wa haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya, kijinsia, na kimazingira badala ya kurudia rudia sala na kujadili historia ya Mashariki ya Kati bila kuonyesha uhusiano wake na Kanisa mahalia; na kwamba, mfumo wa utendaji kazi wa Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo unapaswa kupangiliwe katika namna ambayo inawaruhusu waumini kujadili changamoto za maisha yao kulingana na haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya, kijinsia, na kimazingira badala ya kurudia rudia sala na kujadili historia ya Mashariki ya Kati bila kuonyesha uhusiano wake na Kanisa mahalia;
22. PSYCHOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, king'amuzi cha kibinadamu (human mind) ni roho inayojidhihirisha katika umbo la akili na utashi, mithili ya akili na utashi vilivyoko katika king'amuzi cha ki-Mungu (divine mind), ambaye ni mfano asilia wa uperisona wa kibinadamu.
23. SACRAMENTOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kuna sakramenti nane zifuatazo: ubatizo, kitubio, ekaristi, kipaimara, mpako wa wagonjwa, ndoa, upadirisho, na sakramenti ya kazi; kwamba, sakramenti ya kazi ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kuliweka Kanisa karibu zaidi na wavujajasho wanaojaribu kumfuata kwa vitendo Kristo Mfanyakazi; na kwamba, sherehe za kisakramenti zinapaswa kufanyika katika namna ambayo inaashiria kumbukizi ya kazi za Yesu Kristo, badala ya kuziendesha kana kwamba ni matukio ya kimiujiza ambako, kwa hakika kanuni za kietiolojia zinawaruhusu wanadamu kuongea na Mungu, Malaika na watakatiifu.
24. SEXOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kwa mujibu wa anatomia katika ngazi ya jenitalia, watu wote duniani ama ni wanaume, wanawake, au mahunta; kwamba, kwa mujibu wa sumaku ya kijinsia watu wote duniani wanagawanyika katika makundi matatu ya heterofilia, homofilia na ambifilia; kwamba, tendo la ngono ambalo milango yake ya kukaribisha uhai katika ngazi ya kifiziolojia imejifunga, na wahusika wanajua hivyo, haliwezi kuhesabika kama tendo ambalo ni rafiki wa uhai kwa sababu tu kwamba milango yake ya kukaribisha uhai katika ngazi ya dhamira iko wazi (a genital-to-genital coital activity which is known by participants to be intrinsically closed to life at a physiological level cannot simultaneously be open to life simply because it is open to life at an intentional level); na kwamba, kuna ufanano mkubwa kati ya wanaume na wanawake, kuliko utofauti uliopo kati yao;
25. SOCIOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, jamii ya wanadamu hustawi na kutekeleza majukumu yake vizuri zaidi kama ikikubali na kuenzi ukweli ufuatao: kwamba kila taasisi za kijamii kama vile familia, dini na dola, ni kama tufe la himaya huru, lenye haki ya kujitawala bila kuingiliwa wala kuingilia haki za kujitawala za matufe baki; kwamba, familia ya baba, mama, watoto (BMW) ndio kikonyo cha maisha ya jamii yenye amani; na kwamba, maamuzi ya kutatua matatizo hufanyika vizuri zaidi kama yakifanyika karibu zaidi na watu au mahali ambako tatizo husika limezaliwa.
26. THANATOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, kitendawili cha kifo ni kama mti wenye matawi mengi; kwamba, kitendawili cha kifo huambatana na changamoto za kisaikolojia, ambapo wafiwa huhuzunika na kutaharuki; kwamba, kitendawili cha kifo huambatana na changamoto za kisheria kuhusu haki ya maiti kuzikwa kwa heshima stahiki, watu wenye jukumu la kuzika mwili wa marehemu, na haki za warithi wa mali za marehemu; kwamba, kitendawili cha kifo huambatana na changamoto za kibayolojia kuhusiana na fasili ya kitabibu ya kifo, sababu za kifo cha marehemu, na michakato ya kibayojikemia itakayofuata mara tu baada ya mwili kuzikwa kaburini; kwamba, kitendawili cha kifo huambatana na changamoto za kiteolojia na kimaadili, kuhusiana na tabia za marehemu wakati wa uhai wake, uwezekano wa roho yake kwenda mbinguni au kwenda jehanamu, ambapo swali kuhusu mbingu na jehanami ni wapi huweza kuibuka; kwamba, kitendawili cha kifo huambatana na changamoto za kiuchumi na kijamii kuhusiana na uendeshaji wa msiba; kwamba, kitendawili cha kifo huambatana na changamoto za kimetafizikia kuhusu swali la kifo ni kitu gani na sio kitu gani, ambapo wakati wa mazishi na katika kipindi cha msiba ni majira mwafaka ya kutafuta jawabu kwa swali hili; na kwamba, ni kazi ya Kanisa kusaidiana na wafiwa kutatua changamoto hizi zote.
27. THEOLOGY: Kwamba kuna Kanisa linalotambua, kufundisha na kusisitiza ukweli kwamba, Kanuni ya Imani ya Mitume, Kanuni ya Imani ya Nikea, Kanuni ya Imani ya Constantinopoli, na Kanuni ya Imani ya Mt. Athanazi, kila moja kwa namna yake, inafundisha kwa mpigo kwamba “Mungu ni mmoja” na kwamba “Miungu ni wanne,” jambo ambalo linamaanisha mkanganyiko wa kimantiki unaobatilisha teolojia ya Mungu ambayo tunaiimba kila siku wakati wa Misa; kwamba, mkanganyiko katika mafundisho ya kiteolojia kuhusu Mungu unamaanisha kwamba hayo ni mafundisho ya uwongo, kwa kuwa ndani ya Mungu hakupaswi kuwa na mkanganyiko; na kwamba, dhana ya Mungu tuliyo nayo Wakatoliki ni dhana iliyo tofauti na dhana za Mungu walizo nazo Madhehebu kama vile Waanglikana, Walutheri, na Wasabato, kiasi kwamba, katika mazoea madhehebu haya yanaabudu miungu tofauti; kwamba, teolojia ya mahusiano yanayopaswa kuwepo kati ya madhehebu ya kidini na dola inapaswa kuongozwa na ukweli kwamba kila dhehebu linamwabudu Mungu wake.
VI. KIAMBATANISHO CHENYE KUORODHESHA MASWALI MADOGO YA SINODI
Kwa ajili ya kurahisisha utoaji na ukusanyaji wa maoni, swali kuu la dodoso limegawanywa katika maswali madogo 50 yanayoanguka katika sehemu kumi zifuatazo:
- Sinodi kama safari ya Pamoja,
- Utamaduni wa kusikiliza,
- Utamaduni wa kuzungumza,
- Kuadhimisha Ekaristi,
- Kuwajibika kwa pamoja katika utume,
- Mazungumzo katika kanisa na jamii,
- Kushirikiana na madhehebu mengine ya Kikristo,
- Mamlaka na ushiriki,
- Kutambua na kuamua, na
- Kujiunda katika sinodi.
Maswali kuhusu Sinodi kama safari ya Pamoja
Ikizingatiwa kwamba, katika Kanisa na katika jamii, tuko bega kwa bega katika safari ile ile:
1. Katika Kanisa lako mahalia, ni akina nani “wanaosafiri pamoja”?
2. Tunaposema: “Kanisa letu,” ni nani aliye sehemu yake?
3. Ni nani anayetuuliza tusafiri pamoja?
4. Watu tunaoandamana kwa pamoja barabara ni akina nani?
5. Je Watu tunaoandamana kwa pamoja wanahusisha wale walio nje ya mipaka ya kanisa?
6. Ni watu au makundi gani yameachwa pembeni, kwa uwazi au kwa hakika?
Maswali kuhusu Utamduni wa kusikiliza
Kwa kuzingatia kwamba, kusikiliza ni hatua ya kwanza, lakini inahitaji kuwa na akili na moyo wazi, bila chuki:
7. Je, Kanisa letu “linahitaji kumsikiliza nani”?
8. Je, Walei, hasa vijana na wanawake, wanasikilizwa vipi?
9. Je, tunaunganishaje mchango wa Wanaume na Wanawake Waliowekwa wakfu?
10. Je, kuna nafasi gani kwa sauti ya walio wachache, waliotupwa na waliotengwa?
11. Je, tunatambua chuki na fikra potofu zinazozuia usikilizaji wetu?
12. Je, tunayasikilizaje mazingira ya kijamii na kitamaduni yanayotuzunguka?
Maswali kuhusu Utamaduni wa kuzungumza
Kwa kuzingatia kwamba, wote wanaalikwa kuzungumza kwa ujasiri na kwa kuunganisha uhuru, ukweli, na upendo:
13. Tunakuzaje mtindo huru na wa kweli wa mawasiliano ndani ya jumuiya na mashirika yake, bila undumilakuwili na ukinyonga?
14. Tunakuzaje mtindo huru na wa kweli wa mawasiliano katika jamii ambayo sisi ni sehemu yake?
15. Ni lini na jinsi gani tunaweza kusema yaliyo muhimu kwetu?
16. Je, uhusiano na mfumo wa vyombo vya habari (sio vyombo vya habari vya Kikatoliki pekee) hufanya kazi vipi?
17. Ni nani wanaozungumza kwa niaba ya jumuiya ya Kikristo, na wanachaguliwa jinsi gani?
Maswali kuhusu Kuadhimisha Ekaristi
Kwa kuzingatia kwamba, "kusafiri pamoja" kunawezekana tu ikiwa kunategemea kusikiliza Neno la jumuiya na adhimisho la Ekaristi:
18. Je, sala na maadhimisho ya kiliturujia hututia moyo na kuelekezaje “kusafiri pamoja”?
19. Je, sala na maadhimisho ya kiliturujia yanahimizaje maamuzi muhimu Zaidi miongoniwetu?
20. Je, tunakuzaje ushiriki hai wa Waamini wote katika liturujia na utendaji wa kazi ya kutakatifuza ulimwengu?
21. Je, ni nafasi gani zinatolewa kwa ajili ya watoa huduma za usomaji wa masomo Kanisani?
Maswali kuhusu Kuwajibika kwa pamoja katika utume
Kwa kuzingatia kwamba, sinodi iko katika huduma ya utume wa Kanisa, ambapo washiriki wake wote wameitwa kushiriki, kwa vile sisi sote ni wanafunzi wa kimisionari:
22. Ni kwa jinsi gani kila mtu aliyebatizwa anaitwa kuwa mhusika mkuu katika utume?
23. Je, jumuiya inaunga mkono vipi wanachama wake waliojitolea kutumikia katika jamii (jitihada za kijamii na kisiasa, katika utafiti na mafundisho ya kisayansi, katika kukuza haki ya kijamii, katika ulinzi wa haki za binadamu, na katika kutunza Nyumba ya Pamoja, n.k.) ?
24. Je, unawasaidiaje kuishi ahadi hizi katika mantiki ya utume?
25. Je, utambuzi kuhusu maamuzi yanayohusiana na utume hufanywaje, na ni nani anayeshiriki katika hilo?
26. Ni kwa jinsi gani mapokeo mbalimbali yanayounda urithi wa Makanisa mengi, hasa yale ya Mashariki, yanaunganishwa na kurekebishwa, kuhusiana na mtindo wa sinodi, kwa mtazamo wa ushuhuda mzuri wa Kikristo?
27. Je, ushirikiano hufanyaje kazi katika maeneo ambako Makanisa tofauti yapo?
Maswali kuhusu Mazungumzo katika kanisa na jamii
Kwa kuzingatia kwamba, mazungumzo ni njia ya ustahimilivu inayojumuisha pia ukimya na mateso, lakini yenye uwezo wa kukusanya mang’amuzi ya watu na watu:
28. Je, ni maeneo gani na njia gani za mazungumzo ndani ya Kanisa letu mahalia?
29. Je, tofauti za maono, migogoro na matatizo yanatatuliwa vipi?
30. Je, tunakuzaje ushirikiano na Dayosisi jirani, pamoja na miongoni mwa jumuiya za kidini katika eneo hili, pamoja na miongoni mwa vyama na mienendo ya walei, n.k.?
31. Je, ni uzoefu gani wa mazungumzo na ahadi ya pamoja tuliyo nayo na waumini wa dini nyingine na wasioamini?
32. Je, Kanisa linajadiliana vipi na kujifunza kutoka sekta nyingine za jamii: ulimwengu wa siasa, uchumi, utamaduni, jumuiya za kiraia, maskini?
Maswali kuhusu Kushirikiana na madhehebu mengine ya Kikristo
Kwa kuzingatia kwamba, mazungumzo kati ya Wakristo wa maungamo mbalimbali, yaliyounganishwa na Ubatizo mmoja, yana nafasi ya pekee katika safari ya sinodi:
33. Tuna uhusiano gani na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo?
34. Je, ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo wanahusika na maeneo gani?
35. Tumepata matunda gani kutokana na ‘kusafiri pamoja’ na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo?
36. Kuna matatizo gani kutokana na ‘kusafiri pamoja’ na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo?
Maswali kuhusu Mamlaka na ushiriki
Kwa kuzingatia kwamba, Kanisa la Sinodi ni Kanisa shirikishi na linalowajibika pamoja:
37. Tunatambuaje malengo ya kufuatwa, njia ya kuyatimiza, na hatua zinazopaswa kuchukuliwa?
38. Je, mamlaka yanatekelezwaje ndani ya Kanisa letu mahalia?
39. Je, ni kazi gani hufanyika kwa njia ya uwajibikaji wa Pamoja ndani ya kaniza mahalia?
40. Je, huduma za walei na utekelezaji wa wajibu kwa Waamini walei hukuzwaje?
41. Je, vyombo vya sinodi hufanya kazi vipi katika ngazi ya Kanisa mahalia?
42. Je, vyombo vya sinodi ambavyo hufanya kazi katika ngazi ya Kanisa mahalia vinatoa ushuhuda wenye manufaa?
Maswali kuhusu Kutambua na kuamua
Kwa kuzingatia kwamba, katika mtindo wa sinodi, maamuzi hufanywa kwa njia ya utambuzi, kulingana na maafikiano yanayotokana na utii wa kawaida kwa Roho:
43. Je, kwa taratibu na mbinu gani tunatambua pamoja na kufanya maamuzi?
44. Je, taratibu hizo za kufanya maamuzi zinaweza kuboreshwaje?
45. Je, tunakuzaje ushiriki mpana katika kufanya maamuzi ndani ya jumuiya zenye uongozi ulio na muundo wa hierakia?
46. Je, tunaelezaje uhalali wa mfumo wa maamuzi ndani nya Kanisa unaotenganisha awamu ya walei kutoa ushauri kwa makleri na awamu ya makleri kufanya maamuzi?
47. Je, ni kwa jinsi gani na kwa zana zipi tunakuza uwazi na uwajibikaji katika mfumo wa maamuzi ndani nya Kanisa unaotenganisha awamu ya walei kutoa ushauri kwa makleri na awamu ya makleri kufanya maamuzi?
Maswali kuhusu Kujiunda katika sinodi
Kwa kuzingatia kwamba, hali ya kiroho ya kusafiri pamoja inaitwa kuwa kanuni ya kielimu kwa ajili ya malezi ya utu wa kibinadamu na ya Mkristo, ya familia na jumuiya:
48. Je, tunaundaje watu, hasa wale wanaoshikilia majukumu ndani ya jumuiya ya Kikristo, ili kuwafanya wawe na uwezo zaidi wa “kusafiri pamoja,” kusikilizana na kushiriki katika mazungumzo?
49. Je, ni malezi gani tunayotoa kwa ajili ya utambuzi na utumiaji wa mamlaka?
50. Ni zana gani hutusaidia kusoma mienendo ya utamaduni ambamo tumezama na athari zake kwa mtindo wetu wa Kanisa?
VII. MAREJEO MUHIMU
Kwa ajili ya kuandika makala hii nimetumia marejeo mengi, lakini yaliyo muhimu zaidi ni haya yafuatayo, na mengi nimeambatanisha nakala tepe kwa ajili ya kujibu changamoto za kiepistemolojia kutoka kwa wasomaji:
- Beau Branson (2014), The Logical Problem of the Trinity, A Dissertation Submitted to the Graduate School of the University of Notre Dame in Partial Fulfillment of the Requirements for the Degree of Doctor of Philosophy.
- Bernard Lonergan (1956), Insight: A Study of Human Understanding (New York: Philosophical Library Inc.).
- Brian Dive (2020), Accountability and Leadership in the Catholic Church: What Needs to Be Improved (UK: Cambridge Scholars Publishing). (Attached)
- Brian Walsh and J. Richard Middleton (1984), The Transforming Vision: Shaping a
Christian Worldview, (Downers Grove: InterVarsity).
- CAO Qingyun(2015), "Aristotle on the Unity of Composite Substance," Front. Philos. China. 10.3: 457-473.
- David A. Noebel and Jeff Myers (2015), Understanding the Times: A Survey of Competing Worldviews,1st Ed. (Manitou Springs, Colorado: Summit Press, 2015). (Attached)
- James W. Sire (2009), The Universe Next Door: The Worldview Catalogue (InterVarsity Press). (Attached)
- James Olthuis (1989), “On Worldviews,” In: Paul A. Marshall, Sander Griffioen, and Richard J. Mouw, (Eds.), Stained Glass: Worldviews and Social Science (Lanham, Md: University Press of America, 1989), pp. 26-40, at 29.
- James W. Sire (2015), Naming the Elephant: Worldview as a Concept, 2nd Edition (Illinois: InterVarsity Press) (Attached)
- John Rawls(1987), "The Idea of an Overlapping Consensus," Oxford Journal of Legal Studies, 7.1:1-25.
- Joshua Hoffman and Gary S. Rosenkrantz (1998), "On The Unity Of Compound Things: Living And Non-Living," Ratio 11.3: 289-315. (Attached)
- Kabuye Uthman Sulaiman(2018), "Meaning, Classification, Epistemological Foundation and Significance of Worldview," Scholars Journal of Arts, Humanities and Social Sciences," 6.7:1318-1327.
- Manning, P. R. (2018). Disintegrating Worldviews and the Future of Catholic Education: Addressing the Deep Roots of Catholic Disaffiliation. Journal of Catholic Education, 21(2): 26-52.
- Rebekah Johnston (2013), "Marriage and the Metaphysics of Bodily Union: Framing the Marriage Debate," Social Theory and Practice, 288-313, at 296-98.
- Robert P. George (2001), The Clash Of Orthodoxies: Law, Religion, and Morality in Crisis (Wilmington, Delaware: ISI Books). (Attached)
- Robert Wuthnow (1993), Christianity in the Twenty-first Century: Reflections on the Challenges Ahead (New York: Oxford University Press). (Attached).
- Tuomas E. Tahko (2009), "The Law of Non-Contradiction as a Metaphysical Principle," The Australasian Journal of Logic, 7:32-47.
- William Lane Craig and Quentin Smith (1995), Theism, Atheism, and Big Bang Cosmology (Oxford: OUP). (Attached)
Shukrani kwa maelezo.
Kinachinishangaza ni uamuzi wa TEC kuondoa U na kuweka O yaani Kristu na Kristo. Hapa sielewi mantiki yake ni nini hasa kwetu Tanzania. Nimejaribu kufanya kautafiti kadogo tu kama ifuatavo:-
1.Kilatini - Jesus Christus (hii ndio lugha ya Kanisa Katoliki la Roma yaani Roman Carholic).
2. Kiarabu - Almasih Eisaa.
3. Kitaliano - Gesu Cristo.
4. Kigiriki - Iisous Christos.
5. Kireno - Jesus Cristo.
6. Kijerumani - Jesus Christus.
7. Kiingereza - Jesus Christ.
8. Kifaransa - Jesus Christ.
9. Kispaniola - Jesucristo na
10. Kiebrania - Yehoshua.
Mie ni Mroma Mkatoliki na nilipata Kipaimala mwaka 1972 na katika miongo yangu hii sita nilikuwa nafaham kwa hapa nchini neno Kristu linatumiwa na Roman Catholic (rejea vitabu vyote hapo nyuma) na neno Kristo linatumiwa na Protestants, cha ajabu sasa naanza kusikia watawa (wakike), wanakwaya, mapadre na baadhi ya viongozi wakigeuza gia angani kuelekea kile Protestants wanakitumia.
Pana maswali mawili najiuliza,
1. Maaskofu waliopita hawakuwa sahihi na
2. Makao Makuu (Vatican) kwa kutumia Kilatini hawakuweza kutumia O na badala yake waweke U. Nimepitiapitia baadhi ya sala kwa lugha hiyo nimekuta:-
Christi,
Christe,
Christum na sijaona Christo.
Tumsifu Yesu KristU.