Utajiri wa Rasilimali ofcourse, shida ni kuweza kuzitumia hizo rasilimali ili ziingize pesa, shida ipo hapo tu. Ni kama sisi tunavyowekewa vikwazo vya kimazingira wakati wa ujenzi wa Rufiji, ona Lissu na Zitto wanavyotumika vibaya kukwamisha hili bwawa, ni ushenzi tu!
Kama nchi ina Demokrasia lazima maendeleo yafanyike kwa kasi.
Nchi isiyokua na Demokrasia inatumia nguvu kubwa sana kuleta maendeleo.
Kongo ilikwama kutokana na Ubabe wa Mabutu na familia yake kwa watu wa Kongo huku watu wa Chache wakiwa wanatumia muda mwingi kula raha za nchi na wengine wakiwa watumwa wao.
Hilo ndilo linaloikwamisha Afrika.
Udiikteta ni mgumu kutekelezwa kwa karne hii bila kuua sana mpaka ubakiwe na watu waoga tuuu na wanaokuunga mkono kwa kila jambo jambo ambalo sio rahisi mana Dunia na wanadamu walishatoka huko !
Hatuwezi kamwe kurudisha Afrika kwenye Udikteta kwa sababu kila kitu kinachoitwa maendeleo ni kile kilicholetwa na Mabeberu.
Hata hayo mabwawa ya Umeme sio urithi wa Mwafrika Bali ni Vitu vilivyoletwa na mabeberu. Meli ni mazao ya mabebebru,Treni ni mazao ya mabeberu, ndege ni mazao ya mabeberu , Mfumo wa kijeshi,polisi mpaka mitaala yao ni mazao ya mabeberu , Fedha ,mabenki,mikopo, mfumo wa utawala, mifumo ya kisiasa ya vyama kiwe kimoja au vingi, ulinzi na usalama wote ni mifumo ya kikoloni na mabeberu,mifumo ya mahakama ,mifumo ya bunge . Kila kitu ni mabeberu mpaka imani za hao wanaowapiga vita mabeberu nao wananyenyekea mbele ya Vatican .
Sasa kama tuna kila kitu cha Mabeberu halafu Leo wanatuambia kuwa tunakosea namna tunavyoanzisha mifumo ya kidemokrsia na namna tunavyofanya Chaguzi zetu na tunavyounda Serikali bila kushirikisha wadau wote na kuunda serikali za umoja wa kitaifa ili kila kitu tukipange wenyewe.
Hilo Bwawa la Kongo litajengwa na wachina lakini Rasilimali zao zitasombwa kwa matrilioni ya Tani kwenda China kuwanufaisha wachina huku wakongo wakiwa wanaikimbia nchi yao na kuitwa kupigana vita wenyewe kwa wenyewe.
Tatizo ni Uroho wa vyama vilivyoanza kutawala Afrika vilikosa dira za maendeleo kwa wote wakajikita kwenye kujenga misingi ya kusalia madarakani na kuwarithisha watoto wao na wajukuu zao.
Ukiwaehirikisha wapinzani wote kwenye Siasa na utawala kamwe vurugu na kutumiwa na Mabeberu haiwezekani milele.
Hata kwenye Familia baba au mama akionyesha upendeleo kwa baadhi ya watoto na kuwatenga wengine Chuki inajitokeza na Hata kutengena na kutothamini tena Mali ya familia na kuanza kuigombania.
Ndivyo wanavyofanya watawala wa Afrika.
Ni wakati sasa wa kuleta vyama vingine vyenye dira ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili tujenge maendeleo endelevu yenye kujengwa kwa mijadala mipana ya pamoja nje ya Bunge na baadae bunge lipitishe tu mana wabunge nao wamelewa kwa ahadi za vyeo na pesa.
Hii ndiyo Afrika yenye mipango ya Mabeberu kisha wanauana ili kuitekeleza.
Hakuna mpango mpya Afarika zaidi ya ile iliyoachwa na Mabeberu na vyama walivyoviamini na kuvikabidhi nchi . Hata Mobutu alikua ni Chaguo la Mabeberu huku akishirili kumuua Patrice Lumumba.
Kama tuna Gesi na mjadala ulifanyika kwa miaka namna ya tutakavyonufaika nayo . CCM hao hao wakatuaminisha kuwa tutakimbia na kuwa nchi yenye uchumi mkubwa sana huku pakiwa na Mfuko maalumu wa kuweka akiba ya Fedha kwa vizazi vijavyo . Ghafala utawala mwingine unakuja na kutuambia ule mradi ulikuwa ni wizi na ufisadi tu hauna maana tena kwa watanzania . CCM wale wale wanashangilia na kutuamisha kuwa tusiuendeleze tena. Lakini hapo suala ni kugombania pesa zinazotokana na Tenda .
Kila mmoja anawaza namna ya kuwajaza watu wa nyumbani kwakwe kwenye miradi mipya. Wivu uliopo ni kuona kuwa Walotangulia wamesha jaza watu wao kwenye miradi iliyopo. Kinachofanyika ni kuanzisha mingine tena yenye dili kubwa zaidi. Afrika hatuna mwendelezo wa alipoachia mtangulizi.
Kama tulianzisha miradi ya Gesi kwa nini tusingeikamilisha ili Fedha zake zitumike kuanzanisha miradi mingine ikiwemo ya Bwawa .
Tukiwa na serikali ya umoja wa kitaifa na sheria na katiba inayozuia upendeleo ,ukabila,udini, uvyama , Biashara kuchanganywa na madaraka,dola kujokita kwenye ukada wa chama kimoja kinyume cha katiba, kukataza wakuu wa majeshi kuwa makada wa vyama vya siasa. Baada ya hapo nchi inaweka vipao mbele vyake kwa miaka 50 ijayo kisha wanasiasa wanashindana namna ya kuvitekeleza.
Hapo hatuwezi kuvurugana na kutumiwa na Mabeberu mana kura za wananchi zitaheshimiwa na wananchi watajua nani atakatewafaa kwa sababu patakua na usawa katika kunadi Sera na kutoa taarifa kupitia vyombo vya umma.
Mfano mwaka huu watanzania kwa miaka mitano walinyimwa fursa ya kujua Sera za wapinzani kuanzia Bungeni zaidi walionyeshwa wakiwa wanapandishwa kwenye makarandinga wakiburuzwa magerezani kuonyesha umma kuwa hao ni wasaliti. Mbaya zaidi hata kwenye Kampeni hawapewi nafasi sawa na wale waliofanya siasa kwa miaka mitano.
Woga huu ndio unaopekeka taifa kwenye Udikteta kwa kuamini kuwa anachopanga mtu mmoja ndicho kinachokuwa Alfa na Omega na anayepinga anastahili kuondoshwa duniani.
Afrika tumejawa na Ubinafsi na uroho wa kutawala bila hata ridhaa ya wananchi.
CCM ilipokuja na Sera za kuvuruga Chaguzi waroho wote wa madaraka walikimbilia CCM kwa ajili ya kuneemeka huko na madaraka.
Wagombea ubunge kupitia CCM walikua zaidi ya 43,000 . Watu wanaotosha kupiga kura kwenye jimbo na kumchagua Mbunge kwenye jimbo lenye watu wengi sana . Hapo huwezi kutegemea kupata watu wenye nia ya dhati kuleta maendeleo yanayowagusa watu wenyewe zaidi ya kujikomba kwa watawala kwa lengo la kupata madaraka.
Na hata ukifuatilia kampeni za CCM zimejaa ahadi za kugawana vyeo na rushwa ya kuahidi madaraka na ajira.
.