Dubai: Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Uwekezaji ya thamani ya Trilioni 17

Mama kasema na itekelezeke, anatambua kusaini haimaanishi kwa wameyafanya. Na waowawekea vikwazo katikati kasema wampe taarifa.

Tuombee mikataba ya leo itimie, Mama anajua mwisho wa siku inaweza kati ya hiyo kama 36 ikatekelezeka hata mitano au chini ya hapo

Tabu Watanzania wanapenda rushwa sana sana na wengine wanataka chao kwa % wanayoitaja. na hii baadae wawekezaji wanakimbia.
 
Ni bahati Mbabane marekebisho haya hayapewi publicity ya kutosha ndani ya Nchi ila majariba mengi ya nje yameelezea hili hasa reformations za kisheria zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya 6
 
Sasa waarabu nao wakuchukulia serious kweli! Mambo muhimu ya nchi unawahusisha waarabu! Nadhani tumekosa tu cha kufanya kama nchi.
 
Sasa waarabu nao wakuchukulia serious kweli! Mambo muhimu ya nchi unawahusisha waarabu! Nadhani tumekosa tu cha kufanya kama nchi.
Waarabu walioajiri wazungu na wahindi wawafanyie kazi ndio hao tunaowafuata.

Zaidi ya fedha za mafuta waarabu hawana jambo lolote la maana la kufanya nao.
 
yani safari moja inaongeza deni la 14 trilion? Mgogo aliona mbali sana kwakweli
 
Soma uzi acha uvivu
Sekta zilizoguswa ni Kilimo, Madini, Utalii, Viwanda na Biashara

Maeneo wametaja mengi ikiwemo industrial parks za Kibaha na maeneo ya uwekezaji( Economic Zones)
Tanzania itajengwa na watanzania na siyo wawekezaji. Kuna hatari ya watanzania kuja kushika silaha siku zijazo ili kuikomboa tena Tanzania kutoka kwenye mikono ya wageni! Ni hatari sana kuwa na rais anayezunguka kuokoteza wageni eti anaijenga nchi yake!
 
Endelea kujidanganya. Nchi gani duniani imeendelea bila foreign investment?
 
Yule baba si katurudisha nyuma Mtwara ilikuwa inakuja juu
 
Semeni Wamasai wa Loliondo wajiandae kuamishwa,Mwarabu hawezi kuja kuwekeza huku,hakuna nchi hata moja Africa Mwarabu ambayo aliisha wahi fanya uwekezaji wa hivo.Mnaanza kuturetea ya Kikwete,siku moja alisaini mikataba karibu 300 na China,watu wakaanza kushangiria kuwa tunauaga umasikini,mpaka Sasa tulichoambulia ni Kikwete kupewa Uprofessor 🤣🤣🤣 watanganyika ni wepesi kudanganyika
 
AJIRA LAKI MBILI TU KWENYE AWAMU ILIYOPITA AMBAYO YEYE ALIINADI WALITO AJIRA MILIONS 8 NA KUJENGA VIWANDA 8000 KWA MIAKA 4
 
Wawekezaji muhimu tena mno
Zimbabwe uchumi ulikufa sababu ya kufukuza wawekezaji

Wazungu waliwekeza sana kwenye kilimo na ufugaji Zimbabwe mazao yao na mifugo wakawa wanauza sana Ulaya. Mugabe akawanyanganya mashamba akawapa nduguze na wanasiasa wenzie wakawa wanalima mazao yaleyale waliyokuwa wanalima wazungu kila kitu wakizingatia kuanzia ubora lakini wakashangaa soko Ulaya halipo wazungu hawataki kununua hawaamini mswahili aweza zalisha budhaa ya kiwango cha Ulaya wakakataa kununua

Wawekezaji wakija wanauzia kwao wanakotoka kwa watu wao ,wewe mswahili huwezi penya soko lao kirahisi hata uzingatie vigezo vyote nobody is interested

Mama Samia yuko sahihi sana kwa hili
 
Embu tupe ushahidi wa Mwarabu kuwekeza Ngorongoro.

Tupe pia ushahidi wa Kikwete kusaini mikataba 300 na china
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…