DPP, TAKUKURU na Polisi: Wasikilizeni CHADEMA. Kuna jinai kubwa imetendeka

Wafukuzwe tu hakuna namna
 
Wacha kutetemeka, wameshaitwa kujitetea, then after ndio maamuzi yatafanyika ya kuwachukulia hatua.
 
Hawatathubutu !!. Vyombo vyetu kama ni mtoto wa kambo havihusiki
 
Kama hawakuteuliwa na chadema kwanini wameenda bungeni? Taarifa kawapa Nani na Kama wao hawaafiki huo uteuzi wangekaa majumbani kwao waendelee na kazi zao za kila siku. Matiko kasema wameteuliwa na mamlaka husika na Kama Kuna lisiloeleweka majibu yatatolewa na msemaji wa chama, Sasa wewe hujaelewa Nini?
 
Alifukuzwa Silinde na Lijualikali kwenye chama ila nini kilitokea?
Hapa hata wakifukuzwa uanachama Ndugai akili zake anazijua mwenyewe
 
Siyo uharisia, ni uhalisia. Huyo mfungwa wa kisiasa aliyetolewa Gerezani alikuwa keshahukumiwa au kesi ilikuwa bado Mahakamani?
 
Ni jinai kwelikweli, lakini kwakuwa imefanywa na malaika wa Mungu, sina hakika hata CHADEMA wakienda mahakamani kama watabadili kitu! Nikikumbuka kilichofanyika kwa wale wabunge 8 wa CUF na wale wabunge 10 wa CHADEMA, I have lost my Credibility upon these organs!
 
Labda mimi ndo sielewi siasi, hao kina mdee walipewa taarifa na nani kwamba wameteuliwa na wanatakiwa kwenye kuapishwa bungeni?
Fuatilia haya mahojiano ya Matiko uone anavyojikanyaga

MWANDISHI: Mmepata baraka za Chama?

MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.

MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?

MATIKO: Na mamlaka husika

MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?

MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.

MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?

MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.

MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa

MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.

MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri

MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.
 
Nusrat
 

Umeandika mambo ya msingi sana, ila kwa Magufuli katiba ni sawa na gazeti la udaku. Na taasisi zote zinatii atakacho hata kama hawaafiki. Hayo ndio madhara ya katiba hii mbovu.
 
Mwaka 2020 kulikuwa na uchafuzi mkuu!
Katiba imevunjwa, sheria zimevunjwa.
Hamuutambui uchaguzi, na Magufuli ameshamaliza muhula wake. Ndiyo kusema Tanzania haina serikali (2020- 2025)
Sasa katiba imevunjwa, sheria zimevinjwa, hapo mnamtaka nani asimamie enyi uzao wa watu wasiojitambua?
DPP, TAKUKURU na Polisi, wasaidieni watanzania
Hizo zote ni taasisi za kiserikali, hapo nadhani unaongelea za serikali yenu ya Ubeligiji...
 
Usanii gani ?

Kazungukwa na nani ?
 
Na hii ni episode II ya kile walichofanyiwa CUF.
 
Wanaendaje Dodoma bila kutusainia fomu za makato ya wabunge kuimarisha Chama 😀😀
 
kupitia sentensi hiyo it means chama ndo kiliwachagua, ila kwa alivyomalizia inaonyesha kulikuwa na vuta nikuvute, na kwa hilo tatizo si bunge, wala ccm tatizo liko kwao wenyewe, waache kutafuta mchawi nani
 
Ahahahah nacheka lakini naogopa. Tatizo hiki tunachokifikiria sisi ata hao wahusika wa hii move walishakifikiria na walishajua jinsi ya kukabiliana nacho.

Kuna wana-nchi na wenye nchi ambao ndio wana mamlaka ya kuamua kesho yetu iweje, kama upo upande wa wananchi jaribu kuhamia upande wa wenye nchi angalau na ww ule mema ya nchi. Mshaambiwa "nitawalinda" bado mnataka wafukuzwe? Leo hii tumesahau ya Lijualikali, Silinde na Mwambe? Watoto wa mjini wanasema imeisha hiyo.

Sisi tujilie ugali wetu tu.
 
Muache bhana, Kwanini mnapenda kuwaintimidate watu?! Nyie mkimpost Mbowe kwa mikashfa kibao ya kutunga haiwagi provocation?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…