Elon Musk atangaza kampuni yake ya Neuralink kuleta kifaa tiba cha kuwawezesha vipofu kuona!

Habari njema hii kama kawaida tech ikifanikiwa tatizo jipya litaibuka.

Miaka 30 ijayo usishangae Africa tukapewa misaada ya kuona kwa vipofu walioongezeka sana kwa masharti fulani fulani.
Akili ya mwafrika halisi hii
 
Reactions: Tsh
Hi habari nzuri sana kwa wote sio kwa vipofu tu hata wenye matatizo ya kuona vizuri.
 
Si ndio maana tunafanya gunduzi Kila leo hili kukabiliana na hicho unachokihofia.

Leo hii tunavyoandika hapa wamarekani kupitia taasisi yao ya Planetary lab kwa msaada wa Robotic spacecraft wamebaini kuwa, mbali na Mars pia Kuna sayari zingine zaidi ya mbili ambazo zinaweza zikamu accommodate binadamu endapo kama zitakuwa oxygenated... Hii tafsiri yake ni kwamba maisha nje ya hii dunia yanawezekana.

Hivyo mpaka tunafikia kwenye hiyo miaka ambayo binadamu wote jumla yetu itakuwa ni hiyo idadi uliyoitaja ni wazi kwamba Kuna wengine tayari watakuwa wameshaanza kuishi kwenye hizo sayari zingine na hivyo suala la depopulation kutokuwa na ulazima wowote.

Hii hoja yako inanikumbusha Kuna mama mmoja humu siku za nyuma aliwahi kuandika watu wanazidi kuzaliana na kurundikana tu dar na wakati nafasi hata nafasi ya kujenga chumba kimoja hamna, alikuwa anaandika hivyo mantiki yake ilikuwa Wana dar salaam hawatakiwi kuzaliana Wala kuongezeka kwa namna yoyote ile....
 
Kwa hiyo hiki kichwa Nappe ndo alitaka kije mezani wajadiliane? Kuna watu wana mizaha sana.
Nape yule kilaza form four failure mbwa mmoja zero brain Ndio alitaka akae meza moja na visionary mkubwa wa teknolojia wa karne hii Elon Musk ,sijui hata angeongea naye nini ,maana hata kiingereza hajui .
 
Ee Mungu tuonee huruma na sisi wa Africa ili IQ zetu zipanuke tupate kufanya yanayofanywa na wenzetu.
Iq inashushwa pia na mifumo ya kishenzi na tamaduni za kipumbavu zinazoongoza nchi zetu na jamii zetu
Tukiacha uchawa ,rushwa , UMungu mtu ,ubinafsi ,chuki ,wivu ,Majungu na kutengeneza mifumo bora ya watu kufanikiwa bila vikwazo kwa haki na uwazi na kujali haki za binadamu bila kulamba watawala makalio na kuwafukuza kama miungu watu .
Hiyo miaka tutapiga hatua na kuanza kufanya vitu ambavyo tulidhani ni ndoto
 
Duh! Walimfanyia nini mkuu?
Walimbania kufanya uwekezaji wake humu na kulaunch ile Nala hapa ,wakamyima vibali na legal approval akaenda Kenya ,Leo hii ni multimillionaire na kampuni yake imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa pale Marekani na alifanikiwa kuraise bilioni 200 kama mitaji ya wawekezaji kwenye masoko ya hisa pale Marekani mwaka huu.
Imagine ni mapato kiasi na ajira kiasi gani kama nchi imekosa kwa upumbavu ,ubinafsi na uzezeta wa hawa policy makers na Mazezeta wenzao kwenye hizi taasisi mfu za serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…