Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

Poleni bro kwa msiba huo mzito.
 
Kwamba akimuona dean of student atampa matokeo ya dogo!!
Mkuu,matokeo anapewa vizuri tu.tukiwa mwaka wa pili pale udsm,kuna jamaa alikua haonekani nyumbani kwao kila tukifunga chuo,jamaa story zilikua nyingi mara asingizie kuna kazi temporary kapata,so dada yake aliyekua anamsomesha akaingiwa na mashaka kama kweli jamaa anasoma chuo au kaacha,akafunga safari kutoka kigoma akaenda Dar kuhakikisha kama ndugu yake yupo chuo kweli,bahati siku hiyo anafika pale udbs mimi nikawa nashuka kwenye ngazi akawa ananiulizia huyo ndugu yake,jamaa alikua anasoma bcom banking alivyonionyesha picha yake nikawa nimemtambua lkn bahati mbaya sikuwa na majibu sahihi kama jamaa yupo chuo au hayupo sababu kwa mwaka wa pili tulikua hatushei masomo mengi na watu wa banking, so mimi nikampeleka hadi kwa secretary wa ofisi ya dean akamwelezea shida yake,baada ya kama nusu saa hivi yule secretary akaja na kitu inaitwa provision results ya jamaa akamwonyesha yule dada,ebana yule dada wa jamaa alipiga ukunga pale,kumbe mwamba alikua kaliwa kichwa toka mwaka wa kwanza.ikabidi tu dada wa watu amtafute jamaa akamchana ukweli.
 
Upo sahihi... Nilitofautiana na member aliyeshauri akaombe matokeo ya semister hii! Kwa sababu ndiyo dogo hajaonyesha...
Nimekuelewa POV yako.

matokeo sio ishu sana.
Je mtoto wao ni miongoni kwa graduates?.
Hilo ndio wanatakiwa kujua.

Alafu kwan wana utaratibu wa kumkagua mtoto wao matokeo?.

Mm miaka yote nilikuwa naulizwa. Vip matokeo. Yako fresh? Huna SUPP.. Nikijibu yako fresh sina Supp. Basi ndio imetoka.
Hakuna mtu anajua nimepata ngap.
Ila Thanks God nilipata 3.8 GPA. Overall.
UDOM.
 
Dv Two umefeli mpaka mkuu wa shule kamtafuta mzazi?
 
Mzee wako alikuwa mkaksi sio?

Jau sana hiyo, sema na wewe ulikuwa mwoga kinyama, yaani. Division 2 bado unadhani umefeli
 
Nahisi vyuo vinatofautiana taratibu. Kuna ndugu yangu mmoja niliagizwa kufuatilia matokeo yake kwa sababu wazazi walikuwa na mashaka nae...

Bila kumtaarifu dogo nilifika mpaka kwa dean of student akaniambia taarifa zote muhimu za maendeleo anaweza kunipatia(Alikuwa anakaa Hostel) isipokuwa matokeo ambayo ni mpaka muhusika athibitishe.
Basi ikabidi dogo apigiwe simu make hakuwa mazingira ya chuo, akataja particulars zake ndio nikapatiwa matokeo yake.
 
H
Aya mambo yanasikitisha sana kuna binamu yangu alidanganya hivyo , akaolewa na kibibi cha kizungu mwisho wa siku kibibi kilimdump baada ya kuendekeza pombe na mademu akapigwa chini akaludi tz mkia ameuficha anaulizwa cheti kiko wapi hana .
 
Hongera mkuu...
 
Labda kwa sababu wewe hukuwa ndugu yake ndio maana walikuzingua,lkn kwa yule dada wa jamaa haikua ngumu kabisa sababu alijitambulisha kuwa yeye ndio mlezi wa jamaa na ndio mlipa ada.
 
Huyo dogo anaroho ya Pala..

How do you even start?

Shida ni pale wazazi wanao shindwa kuwafanya watoto wao kuwa comfortable.

Wanaishia kuogopa wazazi, na baadae kupotea kimaisha
 
Janja ya ya nyani kula kunde mbichi, kuna mwana tulikuwa naye UK kwao safi ni super siyo diesel.

Basi mshuwa wake alimpa pesa za kulipia tuition fee ya chuo akaja kwa student Viza asome college.

Kipindi Uingereza walikuwa powa sana hawana noma, Admission letter Lincoln college wanatowa bure bila kulipa hata mia hata mtu ambaye yupo UK anakuombea anachukuwa kwa mkono anakutumia, ni chuo tulikutumia sana kwa michongo ya student viza.

Basi mwana kuja akafikia mtaani wala hakureport college na mishe zikamkubali sana mambo ya michanjo ya viwembe Cardif City na ada mshuwa anatuma, mambo yamekwenda game imechange yupo Bongo mshuwa yuko mbele za haki sasa ndio anakumbuka ujinga aliofanya Graduate wa UK huwezi kuteseka Bongo siyo rahisi, ukipenda maisha ya kuajiliwa hukosi kazi na hasa kwa sisi wa Mzizima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…