PostGE2025 Elezea kinagaubaga jinsi mabeberu wanavyohujumu nchi yetu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mbona hii ni ya kawaida baadae wakasalitiwa
 

Attachments

  • Screenshot_20251220-071210_1766204935841.jpg
    134.1 KB · Views: 10
Kawaida hivyo ni visingizio ambavyo huletwa na serikali baada ya kushindwa kuwajibika katika majukumu yake.

Serikali yoyote iliyochaguliwa kihalali na wananchi lazima iwajibike kwa wananchi wake lakini hii serikali inakosa hiyo sifa kwa sababu haina ridhaa ya wananchi.
 
Ccm ndo siasa walizobakiza.
Kwamba beberu wanataka rasilimali.

Hizi propaganda za kuwadanganya watanzania kwasababu wanajua wengi wao ni mambumbu, na ndio maana ni vigumu sana kuikomboa nchi hii.
Mabeberu wana access ya rasilimali za Africa hilo sio swala la kujadili na CCM wamekuwa madalali wakubwa kwa miaka yote hii
 

Mimi ninachojua Kuna mbuzi anaitwa beberu kwa sababu ya ndevu zake tunaita mbuzi beberu kwa maana ya mbuzi mwenye jinsi ya kiume mwenye ndefu
 
Mkuu uko sahihi sana.
Elimu inayojitolewa na c c m ni ya kipumbavu.
Wametengeneza kizazi cha wapumbavu.
Watumishi wa umma wote ni machawa.
 
Nadhani ukirudia kusoma hichi ulicho andika unaweza kujicheka mwenyewe😃

Hoja hapa kivipi hao mabeberu wanapelekea nchi yetu ushindwe kuendelea?

Miaka 60 bila maji safi na salama Huku tukiwa na rasilimali za kutosha nini shida?
 
HAYA LAND HOV & Ertugrul Bey
Menununuliwa sh ngapi?

Maana sio kwa mapambio hayo .
Hatuna bei bwana Juuchini,

Ni kupambania vijana wetu,watoto wetu,ndugu zetu na kila mtanzania

Amani ya nchi hii ni tunu ambayo mataifa mengi hayana,mpaka tukaitwa kisiwa cha amani

Sasa ni nani wa kuipigania amani yetu kama sio sisi???

Nani wa kuhamasisha wengine wajue ubaya wa kuipoteza amani hii?

Amani ni tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana
 

1. Kwenye hadaa apa utakutana na vyombo like Tissue, Cia M16 nawengineo... Utapeli, wizi na ujambazi, ukiachana na huu wa mtaani, unaweza ukafika hadi ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Ukishafika national na international level unalasimishwa na kua carrier katika organization.
Hapa ndio utakutana na vitengo vya kijasusi, division za polisi na jeshi.

#Ujasusi→wizi/utapeli.

#Police na jeshi→wezi na majambazi.

Kama unafanya vetting sifa za kumpata jasusi wa aina flani au mwanajeshi au polisi ndio hizo hizo walizonazo wezi/matapeli na majambazi tofauti yao ni mmoja amerasimishwa na kuongezewa mafunzo, wakati hawa mwingine ni wanapiga harakati zao kiholela.

Sasa kama tapeli tu!(q-net, Bit coin na wengineo) huwezi ukamkamata kirahisi au ukamshtukia kirahisi mpaka anakamilisha mission yake ndio mnashtuka kua mmepigwa... Itakuwaje kwa hawa waliorasimishwa, wakapewa mafunzo ambayo huku uraiani hatuna, wana-back up ya black budget utawapatia wapi wanawapiga tukio kama Nchi na mnajua kabisa Fulani ndio kahusika ila shida inakuja huna ushahidi wakutosha kumshitaki... Hivyo na wewe kama Nchi inatakiwa uwe na vitengo kama hivyo ili kuweza kujibu mapigo... Jino kwa jino/dawa ya moto ni moto.

Na Tanzania katika hizo kazi hasa za kupangua na kujibu mapigo inaonekana wapo vizuri,

Ndio maana kuna vitetesi vilivumaga kuwa jeshi ni no 6 duniani.

Ndio maana kuna fursa nyingi mtandaoni ila serikali ahihalalishi sio kwamba hawajui au hawana uhakika la hasha wanajua nini kinaendelea wanachokifanya hawakuzuii bali wanawataadharisha wewe Wananchi, ili kama unafanya ufanye kwa your own risk (mtoto akililia wembe).

Mfano mzuri ni hizi digital currency hizi ni scam na scammer ana-act kama panya anang'ata huku anapuliza, kaamua kuishi nao na inaweza kua life time scam. Lakini pia huwezi kujua lini atalala mbele.

Kati ya serikali ambazo hua hazibaatishi mambo tz ni miongoni ila sina guarantee ya huko mbeleni ni kama tunaanza kupotezana.

Lakini kama unajambo lako na unawasiwasi nalo basi wewe nenda kwa serikali kaangalie serikali yenyewe inamsimamo upi juu ya hilo jambo kisha fuata, yaani we usiwe na shaka fuata tu huo msimamo wa serikali...

Na kama hautafuata basi tambua kua maamuzi unayoyachuku yana risk na uko tayari kwa madhara yatakayo jitokeza... Unaweza ukafanikiwa/au usipate madhara lakini serikali ilishaweka bayana.

2. Katika ulimwenguni wa kijasusi/kijambazi mapandikizi hayakosi nchi yoyote ile...haya mapandikizi yanakuwaga na uwezo mkubwa (kuanzia ushawishi, pesa(biashara) hivyo anakua anaamua hatma au dira ya nchi muda mwingine hata nguvu itatumika kama ikibidi kwanini kwasababu anaback up ya uhakika kutoka katika taifa analolitumikia zaidi anahakikishiwa kila kitu atakachokihitaji kwa mission hiyo.

Sasa juilize kwanini watu wanajua kifo cha mtu kabla, na kwanini watu wazuri wakutegemewa ndio wafe. Mipango mizuri ipo ila akipatikana mtekelezaji wa kweli kelele zinakua nyingi, vikwazo kibao, anaweza akaondolewa kwenye nafasi au akapotezwa kabisa...

Tulikua na tanzania ya viwanda ila sizani kama ile spirit bado ipo (tayari tumeshakua distracted katika focus ya msingi na ya muhimu mno... Viwanda nchini vingechagiza maendeleo marighafi(mazao/Kilimo) zingetengenezwa hapa hapa ajira zingezalishwa...)

Yaani kwa asilimia kubwa mnyororo mzima wa thamani ungekuwa unazunguka hapa. Ila sasa tunachokifanya ni kuvuna pesa nchini kisha tunaenda kuagiza mzigo uturuki china india hii inamaana tunasapoti mnyororo mzima wa thamani wa nchi hizo na wakulima wao vijana wao wananufaika na ajira kwa sababu industry yao ina-run... sasa kwanini sisi.

3. Mkuu linapokuja suala la ujasusi tambua kua Nchi zinauwezo mkubwa wana-capability sio za viwango vya kibinadam wanaweza wakafanya tukio sisi watoto wa mungu tukakimbilia katika nyumba za ibada kutubu huku tukitafuta ni wapi tumemkosea mungu.

a). Sasa leo chukua hii si kila majanga ya asili ni ya asili kweli, na hakuna ushetani wala secret society ni ubobevu mahsusi katika Elimu/fani/ujuzi. Kuna wahuni wanacheza na hali ya hewa, tectonic plates, kama mtoto anavyochezea matope.

Sasa rudi nyuma mwaka 2021---2024 Kapitie matamko ya TMA, Na nabii za manabii mbalimbali vile vitu vilivyokua vinaongelewa sio utani tungeteketea. Sasa jiulize kwanini havikutokea(fikiria mtu mhimu katekwa waliomteka wanasema wakipata milioni mia wanamuachialia huru, la sivyo watamuua...!baada ya muda unasikia yule mtu alietekwa ameachiliwa huru! We utaelewa nini hapo.

Kisha ndani ya kipindi hicho hicho kaangalie Jeshi la zimamoto, shilika la ndege kulikua kunatokea nini na ujiulize kwanini ni kipindi kile ndio walifanya vile baada ya kutokea yale na sio Sasa.

b). Vitishio vya ugaidi vipo sema mapambano yanakaa kimkakati zaidi kumbuka hii nchi ni ya kitalii kwa angle fulani hivyo huwezi kusema tumepambana na magaidi tukayashinda utaharibu brand ya Nchi katika secta ya utalii uwekezaji nk. Mfano: kusini mpakani kwenye gasi.

c). Majirani wanavyojiimarisha kiulinzi, juzi hapa Uganda kapokea vifaa vya kijeshi toka Urusi punde kidogo Kenya kapokea mfumo wa ulinzi... Sasa hapa katika medani za kijasusi tayari hari ni mbaya vita vikianza utaona kama ni gafra kumbe watu walikua wanaliana timing toka kitambo... Sasa hapo sisi tunahisikaje hiyo ni kijasusi zaidi/kimkakati na kwa kiasi kikubwa hii issue ni ya kikanda sio nchi moja moja.

NB. Hizi ni fikra binafsi zinaweza zisiwe na uhalisia hivyo zinawezwa kupuuzwa
 
Kama mnataka amani mwambieni samuya atende haki.
Heshimu maoni ya watu.
Asiwateke na kuuwa watu.
 
Nilichogundua watu wengi wamekata tamaa na mapambano kwa maana hawaoni mwanga mbele yao wanaona hamna namna tena zaidi ya kuunga juhudi kinafiki ilimradi maisha yasonge kilichotokea kimewakatisha wengi tamaa poleni sana na hiyo sio kwa Tanzania tu dunia nzima hali iko hivyo

Tulindeni amani ya nchi, amani ni tunu ya Taifa
 
[QUOTE="Kazanazo, post: 55442308, member: 724197"
Tulindeni amani ya nchi, amani ni tunu ya Taifa
[/QUOTE]Amani inalindwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…