Dola isije kuthubutu kuwapa wapinzani (CHADEMA) nchi

Dola isije kuthubutu kuwapa wapinzani (CHADEMA) nchi

..usaliti wa Ccm unaonekana ktk hali yetu kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

..Nitakupa mfano mdogo. Ndege yetu imekamatwa kwasababu tunadaiwa bilioni 300+.

..Tunadaiwa kwasababu kuna mwana-Ccm alisaini mkataba mbovu. Halafu kuna mwana-Ccm mwingine kavunja mkataba kipumbavu. Matokeo yake ni hasara ya billioni 300+.

..Hizo billioni 300 ni zaidi ya bajeti ya maendeleo ya KILIMO kwa mwaka mzima.

..Wale kina mama wamesaliti chama chao.

..Ccm wanasaliti Watanzania. Hizo billion 300+ zitalipwa kwa kodi, na tozo, tunazokamuliwa mimi na wewe.

..Unaweza kushabikia Ccm, lakini make sure wanakulipa vizuri na kumaliza shida zako zote.
Dawa yake sio Chadema Bali Katiba bora
 
Sijakataa kama ccm ni mbovu maana ndo imetuletea umaskini..Ila note maneno yangu Cdm haifai kabisa .


..What are your dreams for your country?

..Ukiangalia miaka 60 ya utawala wa Ccm, unaona ndoto zako kwa Tanzania zikitimia?
 
stori za vijiweni huku niliko raia walichoma road kisa walitangaza mgombea wa CCM wakati wao kura walizihesabu CDM walishinda, wakala virungu night kali vya jwtz
Hiki ilichfanyika ni uhuni tu wala siyo mamlaka stahiki za kidola. Chanzo cha uhuni huu ni katiba mbovu ambayo pia inazaa tume mbovu ya uchaguzi inayoruhusu chama tawala kuvitumia vyombo vya dola kufanya vitu vya hovyo.
 
..What are your dreams for your country?

..Ukiangalia miaka 60 ya utawala wa Ccm, unaona ndoto zako kwa Tanzania zikitimia?
Tunahitaji transition especially political, Tena chama kipya sip walevi.
 
Wa kulaumiwa ni serikali kuruhusu vyama vya ukoo kufanya siasa za kitaifa.๐Ÿ˜…


Screenshot_20221212-215906.png
 
Ishu hata sio katiba mpya ki vile ni kutii hiyo katiba, labda uniambie mpya itaondoa immunity aliyowekewa Mheshimiwa, dola ndio inayoishikilia hiyo katiba mbovu inayoipa moo pawa unadhani itaiachia kirahisi, yaani katiba iliyopo tu haifuatwi. Unadhani ikiwa katiba mpya ndio itafuatwa na ili uipate kumbuka inabidi mkubaliane na walioshika dola sasa hivi, CCM.
Hiki ilichfanyika ni uhuni tu wala siyo mamlaka stahiki za kidola. Chanzo cha uhuni huu ni katiba mbovu ambayo pia inazaa tume mbovu ya uchaguzi inayoruhusu chama tawala kuvitumia vyombo vya dola kufanya vitu vya hovyo.
 
Tunahitaji transition especially political, Tena chama kipya sip walevi.

..Hujanijibu swali langu.

..What are your dreams for your country?

..Baada ya kushuhudia uongozi wa Ccm tangu uhuru, unaamini ndoto na matarajio yako yatafikiwa?
 
CHADEMA INAPIGIWA KURA NA WENYE AKILI NI MJINGA TU AMBAYE HAJUI UMUHIMU WA UPINZANI NDIO HATA IPIGIA KURA CHADEMA
Chadema familia zao wamezificha ughaibuni. We kufa njaa kwa kuishabikia chadema wale siyo wenzako na hawapo kwa ajiri yako
 
Chadema familia zao wamezificha ughaibuni. We kufa njaa kwa kuishabikia chadema wale siyo wenzako na hawapo kwa ajiri yako
Halafu maneno haya ya kipuuzi unakuta yanatoka kwa mtu alie na dhamana ya kutoshiriki siasa
 
Hawa watu ,uzalendo wao ni zero, Wabinafsi , na kila kukicha wanazidi kuweka wazi sura zao asili, hata iweje Hawa watu wasipewe Nchi, wawe wanapewa ubunge tu

Naam kwakua, Chama Cha mapinduzi ndicho kilichojishikanisha na Dola Moja Kwa Moja.

Basi, Dola ni vema ikahakikisha inatawala kama Ulivyo Utawala wa China.

Yaan tupate CCM ambayo Ina watu wenye Uchungu, Uzalendo, Watu watakaoipenda Nchi Yao, nakulinda mali Asili za Nchi hii pamoja na utajiri wake. Watu ambao watatanguliza Maisha Yao mbele Kwa ajili ya kujenga Nchi hii.

CCM ya Akina Kinana, Makamba, JK, Yusuph, Nape, hiii haitokaa kutuvusha.

Tunahitaji CCM yenye U-Magulification, Mkono wa Chuma wenye lengo la kuifikisha mbali Nchi hiii kama ilivyo UCHINA NA UTAWALA WAKE.

Kwa Sasa CCM ya Kinana ni sawa na CHADEMA TU, wote ni viburi, jeuri, ubinafsi!

Tunawataka akina Bashiru, Mpina, Akina Gwajima, Akina Kassim, tunawataka wawepo Akina Marehemu Mfugale wengi, Deo Filikunjombe wengiii!

Yangu ni hayo!
Wewe ni K
 
Ishu hata sio katiba mpya ki vile ni kutii hiyo katiba, labda uniambie mpya itaondoa immunity aliyowekewa Mheshimiwa
Katiba bora haiombi ama kumbembeleza mtu kuitii. Asiyeitii inamuadhibu.

Kuhusu immunity aliyo nayo rais kwa Sasa. Hili ni moja ya (ubovu) mapungufu makubwa ya katiba tuliyo nayo. Imagine rais yuko juu ya katiba. Yaani anaweza hata kuamuru kundi fulani, kabila fulani, ama wafuasi wa chama fulani wauawe. Halafu katiba yetu unasema hatahojiwa Wala kushitakiwa popote.

Pia rais anaweza kuuza kipande cha ardhi ya nchi hii bila waswasi waowote. Yaani mafano anaweza kuuza mlima Kilimanjaro, anaweza kuiuza mikoa ya kanda ya ziwa au kanda ya pwani ama kanda ya kati ama kanda ya kusini na sifanywe kitu.

Anaweza akaiba uchaguzi (siyo kuiba kura) kama alivyofanya Magufuli na asifanywe kitu
 
Back
Top Bottom