Duru za Uchaguzi Afrika Kusini. Umokhonto We Sizwe

Ni kweli kabisa ulichoeleza.

"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."

By Martin Luther King Jr.

BTW; Uzoefu duniani kote unaonyesha kwamba Katiba nzuri itokanayo na mawazo au fikra za Wananchi walio wengi zaidi kwenye nchi husika haijawahi kupatikana hivi hivi tu kiurahisi bila ya Watu kupigana makonde.
 
Alikuwa vizur ila alijikanyaga majuzi hapa kuhusu sera ya chama hiko
Yes, na ana lugha kali, kama Tundu lissu, hamungunyi maneno, kwenye suala linalopigiwa kelele sana na wa south ukiacha umeme,maji na ajira basi sera za uhamiaji zimechukua nafasi kubwa kwenye anguko la Anc,sasa Malema naye sera yake ya uhamiaji haipendwi ma wananchi wengi,maana yeye haoni kuwa wahamiaji ni tatizo,wakati wananchi wa kawaida wanasema kuwa wahamiaji (hasa haramu) ndiyo chanzo cha matatizo mengine kama uhalifu wa mitaani,uchimbaji haramu wa madini(ZAMAZAMA) Ukosefu wa ajira, kusambaa kwa biashara ya madawa ya kulevya, pia jamii ya wa pakistan na wasomali wanatuhumiwa kuuzia raia vyakula vibovu au vyenye sumu kwenye Spaza shops zao,kuhusu ajira raia wanasema kuwa waajiri wanapenda zaidi kuwaajiri wageni(hata wakiwa ni wahamiaji haramu) sababu wanawalipa ujira mdogo, na wanapiga kazi sana, sasa Malema huwa anawachana raia wao waache uvivu kama wanataka kuajirika, juzi hapo aliwaambia wasouth waache ujinga wa kugombania vi biashara kama vya spaza na sweets,hizo wawaachie wahamiaji,wao wapambane kufanya kazi decent zinazofanana na hadhi yao,wakamnunia.
 
Ni kweli kabisa haki lazima ipiganiwe, pale ambapo inapo nyimwa. Kukaa na kusubiria uletewe sio rahisi.
 
Labda CCM imeguke mtu/watu wenye ushawishi watoke CCM waje kugombea upinzani.Usitegemee chochote kwa hawa akina lissu, mbowe,zitto nk hawana jipya ni wafurahisha genge tu ni ukweli mchungu lakini hakuna namna
Punguza unafiki. Nani anaushawishi CCM?. Halafu upinzani sio Lissu au Mbowe, upinzani ni progressive Ideas nje ya CCM . Shida yako unaangalia personalities na kudhani ndio upinzani.
 
Sawa sawa . Wewe unaonaje Malema yupo sawa kwenye suala la uhamiaji au anakosea?
 
Believe me licha ya fair play, ccm itatikisa tu, upinzani bado hujawa serious kuonyesha unataka nini..wapo wapo tu
Haya maneno ya Wana CCM tulishayazoea. Kama upinzani si lolote CCM wasingehangaika kuharibu uchaguzi wa 2020 au kutuma majeshi Zanzibar 2015 kuzuia Maalim asitangazwe Rais. Acheni kuongea kinafiki kana kwamba hatuoni yanayoendelea.
 
Haya maneno ya Wana CCM tulishayazoea. Kama upinzani si lolote CCM wasingehangaika kuharibu uchaguzi wa 2020 au kutuma majeshi Zanzibar 2015 kuzuia Maalim asitangazwe Rais. Acheni kuongea kinafiki kana kwamba hatuoni yanayoendelea.
Ur judgments are so clouded by cdm-hood.
Wenzako tulishatoka kwenye mindset hizo na kuamua kuyatazama mambo kwa mapana yake. Mimi sio mwana ccm kiongozi tuelewane
 
Asante kutukumbusha.
 
Sawa sawa . Wewe unaonaje Malema yupo sawa kwenye suala uhamiaji au anakosea?
Kwa hapa nchi ilipofikia nasema kabisa boldly kuwa hayupo sahihi, case ya illegal immigrant SA ni next level,
Kuna mitaa ina wahamiaji wengi kuliko wenyeji, na wako well organized, utakuta wahamiaji wanafanya biashara haramu au uhalifu ule wa gangstarism, raia wanaona kabisa, the best they can do ni kuwaita SAPS, saps wakija wana compromise na wahalifu then msala unaachiwa wewe raia mwema, sasa wanataka kiongozi yeyote atakayewaahidi kuwa ata fanya border closure, angalau Gayton Mackenzie anaeleweka msimamo wake kuhusu hilo, hivyo kwa Malema kusema kuwa yeye haoni kama immigrants ni tatizo ni kama kuwatukana wananchi.
 
Sijui nini kinatufanya tuiache CCM iendelee kututesa miaka 63 baada ya uhuru?!
 
Ni kweli inatakiwa wapunguzwe wahamiaaji, weende kwa kufuata utaratibu wa vibali
 
Kuna hujuma zilizofanywa kuna kifaa kiliibwa mahali ndiyo kuleta shida ya umeme

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
CHADEMA.
 
Kwa mujibu wa msemaji wa chama cha MK cha Jacob Zuma kadai kwamba ili chama chochote kiweze kuungana nao lazima wakubali kumfutia mashitaka Zuma na zuma asimame kama Rais ili agombee je Ramaphosa atakubali ilo litokee.
Kwan Kwa matokeo haya wataenda Kwa second run off?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…