Elon Musk atangaza kampuni yake ya Neuralink kuleta kifaa tiba cha kuwawezesha vipofu kuona!

Elon Musk atangaza kampuni yake ya Neuralink kuleta kifaa tiba cha kuwawezesha vipofu kuona!

Habari njema hii kama kawaida tech ikifanikiwa tatizo jipya litaibuka.

Miaka 30 ijayo usishangae Africa tukapewa misaada ya kuona kwa vipofu walioongezeka sana kwa masharti fulani fulani.
Akili ya mwafrika halisi hii
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Tajiri namba moja duniani Elon Musk ametangaza kampuni yake mojawapo ya Neuralink inayofanya kazi za kuhusianisha ubongo wa binadamu na teknolojia ya computer kuja na kifaa cha kuwawezesha vipofu kuona.

Anasema kwa kuanzia uoni kupitia kifaa hicho utakuwa hafifu lakini utazidi kuboreka na kuwa kama uoni wa binadamu mwenye macho mazima kabisa kadri muda utakavyoenda.

Pia amewashukuru mamlaka ya dawa na vifaa tiba ya Marekani (FDA) kwa kuwapa kibali cha kuanza majaribio ya kifaa hicho.

View attachment 3099144
View attachment 3099145
View attachment 3099147
Hi habari nzuri sana kwa wote sio kwa vipofu tu hata wenye matatizo ya kuona vizuri.
 
Hii movie nimeitazama. Binafsi nadhani kuna umuhimu kweli wa population control. Hatuwezi kuzaliana tu kama ng'ombe wakati tunategemea viumbe wengine kusurvive.

Sisi ni predetors wa mimea, wanyama, ndege, samaki n.k. sasa imagine tupo binadamu B50 duniani, what will happen?

Kama Leo tu tupo B6 kuna nchi ukienda hospitali watu wamelundikwa kama ng'ombe tukifika B50?. Maisha yatakosa thamani kabisa.
Si ndio maana tunafanya gunduzi Kila leo hili kukabiliana na hicho unachokihofia.

Leo hii tunavyoandika hapa wamarekani kupitia taasisi yao ya Planetary lab kwa msaada wa Robotic spacecraft wamebaini kuwa, mbali na Mars pia Kuna sayari zingine zaidi ya mbili ambazo zinaweza zikamu accommodate binadamu endapo kama zitakuwa oxygenated... Hii tafsiri yake ni kwamba maisha nje ya hii dunia yanawezekana.

Hivyo mpaka tunafikia kwenye hiyo miaka ambayo binadamu wote jumla yetu itakuwa ni hiyo idadi uliyoitaja ni wazi kwamba Kuna wengine tayari watakuwa wameshaanza kuishi kwenye hizo sayari zingine na hivyo suala la depopulation kutokuwa na ulazima wowote.

Hii hoja yako inanikumbusha Kuna mama mmoja humu siku za nyuma aliwahi kuandika watu wanazidi kuzaliana na kurundikana tu dar na wakati nafasi hata nafasi ya kujenga chumba kimoja hamna, alikuwa anaandika hivyo mantiki yake ilikuwa Wana dar salaam hawatakiwi kuzaliana Wala kuongezeka kwa namna yoyote ile....
 
Kwa hiyo hiki kichwa Nappe ndo alitaka kije mezani wajadiliane? Kuna watu wana mizaha sana.
Nape yule kilaza form four failure mbwa mmoja zero brain Ndio alitaka akae meza moja na visionary mkubwa wa teknolojia wa karne hii Elon Musk ,sijui hata angeongea naye nini ,maana hata kiingereza hajui .
 
Ee Mungu tuonee huruma na sisi wa Africa ili IQ zetu zipanuke tupate kufanya yanayofanywa na wenzetu.
Iq inashushwa pia na mifumo ya kishenzi na tamaduni za kipumbavu zinazoongoza nchi zetu na jamii zetu
Tukiacha uchawa ,rushwa , UMungu mtu ,ubinafsi ,chuki ,wivu ,Majungu na kutengeneza mifumo bora ya watu kufanikiwa bila vikwazo kwa haki na uwazi na kujali haki za binadamu bila kulamba watawala makalio na kuwafukuza kama miungu watu .
Hiyo miaka tutapiga hatua na kuanza kufanya vitu ambavyo tulidhani ni ndoto
 
Duh! Walimfanyia nini mkuu?
Walimbania kufanya uwekezaji wake humu na kulaunch ile Nala hapa ,wakamyima vibali na legal approval akaenda Kenya ,Leo hii ni multimillionaire na kampuni yake imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa pale Marekani na alifanikiwa kuraise bilioni 200 kama mitaji ya wawekezaji kwenye masoko ya hisa pale Marekani mwaka huu.
Imagine ni mapato kiasi na ajira kiasi gani kama nchi imekosa kwa upumbavu ,ubinafsi na uzezeta wa hawa policy makers na Mazezeta wenzao kwenye hizi taasisi mfu za serikali
 
Back
Top Bottom