naiman64
JF-Expert Member
- Nov 22, 2013
- 6,961
- 5,460
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yani mna tabu haswa kuongozwa na watu amabao wana uelewa mdogo yani kiongozi anashindwa hata kujua tarehe mbowe aliyotangaza mikutano na tarehe ambayo serikali ilizuia mikusanyiko
Halafu mikutano ilikuwa inaanza tarehe 4 april na tangu mbowe qtangaze kutakuwa na mikutano hajawai kuendelea kutangaza mikutano
Je hatua gani zitachukuliwa dhidi yako uliyeweka mikusanyiko leo asubuhi?
tumia akili
Utawezaje kutumia usichokuwanacho?tumia akili
Atoe wapi kama na yeye ni sawa na lile wezere la Bashite tutumia akili
Binadamu weusi ata siku moja awawezi kua watuMjanja hajaingia kichwa kichwa kama halima mdee na bulaya! Nilifikiri angesema makonda mpumbavu tumuone.
Wanajitokeza kipindi cha corona ila kwenye maandamano hawaonekani.
Harafu hajakanusha kama hakuna mgonjwa nyumbani kwao!
Au ndio njia za kula rudhuku.
Umewaza mbali kama mimi aisee.Tushukuru hivi virusi vineanzia kule kwenye ustaarabu na wametuonyesha jinsi ya kukabiliana nao na kuwasaidia walioambukizwa.
Imagine ungeanzia kwetu, hasa kule walikozoea kuua albinos na vikongwe kwa tuhuma za uchawi si tungewafyekelea mbali wazee na wote wenye dalili za maambukizi kama siyo kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi?
Siku ya leo ndio nimegundua kuwa Mbowe ana busara sana.TAARIFA YA FAMILIA YA FREEMAN AIKAELI MBOWE KWA UMMA WA WATANZANIA NA DUNIA.
KORONA NI JANGA KUBWA KULIKO VIONGOZI NA WATANZANIA WENGI TUNAVYODHANI:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, leo asubuhi ametangazia dunia kuwa mmoja wa Wanafamilia wangu (mtoto) amebainika kuwa na virusi vya Corona na pamoja na mambo mengine anamshukuru Mungu kwa janga hili kutokea kwa familia yangu.
Bila kujali Maadili na upotoshaji ulioambatana na taarifa hizo, ni kweli mwanangu Dudley amethibitika kupatikana na virusi vya Corona baada ya kupata homa za vipindi, kuumwa kichwa mfululizo na kukohoa kwa siku tano.
Mama yake, ambaye ni Daktari alipobaini hali hiyo alizitaarifu mamlaka za Serikali zinazoshughulikia Janga hili nazo zilimtaka kijana apelekwe Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kwenye vipimo zaidi ambapo ilithibitika rasmi kuwa ana virusi vya Corona.
Aidha, timu ya Serikali imeendelea kutoa ushirikiano na ufuatiliaji wa karibu kwa familia yote ikiwemo ushauri nasaha kwa wanafamilia na marafiki wengine waliokutana na Dudley katika mikusanyiko mbalimbali ikiwemo kuweka wengine in Isolation au karantini.
Familia yangu inakiri kupokea ushirikiano wa kiwango kilichowezekana kutoka kwa Mamlaka husika za Serikali wakiongozwa na Waziri Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wake, Mganga Mkuu wa Serikali na Wataalam wao wote nikimaanisha Madaktari, Wauguzi nk.
Hali ya Dudley sasa imeimarika. Homa zimekwisha. Kichwa kimepona. Bado anakohoa kiasi na yuko chini ya uangalizi maalum kwenye “isolation”.
Dudley hajasafiri nje ya nchi mwaka huu. Maambukizi haya kayapata ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Ugonjwa huu haupaswi kuwa siri japo kuna miiko inayoongoza utaji wa taarifa za wagonjwa. Tatizo ni kubwa kuliko tulivyojiandaa na tunavyojiandaa.
Wengi wameitafuta familia kutaka kujua ukweli na undani wa jambo hili. Pengine kupitia ushuhuda wangu, tutaweza kuokoa wengi katika nchi yetu. Hakika leo kila mmoja anastahili kujua janga hili
liko mlangoni mwake!
Nimekiri kupata ushirikiano “kwa kiwango kilichowezekana”. Sina uhakika ni wangapi watapata “bahati” hiyo. Nimejifunza mengi. Nazungumza kwa mamlaka ya kuwa mhanga na shuhuda wa hali halisi tuliyo nayo. Tuna mlima mrefu wa kupanda. Hakika Serikali inahitaji msaada. Mlipuko hauko mbali. Tuelezane ukweli tusijechelewa.
Njia mojawapo muhimu ya kulishinda tatizo ni kulikubali na kulikabili kwa nguvu zote na kwa Umoja wetu.
Hatustahili kuchefuliwa na kejeli za Paul Makonda kipindi hiki. Tusiiachie serikali pekee. Tutajuta. Tusiilaumu tu, tuishauri nayo iwe tayari kuupokea ushauri na ishirikishe. Ni janga la Dunia na hakika tutaumizwa kuliko tunavyowaza.
Rai kwa Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Magufuli: Unda timu ya kukusaidia na ushirikishe wadau wengine nje ya Serikali yako. Yako mengi ya kufanya nje ya mikakati ya kitabibu inayosimamiwa na Waziri Mkuu na Waziri Ummy Mwalimu.
Katika maisha maandalizi hayajawahi kuwa hasara, bali hasara iliyo
majuto ni kutokujiandaa na kupuuza yanayofanywa na walioyapitia kama
Ilivyo nchi za wenzetu zilizoendelea na hata nahitaji zetu!
Wengi wako tayari kukusaidia. Chadema tuko tayari kukusaidia na kulisaidia Taifa. Siyo wakati wa kulumbana huu.
Freeman Aikaeli Mbowe
Mkuu wa Familia na Shuhuda wa Janga
Don't make a promise you can't fulfill...
Kwahyo kama ni kweli ndo upinzani utakufa? Viwanda vitaongezeka?Kwahiyo kumbe ni kweli jamaa alikuwa na korona.
Sema DAH!!
You an IdiotJanga la kitaifa halibagui, hakuna kuficha ficha . ukificha maana yake. Utaangamiza wengine kama isabela.
Huyu atangazwe dunia nzima na dunia imuogope ili wengine wapone.
Katiba na sheria ndogo ndogo zimesimama, wafungwa wanatolewa, shule zimefungwa, Haki za utu na Uhuru wa kutembea popote zimefungwa
Sasa inatakiwa atueleze hii corona kaipatia wapi?
Ikibidi ahojiwe kwa lazima tujue alikutana na watu wangapi ili tuzuie kusambaa.
Publication zisambae haraka ili kuvunja chain.
Vinginevyo kitendo cha kuzuia hii taarifa kwa umma ni ishara wazi familia ya Mbowe imejipanga kuangamiza taifa kwa kusambazia watanzania na dunia nzima.
Nasubiri aitishe maandano nchi zima ili kudai haki ya mtoto mgonjwa na siri za gonjwa hatarishi ( corona).
Ambao in ujinga.
Ujinga was siasa za Chadema kunako corona virus.
Huu ni mzigo mkubwa kwa taifa na dunia hawakupashwa kukoroma wala kufurukuta bali kujitangaza na kuomba msamaha wa mwisho wakielekea kujitenga (self quarantine)
Watoto wa kishua hawa wana marafiki zao kibao wanatoka nchi za njeNimejiuliza huyu kapataje Corona, inabidi atuambie, au Ni wale mabeberu ambao hawajazuiwa kuingia mpaka Sasa ambao pia Ni rafiki za baba, nahisi hii corona atakuwa amepata kwa wakishua wenzie.
Ni muhimu Sana kupata taarifa hizi, Mana huyu haendi kariakoo anafanya shoping mall. Mods ukiufuta Uzi jua mpaka pasakaa Hali itakuwa mbaya Sana and we need to lock down Kama Italy na uk Spain na usa
Anamaisha huko Italy walipatia Corona Kariakoo.