Fananisha bandari kavu zetu za Kwala na Isaka na hii ya DP World Kigali

Fananisha bandari kavu zetu za Kwala na Isaka na hii ya DP World Kigali

hiyo sio shida. tungeweza kujenga tu bandari na wawekezaji weningine wangekuja bongo kuwekeza kwenye bandari kavu kama tungekuwa tunaruhusiwa. shida ni pale DP WORLD wanaposema hatutaruhusiwa kuendeleza bandari nyingine wakati wa uhai wa mkataba wao. that means, wanataka wadominate dsm port na mizigo yao iende kigali kwa kutumia reli zetu. pia, tusiweze kujenga dry port zingine zitakazoshindana na kigali ambako wapo. wafanye wao tu.

kwani kama wao wanao uwezo kufanya shughuli za bandari, si waache mlango wazi ili watu wengine waje kujenga na kuwekeza bandari zingine ili ushindani uwepo? sisi watz tunataka wawekezaji wowote wale, na watatumia infrastructure zetu kusafirisha mizigo toka bandarini. dp world wanataka wao tu ndio wamonopolize. wajenge tu, wachina waje wajenge, wajapani waje, waarabu wengine waje kuwe na bandari nyingi reli na barabara zetu zinao uwezo kusafirisha mizigo hata ya bandari tatu zikijengwa bongo. dsm, bagamoyo na tanga.
 
Ushawahi kusikia ndege yoyote ya RwandAir imekamatwa ughaibuni na muwekezaji au scandal za ESCROW na MEREMETA?

Investor huyo huyo mmoja anaweka terms za mikataba kutokana na mazingira ya uwekezaji kwenye nchi husika na historia yao.

Angalia nchi ambazo DPW alitibuana nazo ni zenye historia kama yetu zaidi.

Anzeni kuweka mazingira ya uwekezaji yawe kama Rwanda kwanza.
 
Kama ndo hivyo basi Zanzibar wa sign mkataba na hawa waarabu wa Dubai kesho!!
Mbona Zanzibar wame saini kabla yetu kuendshewa bandari yao ya Malindi.

Kumbe hata habari huna halafu unataka kubishana kwa kujazwa ujinga?
 
Kwa uchache bandari zetu kavu ni mabomu. Tazama bandari kavu mpya inayoendeshwa na DP World Kigali 👇🏾

Halafu kuna wajuba wachache wenye chuki za kijinga wanajaribu kuzuwia maendeleo.

View attachment 2656975
Kinacholalamikiwa sio PD World bali ni mkataba . Vipengele vya mkataba ndio vinavyoongelewa. Mkataba wa DP World na Rwanda unaujua ? Je unafanana na huu unaopigiwa kelele hapa kwetu ?
 
Kinacholalamikiwa sio PD World bali ni mkataba . Vipengele vya mkataba ndio vinavyoongelewa. Mkataba wa DP World na Rwanda unaujua ? Je unafanana na huu unaopigiwa kelele hapa kwetu ?
DP world bado hawana mkataba wa kuendesha bandari, hata ukiwepo hauwezi kuwekwa wazi.
 
Kwa uchache bandari zetu kavu ni mabomu. Tazama bandari kavu mpya inayoendeshwa na DP World Kigali 👇🏾

Halafu kuna wajuba wachache wenye chuki za kijinga wanajaribu kuzuwia maendeleo.

View attachment 2656975
Kumbe hao wasiokuwa na bahari wameshakuwa na bandari za DP world miaka 4 nyuma.Sisi ndio kwanza tunajiuliza maswali.Ni wazi kuwa Kenya wanainyemelea hiyo fursa kuihudumia kanda ya kusini ya Afrika kuiunganisha na dunia kibiashara.
Ile mitambo ya majaribio tu inaonesha mizigo ya mteja haina nenda uje kesho tuitafute kwanza.Ukigusa tu inakuonesha kifurushi chako kipo wapi unaletewa unaondoka zako.
 
Back
Top Bottom