Dola isije kuthubutu kuwapa wapinzani (CHADEMA) nchi

Hivi utajisikiaje Mtu uliyekuwa unamheshimu ghafla ukagundua dish limeyumba?
 
Kuipata hiyo katiba mpya ndio kimbembe, iliyopo sasa katiba mbovu unajua ambao wanamamlaka nayo kubadili unadhani watakubali kirahisi kuibadilisha hapo ndio nafasi ya mtu kama Jiwe inapokuja kwa sababu hawa akina Makamba hawa wezi katu kuibadilisha hata kwa dawa kwa sababu ndio inayowanufaisha wao zaidi kuliko sisimizi raia wakawaida. Yaani ni sawa na umeenda kwa seremala unamwomba akuchongee rungu la kumbondea akikosea kukuchongea sofa. Na ndio maana ni vyema CDM wakae pepembeni CCM ifumuliwe kutokea ndani.
 
Ccm nichama kilicho oza. Hilo halina ubishi, saizi wanawaza kuiba na kurithishana madaraka wazazi kwa watoto. Chedema uchaga unakigharimu. Act ni udini mtupu. Tuvyama twingine ni pet parts
 
Naunga mkono maoni yako kwa 100% isipokuwa natofautiana na wewe hapo kwenye maandishi meusi kwa 100%.
 
Naandika hapa na anayepinga apinge siwezi kupigia kura chadema mpaka nakufa ...Mtafanya makosa yote siwezi kupigia kura chadema mpaka kauli ya mwisho hata kiwe chama cha dola ya kiislamu wakiungana na chadema tu basi kwangu ni sumu.

Bora tuendelee na mgao wa maji na umeme. Na trilioni 91 ya mikopo
 

Chadema haipo seriaklini lakini kutwa kuifatilia. Chadema haimo bungeni, halmashauri wala serikalini lakini unaongea utadhani chadema ndio imeleta mgao wa maji na umeme au imekopa trilioni 91. CCM muipe kura halafu lawama kwa chadema.
 
H
Wapinzani hawajielewi..ccm haiminiki tena yani ni vurugu mechi.

Ila kwa ccm hii bora hata jeshi lishike hatamu.

#MaendeleoHayanaChama


Achana na upinzani kama haujielewi baki CCM hujalazimishwa. Mnaipa kura CCM kwa maringo lakini kutwa lawama akwa upinzani kana kwamba inaongoza serikali.
 
Bora ushabikie Yanga kuliko Chadema ya mlevi baba Joyce

Chadema itakutesa sana. Na bado deni limefika trilioni 91 na tozo juu. Huku mgao wa maji kule ajira hakuna. Unaichukia CHADEMA wakati CCM inatawala nchi kwa asilimia 90%
 

Naona kampeni ya kulazimisha ndoa ya CCM na CHADEMA. 2020 mliwananga chadema leo mnalazimisha kwamaba wapo pamoja na CCM.
 
True chadema ikishika njee tutakuwa kwenye njaa sana ya kufa mtu .
Tutakuwa somalia wale ni mafisi makitu wabaya we Mungu tuepushie na waovu washetani CHADEMA
 

Punguza hasira ndugu, naona mgao wa umeme na maji umekukasirisha sana.
 
Ccm nichama kilicho oza. Hilo halina ubishi, saizi wanawaza kuiba na kurithishana madaraka wazazi kwa watoto. Chedema uchaga unakigharimu. Act ni
u udini mtupu. Tuvyama twingine ni pet parts

Tatizo serikali ilishatugawa wananchi hatuongei kwa kauli, tunachukiana ili kuwafurahisha wanasiasa ndio maana wanakopa deni mpaka linafika trilioni 91, ambalo hao wananchi waliogawanywa watalilipa. Tanzania itabadilika siku wananchi tutakapokuwa kitu kimoja.
 
True chadema ikishika njee tutakuwa kwenye njaa sana ya kufa mtu .
Tutakuwa somalia wale ni mafisi makitu wabaya we Mungu tuepushie na waovu washetani CHADEMA

Punguza hofu, chadema imesema haitashiriki uchaguzi wowote so mtabaki na CCM yenu miaka mia. Unahofu gani?.
 
Mission ya CHADEMA na CCM kwa nchi yetu Tanzania imeisha na sasa inatupeleka kupata Katiba Baada ya hapo ndipo tutapata muelekeo mpya wa Taifa letu!!

TUSUBIRI

Punguza unafiki. Mission ipo kwa ccm yenyewe ndio imeongoza nchi kwa miaka 60, chadema mission yake bado. Acha kulazimisha ndoa ya CCM na CHADEMA kwa uongo wako.
 
Ccm mbovu, chadema/wapinzani mbovu. Kati ya ccm na chadema nani atawale kama hakuna chama bora ccm.
 
Bora jeshi kuliko hao wapinzani mzee .

Mwenzako kakwambia bora jeshi kuliko CCM , wewe umekimbilia bora jeshi kuliko upinzani. Punguza chuki, CCM imeshika madaraka kwa asilimia 98 lakini wewe umekazana na upinzani ambao hawapo kwenye vyombo vya maamuzi.
 

Kweli ugumu wa maisha umewapa watu stress.
 

Maandamano ya mwisho CHADEMA yalifanyika lini?. Maana unaongea kana kwamba kila siku maandamano yanaiyishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…