Duru za Uchaguzi Afrika Kusini. Umokhonto We Sizwe

UNafikiri ni kwann ccm hawatoi hiyo katika mpya??
Moja ya sababu ni kwamba hakujawa na presha ya watanzania wenyewe kudai hiyo katiba mpya, laiti kama kweli watanzania wangeitaka katiba yao , hakuna namna cxm wangezuia mchakato, never. Wasingeweza. Ila sasa hii inatoa picha kuwa takwa la katiba moya wala sio concern ya wananchi (kwa wingi wao) bali ni kikundi cha watu ambao wanapopuuzwa bas wanakosa namna ya ku enforce.

Ndio maana hata mchakato wa katiba ya warioba ulipositishwa licha ya kugharim mamilion, bado hakuna hata mtanzania aliye amka kulianzisha, why?? It is not their thing at all!!.

Ndio maana vyama mbadala kama cdm vinapata wakat mgumu kwakua wanaotetewa wala hawana mpango na utetezi.

Mpaka siku watanzania waamke na akili ziwakae sawa ndio haya mambo yataonekana yana maana na hata chaguzi zitakua na maana ila kwasasa ccm wanajua wananchi % kubwa wala hawapindui kuhusu chama chao.

NATAMAN SANA UWE UMENIELEWA
Ni kweli kabisa ulichoeleza.

"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."

By Martin Luther King Jr.

BTW; Uzoefu duniani kote unaonyesha kwamba Katiba nzuri itokanayo na mawazo au fikra za Wananchi walio wengi zaidi kwenye nchi husika haijawahi kupatikana hivi hivi tu kiurahisi bila ya Watu kupigana makonde.
 
Alikuwa vizur ila alijikanyaga majuzi hapa kuhusu sera ya chama hiko
Yes, na ana lugha kali, kama Tundu lissu, hamungunyi maneno, kwenye suala linalopigiwa kelele sana na wa south ukiacha umeme,maji na ajira basi sera za uhamiaji zimechukua nafasi kubwa kwenye anguko la Anc,sasa Malema naye sera yake ya uhamiaji haipendwi ma wananchi wengi,maana yeye haoni kuwa wahamiaji ni tatizo,wakati wananchi wa kawaida wanasema kuwa wahamiaji (hasa haramu) ndiyo chanzo cha matatizo mengine kama uhalifu wa mitaani,uchimbaji haramu wa madini(ZAMAZAMA) Ukosefu wa ajira, kusambaa kwa biashara ya madawa ya kulevya, pia jamii ya wa pakistan na wasomali wanatuhumiwa kuuzia raia vyakula vibovu au vyenye sumu kwenye Spaza shops zao,kuhusu ajira raia wanasema kuwa waajiri wanapenda zaidi kuwaajiri wageni(hata wakiwa ni wahamiaji haramu) sababu wanawalipa ujira mdogo, na wanapiga kazi sana, sasa Malema huwa anawachana raia wao waache uvivu kama wanataka kuajirika, juzi hapo aliwaambia wasouth waache ujinga wa kugombania vi biashara kama vya spaza na sweets,hizo wawaachie wahamiaji,wao wapambane kufanya kazi decent zinazofanana na hadhi yao,wakamnunia.
 
Ni kweli kabisa ulichoeleza.

"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."

By Martin Luther King Jr.

BTW; Uzoefu duniani kote unaonyesha kwamba Katiba nzuri itokanayo na mawazo au fikra za Wananchi walio wengi zaidi kwenye nchi husika haijawahi kupatikana hivi hivi tu kiurahisi bila ya Watu kupigana makonde.
Ni kweli kabisa haki lazima ipiganiwe, pale ambapo inapo nyimwa. Kukaa na kusubiria uletewe sio rahisi.
 
Labda CCM imeguke mtu/watu wenye ushawishi watoke CCM waje kugombea upinzani.Usitegemee chochote kwa hawa akina lissu, mbowe,zitto nk hawana jipya ni wafurahisha genge tu ni ukweli mchungu lakini hakuna namna
Punguza unafiki. Nani anaushawishi CCM?. Halafu upinzani sio Lissu au Mbowe, upinzani ni progressive Ideas nje ya CCM . Shida yako unaangalia personalities na kudhani ndio upinzani.
 
Yes, na ana lugha kali, kama Tundu lissu, hamungunyi maneno, kwenye suala linalopigiwa kelele sana na wa south ukiacha umeme,maji na ajira basi sera za uhamiaji zimechukua nafasi kubwa kwenye anguko la Anc,sasa Malema naye sera yake ya uhamiaji haipendwi ma wananchi wengi,maana yeye haoni kuwa wahamiaji ni tatizo,wakati wananchi wa kawaida wanasema kuwa wahamiaji (hasa haramu) ndiyo chanzo cha matatizo mengine kama uhalifu wa mitaani,uchimbaji haramu wa madini(ZAMAZAMA) Ukosefu wa ajira, kusambaa kwa biashara ya madawa ya kulevya, pia jamii ya wa pakistan na wasomali wanatuhumiwa kuuzia raia vyakula vibovu au vyenye sumu kwenye Spaza shops zao,kuhusu ajira raia wanasema kuwa waajiri wanapenda zaidi kuwaajiri wageni(hata wakiwa ni wahamiaji haramu) sababu wanawalipa ujira mdogo, na wanapiga kazi sana, sasa Malema huwa anawachana raia wao waache uvivu kama wanataka kuajirika, juzi hapo aliwaambia wasouth waache ujinga wa kugombania vi biashara kama vya spaza na sweets,hizo wawaachie wahamiaji,wao wapambane kufanya kazi decent zinazofanana na hadhi yao,wakamnunia.
Sawa sawa . Wewe unaonaje Malema yupo sawa kwenye suala la uhamiaji au anakosea?
 
Believe me licha ya fair play, ccm itatikisa tu, upinzani bado hujawa serious kuonyesha unataka nini..wapo wapo tu
Haya maneno ya Wana CCM tulishayazoea. Kama upinzani si lolote CCM wasingehangaika kuharibu uchaguzi wa 2020 au kutuma majeshi Zanzibar 2015 kuzuia Maalim asitangazwe Rais. Acheni kuongea kinafiki kana kwamba hatuoni yanayoendelea.
 
Ur judgments are so clouded by cdm-hood.
Wenzako tulishatoka kwenye mindset hizo na kuamua kuyatazama mambo kwa mapana yake. Mimi sio mwana ccm kiongozi tuelewane
 
CCM kamwe haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania ili iendelee kubaki madarakani. Hat wakipata Kura sifuri kwenye Uchaguzi, bado wagombea wao watatangazwa kuwa ni washindi katikà Uchaguzi.

Rejea Uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 na kile alichofanya Mkuu we tume ya Uchaguzi wa huko, Bw. Jecha baada ya Maalim Seif wa CUF kupata Kura nyingi sana kumzidi Dk.Shein wa CCM.

1 Rais Ali Hassan Mwingi wakati akiwa bado yuko hai, aliwahi kusema kwamba "wakati tulipokubali mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania, CCM tulihakikisha kwamba HATUSHINDWI."

NB: Fanya tafakuri ya kina ya neno 'hatushindwi.'

2. "CCM lazima itashinda tu katika Uchaguzi wa mwaka huu hata kama ni kwa kimbunga."

Rais Benjamin W. Mkapa, mwaka 2005.

3. "Nimewatuma marafiki zangu ili waende wakahamasishe Upinzani, kwa hiyo wana-CCM wenzangu msiwe na wasiwasi kwamba tutashindwa kwenye Uchaguzi huu wa mwaka huu."

Mwl. J.K. Nyerere, akiwa kwenye Kampeni za Uchaguzi mjini Morogoro, 1995.

4. "CCM Ina maarifa mengi, kwa hiyo kushinda lazima tutashinda tu ndugu zangu, msiwe na hofu sisi viongozi wenu tupo."

Rais Jakaya M. Kikwete.

5."Serikali haiwezi kuondoka madarakani kutokana na vile vikaratasi tu, Jeshi ni letu kwa hiyo Uchaguzi tutashinda."

John Malecela.

6."Hata kama mtapigia Kura kule upande mwingine, Ila tambueni tu kwamba CCM ndiyo inayoenda kuunda Serikali."

Rais Samia Suluhu Hassan.
Asante kutukumbusha.
 
Sawa sawa . Wewe unaonaje Malema yupo sawa kwenye suala uhamiaji au anakosea?
Kwa hapa nchi ilipofikia nasema kabisa boldly kuwa hayupo sahihi, case ya illegal immigrant SA ni next level,
Kuna mitaa ina wahamiaji wengi kuliko wenyeji, na wako well organized, utakuta wahamiaji wanafanya biashara haramu au uhalifu ule wa gangstarism, raia wanaona kabisa, the best they can do ni kuwaita SAPS, saps wakija wana compromise na wahalifu then msala unaachiwa wewe raia mwema, sasa wanataka kiongozi yeyote atakayewaahidi kuwa ata fanya border closure, angalau Gayton Mackenzie anaeleweka msimamo wake kuhusu hilo, hivyo kwa Malema kusema kuwa yeye haoni kama immigrants ni tatizo ni kama kuwatukana wananchi.
 
Wakuu habari,

Chama cha Umokhonto We Sizwe (MK) chini ya kiongozi wake na aliye kuwa raisi wa zamani Jacob Zuma wamejizolea asilimia 13 ya wabunge wote mpaka sasa wamesha hesabu 80% ya wilaya zote, na MK imeshika nafasi ya 3. Hata hivyo ina tegemewa kuongezeka kufika mpaka asilimia 17 zoezi la kuhesabu litakapo kamilika.

ANC ndio ina ongoza kwa 41% lakini ikiwa Imepoteza idadi kubwa ya wabunge, ikifuatiwa na Democratic Alliance 22% huku EFF chini ya mwanasiasa machachari Julius Malema ikipata 9% na kushika nafasi ya 4. Hivyo kwa sasa Cyril Ramaphosa tumbo lipo joto kwa sababu itambidi azungumze na chama kingine baadae ili aongeze idadi ya wabunge.

Kilicho ni furahisha mimi ni muda mfupi wa hiki chama cha MK lakini kimeweza kuitikisa ANC. Jimbo la Kwa Zulu Natal ndio ngome kuu ya chama hiki na pia ndio asili ya Jacob Zuma.

Mimi naona wazi kuwa raisi Cyril Ramaphosa na chama chake cha ANC lazima watamtafuta Jacob Zuma kiongozi huyu mashuhuri mpigania uhuru wa Afrika kusini wamuombe kujiunga nae kufanya alliance ili waweze kupata wabunge wengi wa kufanya yeye na serikali yake kuwa na ushawishi.

Pia nime furahishwa kwa raisi mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwa muangalizi wa uchaguzi. Nadhani Afrika ya Mashariki tume wakilishwa vema.

Nawasilisha.
Sijui nini kinatufanya tuiache CCM iendelee kututesa miaka 63 baada ya uhuru?!
 
Kwa hapa nchi ilipofikia nasema kabisa boldly kuwa hayupo sahihi, case ya illegal immigrant SA ni next level,
Kuna mitaa ina wahamiaji wengi kuliko wenyeji, na wako well organized, utakuta wahamiaji wanafanya biashara haramu au uhalifu ule wa gangstarism, raia wanaona kabisa, the best they can do ni kuwaita SAPS, saps wakija wana compromise na wahalifu then msala unaachiwa wewe raia mwema, sasa wanataka kiongozi yeyote atakayewaahidi kuwa ata fanya border closure, angalau Gayton Mackenzie anaeleweka msimamo wake kuhusu hilo, hivyo kwa Malema kusema kuwa yeye haoni kama immigrants ni tatizo ni kama kuwatukana wananchi.
Ni kweli inatakiwa wapunguzwe wahamiaaji, weende kwa kufuata utaratibu wa vibali
 
AnC wameharibu sana Ile nchi yani SA ni inaporomoka imagine SA ni ya kukosa umeme na maji safi !?
Nimeishi SA umeme kukatika kwanza haikuwepo ,hapakuwa na kutibu maji kabla ya kunywa ni unakinga unakunywa ,bidhaa bei rafiki kabisa Randi 10 unakula kabisa bila shida Sasa unahitaji Randi 50 ndio ule sio poa
Kuna hujuma zilizofanywa kuna kifaa kiliibwa mahali ndiyo kuleta shida ya umeme

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu habari,

Chama cha Umokhonto We Sizwe (MK) chini ya kiongozi wake na aliye kuwa raisi wa zamani Jacob Zuma wamejizolea asilimia 13 ya wabunge wote mpaka sasa wamesha hesabu 80% ya wilaya zote, na MK imeshika nafasi ya 3. Hata hivyo ina tegemewa kuongezeka kufika mpaka asilimia 17 zoezi la kuhesabu litakapo kamilika.

ANC ndio ina ongoza kwa 41% lakini ikiwa Imepoteza idadi kubwa ya wabunge, ikifuatiwa na Democratic Alliance 22% huku EFF chini ya mwanasiasa machachari Julius Malema ikipata 9% na kushika nafasi ya 4. Hivyo kwa sasa Cyril Ramaphosa tumbo lipo joto kwa sababu itambidi azungumze na chama kingine baadae ili aongeze idadi ya wabunge.

Kilicho ni furahisha mimi ni muda mfupi wa hiki chama cha MK lakini kimeweza kuitikisa ANC. Jimbo la Kwa Zulu Natal ndio ngome kuu ya chama hiki na pia ndio asili ya Jacob Zuma.

Mimi naona wazi kuwa raisi Cyril Ramaphosa na chama chake cha ANC lazima watamtafuta Jacob Zuma kiongozi huyu mashuhuri mpigania uhuru wa Afrika kusini wamuombe kujiunga nae kufanya alliance ili waweze kupata wabunge wengi wa kufanya yeye na serikali yake kuwa na ushawishi.

Pia nime furahishwa kwa raisi mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwa muangalizi wa uchaguzi. Nadhani Afrika ya Mashariki tume wakilishwa vema.

Nawasilisha.
CHADEMA.
 
Kwa mujibu wa msemaji wa chama cha MK cha Jacob Zuma kadai kwamba ili chama chochote kiweze kuungana nao lazima wakubali kumfutia mashitaka Zuma na zuma asimame kama Rais ili agombee je Ramaphosa atakubali ilo litokee.
Kwan Kwa matokeo haya wataenda Kwa second run off?
 
Back
Top Bottom