DPP, TAKUKURU na Polisi: Wasikilizeni CHADEMA. Kuna jinai kubwa imetendeka

Huenda TAKUKURU walijulishwa kabla nini kinaendela, hivyo hawawezi kuchukua hatua.
TAKUKURU? ile ile hadihi ya Nassari.. ni bora uwaandikie UN na Balozi zote kuwaambia uchafu huu kuliko kujichosha kuwatafuata Takukuru...ukifika kwao unawekwa ndani kwanza ueleze hizo docs za ushahidi umezipata wapi.
 
Tumieni hata hiyo akili ndgo mliyopewa na Muumba! Kada kindakindaki kama Mdee, Matiko na Bulaya hawawezi kwenda kuapa bila kwanza kuwasiliana either formal au informal na Mwenyekiti Mbowe!
Nakuhakikishieni wale wanazo baraka za Mbowe na haya matamko mengine ni maigizo tu!
 
Kama kuna mbunge kwenye bunge lililopita alifutwa uanachama na Spika akamtetea, basi tarajia hata hawa kina mama watatetewa na maisha yataendelea...

Kwa lugha nyingine, CDM imeshapigwa bao...
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA ametoa maelezo yaliyonyooka na bayana kabisa. Mimi pia nitashangaa ikiwa ofisi hizi za DPP , TAKUKURU, Polisi n.k kukaa kimya bila kuchukua hatua kuchunguza mchakato huu wenye kuonesha kuna kitu hakipo sahihi kabisa. Ajabu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alibariki uapishwaji wa wabunge wa viti maalum jana 24 November 2020.
 
Jinai kubwa ni kutopeleka majina ya viti maalumu na kuwanyima wawakilishi wa wananchi fursa
WEWE KWELI NI JINGALAO!! Kama chama hakikubali matokeo utakilazimisha kikupe wawakilishi wapi?? CCM si mlijinasibu MNATAKA Bunge la kijani, Sasa mbona mnatumia pesa za Umma kuwarudisha mliowaona hawafai?? CCM n hovyoo Sana kumbafuuuuuu zenu
 
Tanzania hakuna taasisi huru tena amebakia mtawala mmoja aliyejimilisha nchi wote watii hata aliamrisha wajiue hawatasita
 
Yani siuji uliwahi sikia hili neno maelekezo toka ngazi za juu?? basi ndo kinachofanyika, na hakuna takukuru yenye nguvu kufatilia mambo kama haya au ni aache kazi, muulize majaliwa wakati wa korosho aliambiwa nini
 
Afrika na haki ni vitu viwili tofauti, sisi kuitwa nyani ni hvyo bado tunaishi kwa "survivor for fitest"
 
Unaongea mambo magumu kama haya unadhani mzee Meko (Juha) anaweza kukuelewa??? Ufahamu wake umeishia kukariri definition ya catalyst na kuongelea wanawake weupe!
 
Chadema porojo tu kama wako serious wawachukulie hatua wao kwanza ndipo waite DPP wasitumie DPP kama kichaka cha kujificha mleta Mada usirukie kwa DPP

Tumekuwa tukisema Magu haheshimu katiba na sheria, na yote hiyo inatokana na kiburi cha madaraka. Tunaposema uchaguzi wa ujuzi wote haukuwa uchaguzi bali kilichofanyika ni kutii maagizo yake batili. Na lengo lake kubwa ni kukaa madarakani zaidi ya muda sahihi wa kikatiba.
 

Bado na maelezo yote marefu, bado hoja ya mleta uzi imekuwa ngumu kujibika. Zunguka na maneno ya kuokoteza lakini ukweli bad uko pale pale kuwa taasisi za nchi hii zinatumiwa na rais kuvunja na kutotekeleza sheria.
 
Hawana ubavu wa kufanya hayo. Take my word. Nchi imeoza hii.
 

Hujui matumizi ya cartoon? Lengo la katuni ni kutoa ujumbe kwa jamii. Je kuna uongo wowote kwenye hiyo cartoon?
 

Ni hivi, huu uzi haujibiki kishabiki, kila mtanzania anazidi kushuhudia matumizi mabaya ya madaraka ndani ya nchi hii toka tupate uhuru. Leta porojo zote utakazo, lakini huo ukweli wa matumizi mabaya ya madaraka kupitia taasisi uko wazi, hata kama watu wanaogopa kuongea ukweli kulinda uhai wao.
 
Mkuu za kuambiwa changanya na zako. Imeisha hiyooooooooooooooo
 
Majina yamepelekwa na Halima Mdee ambae ndio mwenyekiti wa wanawake wa CHADEMA

Na waliwahi kukaa na wa walikubaliana kuhusu kupeleka majina NEC nadhani Kuna sehemu walipishana kwenye Nani awepo na Nani asiwepo hapo ndio shida imekuja
Walikaa katika baraza lao kuu?!!!
 
Mde alikuwa hadharani na kuuleza umma kuwa ameona kwa macho yake kwenye jimbo lake karatasi feki za kupigia kura, hakukamatwa. hakuhojiwa na wala hakutakiwa kuonyesha ushahidi wake na yeyote yule. Mara tu jana ameenda kula kiapo kuitumikia serikali ambayo yeye mwenyewe amesema kuwa ni wezi wa kura. Sasa jiulize wewe mwenyewe, ikiwa umemuona mtu anakuibia kuku wako, halafu anakuita ukapate supu ya kuku kwa ahadi ya kukupa paja nono, utakubali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…