Hii nadhani jamii nyingine pia wangeiga. Isiwe tu ni sisi wachaga ndo wakusafiri mwezi wa 12.
Iko hivi uchumi wa nchi au sehemu yoyote unakuwa driven sana sana na expenditure.
Watu wasipofanya spending, uchumi hauwezi kukua kamwe. Na nadhani hii ndio inafanya hata maeneo ya jamii nyingi za wachaga kuwa ni sehemu ambazo zina maendeleo fulani ya kiuchumi ukianzia level ya familia.
Kwanini?
Kwa kiasi kikubwa naweza sema hii tabia ya at least kurudi nyumbani haswa hiki kipindi cha sikukuu, ni moja wapo ya sababu kubwa ya ukuaji wa uchumi wa Kilimanjaro na maeneo mengi ya wachaga.
Kinachofanyika ni kwamba, tunavoenda Moshi, maana yake ni kwamba tunahamisha consumption kutoka huku tulipo na kuzipeleka mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa hiyo unakuta volume ya economic activities kwa mkoa wa Kilimanjaro zinakuwa maradufu kwa sababu kwenda kuhesabiwa inafanya kuwe na Capital inflows nyingi kwenye mkoa wa Kilimanjaro.
Maduka mengi, Bar, Hardware, Hotels, Masoko.. n.k huwa wanapata faida sana kipindi hiki.
Matokeo yake ni kwamba kasi ya kuzunguka kwa pesa inakuwa ni kubwa sana kipindi hiki, na unavokuwa na kasi kubwa ya mzunguko wa pesa maana yake ni kwamba, Investment na production ya goods and services nayo inakuwa ni kubwa sana.
Impact ya kuongezeka kwa investment na production ya goods and services ndo hiyo sasa unaweza kuiita wealth creation. Utakuta ukienda Kilimanjaro watu wamejitahidi sana kujenga nyumba nzuri kwenye vihamba vyao, nyumba imekuwa fahari kubwa sana kwetu. Ingelikuwa sio hii movement ya mwisho wa mwaka, uchumi wa Kilimanjaro usingekuwa huu unaoonekana kwa sasa.
Ningewashauri na makabila mengine kuiga huu utaratibu, itasaidia sana kuinua uchumi wa maeneo husika, msijazane tu Dar, mkawanufaisha wahindi.. Rudini makwenu mkawanufaishe na wakina mzee Pwagu Pangu Pakavu.