English Medium ziko Ovarated sana. Hakuna elimu pale zaidi ya utapeli. Shida ni tumekuwa Brainwashed sana

Well said mkuu ndio maana watoto wangu niliwarudisha Kayumba. Wa kwanza ndio alinipuna Ems kuanzia chekechea hadi la saba
 
Utofautii ni mkubwaa mnooo, commitment kwenye public schools ni zeroo kabisaa ni huu umaskini wetu tu lkn hapafai, imagine darasa linawanafunzi 300 nini kinafanyika hapoo. Tusidanganyaneee public wanaambiwa waandike notes tu.
mbona tumesoma kwenye shule za kayumba na tukatoboa mpk University na kupata hadi Phd.?

Pesa ya kulipia mtoto ada milioni 4 ni bora uwe unamnunulia viwanja kila mwaka ili akikua akute baba yake kashamuandalia assets za kutosha.
 
lakini ni ukweli usiopingika kujua kiingereza kunampa fursa zaidi kuliko yule ambaye anajua kiswahili pekee.

Wenye biashara Kariakoo karibu robo Tatu hawajui Kingereza.
Alafu waliowaajiri wanajua.

Kuchangamkia Fursa ni akili ya mtu haihusiani na kujua Lugha Fulani

Mbona Tanzania tunajua Kiswahili kuliko Kenya lakini Wakenya wanatupiga bao Kupata Fursa kimataifa

Usijesema Watanzania hawajui Kingereza
 
Wewe wacha kulialia humu na umasikini wako

Huna ada na shule ndiyo zinaelekea kufunguliwa, hukujipanga

Hukujipanga, hujalazimishwa shule za bure zipo
 
Katika vitu ambavyo siwezi fanya kosa nikumpeleka mwanangu shule ambayo hahawezi kumfundisha english language akaelewa vizuri pindi akiwa mdogo kwa hiyo hizi st kayumba ni big no.

Kwa ulimwengu wa sasa especially hapa tz mtoto anatakiwa aelewe lugha ya kimataifa kwa ufasaha, hisabati, na computer.
Fursa nyingi hapa nchini zinawataka wanaujua lugha yaani lugha ndio kila kitu hata uwe kilaza namna gani ukijua tu kutema yai fursa za pesa zitakutafuta na st kayumba swala la mtoto kujua lugha halipo hata walimu wenyewe hawajui.
 
Mkuu ungana nami kwenye kampeni ya Back to Kayumba Schools

Andika Uzi tuwafungue watu wengi hawajitambui

Hamna Mkuu.
Waache wafanye wapendavyo.
Ila mtu kama Kazi yake ya jasho, kipato hakifiki Milioni Moja kwa mwezi alafu anapoteza pesa English Medium hizi za mtaani atakuwa hajafikiri sawasawa.

Bora waende zile English Medium zenye waalimu WA Kenya, lakini hawa wabongo wengi wao nakuambia hawana C za kingereza sasa watakuwa wanafundisha vitu gani.

Wengine C Zao ni zile zinachechemea
 
EMS hazifundisha kingereza bora ni ujinga unaendelea kule.

Bora English course za ras simba
 
Vingereza vyao vyenyewe vya ajabu ajabu the the nyingi hamna kitu

Zipo shule chache Sana wanajitahidi.

Moja ya dalili kuwa mAxi anapoteza pesa kusomesha English Medium ni kuangalia Mishahara ya hao waalimu WA English.

Hivi mtu Anayelipwa Laki mbili u tatu anajua nini kuhusu kingereza?

Wengine wanalipwa mpaka elfu 80 hata wafanyakazi WA ndani ambao ni darasa la Saba hawalipwi hiyo.

Kama Mwalimu anayemtundisha mtoto wako mshahara wake unaanzia Walau Laki tano tunaweza kusema huyo Mwalimu anauwezekano wa kumfundisha mtoto wako kingereza.
 
Mtoto wako kusoma English Medium anajiweka karibu na Connections hata ma classmates wake Wanakuwa na asilimia kubwa kufika sehemu flan tofauti na kayumba Mnaanza 100 Watafukuzwa 20 Wataacha 10 zero 50 div 3 zipo 10 div 2 zipo 6 div 1 4 kuna nini hapo? Acha ubahili
 
Mwaka huu kwenye interview nimeingia kwenye panel nakutana na wafaransa watatu wote wanakupiga maswali ndani ya lisaa lizima nguvu na mateso mtu unayopitia hata kujiandaa na kujiumama ni makubwa sitaki fedhea kama hizo ziwakute wanangu.

Tunafanya kazi na waganda watanzania wengi wanajua mambo sana lakini tunadharaulika kisa kujua lugha ambayo imetokana na mifumo mibovu ya st kayumba
Niliwahi kutana na kajamaa goba kwenye bajaji anavitoto vyake vidogo vinatema yai yaani nibalaa
 
Mishahara ya wengi inasikitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…