Fananisha bandari kavu zetu za Kwala na Isaka na hii ya DP World Kigali

Fananisha bandari kavu zetu za Kwala na Isaka na hii ya DP World Kigali

Tatizo hamuwapi Raia elimu ya kutosha kuhusu Faida na manufaa yatakayopatikana nanikwamda gani huo Mkataba utadum. Mnalaumu tu kuwa kuna watu wanapinga, mkae mkijuwa wanaowapinga wanahoja za maana namnatakiwa mzijibu, pia toeni Elimu ili hata wenye akili ndogo wawaelewe.
Mbona hili limejadiliwa bungeni na bunge sasa lipo live hata kwenye simu unalipata. Kama limekupita unaingia youtube tu utayakuta.

Huu siyo wakati wa mwendazake.

Sasa hivi mambo mdana mdana 👇🏾

 
Tatizo ni mkataba ulivyo ni general sana sio specific ni hatar sana inakuwa bandar ya ukoo kuna familia watakula pale had kifo chao na watoto watarithi
Wamekudanganya bana.

Hakuna nkaba wa kuendesha bandaru usio na mwisho.


Ule yaiojadiliwa bungeni ni makubaliano ya ushirikiano, huwezi kuyapa muda.

Mikataba ya uendeshaji ndiyo inakuwa na muda.
 
Mbona hili limejadiliwa bungeni na bunge sasa lipo live hata kwenye simu unalipata. Kama limekupita unaingia youtube tu utayakuta.

Huu siyo wakati wa mwendazake.

Sasa hivi mambo mdana mdana [emoji1484]

Unafiki, Ujuaji, ubinafsi na Njaa ndio tatizo. Hilo bunge lenu limejadili kwa mda gani, mkataba una kurasa nyingi tu unajadiliwa within a week., hivi unajuuwa maana ya sheria wew. Statement moja tu inaweza kubadilisha maana ya makabrasha yote.
 
Mkataaa DP World ni mpinga maendeleo.
 
Tunajua utendaji kazi wa DP WORLD hatuna mashaka nao hivyo hizi video ni useless

MADA MEZANI ni MKATABA WA HOVYO hebu acheni kuruka ruka kama popcorn,NENDENI kwenye POINT.
 
Ule yaiojadiliwa bungeni ni makubaliano ya ushirikiano, huwezi kuyapa muda.
Kwahiyo watu wawili wakikaa mezani wakubaliane kushirikiana kwenye jambo flani,ndio muda hauwekwi?

kwamba watashirikiana milele,huo ushirika ni wa roho mtakatifu au ushirika wa aina gani? Mpaka mnakaa

mezani kukubaliana kushirikiana,ni lazima upande mmoja umekubali kuwa umeelemewa/umezidiwa hivyo

unaomba ushirika kwa mtu mwingine,SAWA tumekubali BANDARI yetu imetuelemea imetuzidia uwezo kwahyo

wewe unaekuja kushirikiana na sisi kuvusha JAHAZI ndio tusikupe muda? kwamba utashirikiana na sisi milele

Hata ikifika hatua Tunajiweza,umetusaidia tukafikia hatua ya kujisimamia/kujiendesha wenyewe Bado "utaendelea"

kuwepo kama RUBA, utaendelea kuwepo kama nani? kufanya nini? kusaidia nini? kwanini MUDA usiwekwe tujue

baada ya miaka kadhaa tukifikia uwezo flani tutaangalia kama Tunahitaji huo ushirikiano au hatu uhitaji,kwann

nyie hicho kipengele mnakipiga dana dana na lugha zenu laini laini? Hata makubaliano ya Ushirikiano yana MUDA

Tunahitaji kuona huo muda,hatuwezi shirikiana na watu milele sisi sio watumwa kiasi hicho cha umilele.
 
Halafu kuna wajuba wachache wenye chuki za kijinga wanajaribu kuzuwia maendeleo
You loose your legitimacy
.
Hauko katika nafasi yoyote ya kimaadili ya kuelimisha kihalali, kwamba wananchi wanaokosoa uwekezaji uliowekwa hawana msingi wa kuhoji juu ya hatima ya nchi yao. Kwa sababu wao ni weusi.....

Kwanza, kwa kuwaita "Wajuba" unaashiria wao ni watu weusi, yaani ni watu wenye ngozi nyeusi na huo ni Ubaguzi dhidi yao,yetu.

Pili, kwa kuwalaani na kuwaita wanachuki na ni wajinga.... ni dharau kubwa sana, (ulaaniwe)kwa maneno mengine ni njia nyingine tu ya kuwanyima haki zao/zetu halali, haki ya kuwakataa watu waliotutesa, kutubaka, kutuua na kututenganisha na mababu zetu... Haiingii akilini kuwa Watu ambao wametawala kwa karne nyingi... Chini ya mwamvuli huo huo wa kutu-staha-arabisha na hivyo kutuletea Maendeleo, waje waendelee kwa mwamvuli huo huo! Hii peke yake ni dhana potofu.
Hata hivyo, "chuki" waliyo nayo,tuliyonayo inaweza kuwa halali kama inavyoweza kuwa.


Waarabu ni madhalimu.

Yaani kuwashusha jamii nzima inayopinga "uwekezaji" huu unaonekana kwa udhahiri ukienda kuwanyonya watu hao kuwa ni "Wachache" na hivyo kuashiria kuwa, kwa sababu ya uchache wao, basi wanakosa haki stahiki kuhoji! Huo ni Ukimbari, ni unyanyapaa! Ulaaniwe tena na tena.

Yaani, unawaita "Wajuba" kuashiria Uweusi waliokuwa nao, tayari umefanya kitendo cha kuwatenga kwa ngozi! Unadai ni wachache, wajinga na wanachuki! kwa mantiki ipi zaidi kama sio kutumia lugha ya unyanyasaji tu?

Inastaajabisha bado, katika karne hii, kuona au kusikia lugha chafu kama uliyotumia-that any resistance is a resistance to Development? It is abhorring

...
 
Hizo ndiyo ukisikia fikra za kimaskini.

Bandari yetu kwa kuendeshwa na DP World tumeshajihakikishia 100% ya mizigo ya Rwanda kukutua Dar.
Hiv kuna mtu anapinga uwekezaji kweli
 
Watanzania tumeshindwa, tunaposhindwa ni lazima tuwawachie wanaoweza.

Unamuona Kagame ni mjinga kuwawachia DP World?
Waulize madereva waliokuwa wanaenda Kigali kabla ya bandari kushikwa na DP World na sasa, wakueleze tofauti yake.
Tatizo lipo kweny mkataba ni mbovu
 
Watanzania tumeshindwa, tunaposhindwa ni lazima tuwawachie wanaoweza.

Unamuona Kagame ni mjinga kuwawachia DP World?
Waulize madereva waliokuwa wanaenda Kigali kabla ya bandari kushikwa na DP World na sasa, wakueleze tofauti yake.
Ipoje kaka

Hebu funguka
 
Ipoje kaka

Hebu funguka
Walikuwa wanakaa Kigali mpaka mwezi kungoja kushusha mzigo, siku hizi ni siku hiyo hiyo.

Dar mzigo wa Transit za Kigali dhamana ni DP World, serikali port charges zao za transit goods wanalipwa na DP World. Hakuna kucheleweshana.

Hayo ni madiliko makubwa sana.
 
now
Kwa uchache bandari zetu kavu ni mabomu. Tazama bandari kavu mpya inayoendeshwa na DP World Kigali 👇🏾

Halafu kuna wajuba wachache wenye chuki za kijinga wanajaribu kuzuwia maendeleo.

View attachment 2656975
now I understand kwanini kagame alikuja bongo majuzi hivi. hata hivyo, atakuwa mtumwa wetu kama akiunganishwa na dar port. kiukweli, uwekezaji kwenye hii bandari ni muhimu, tunachokwazika nacho ni terms za makubaliano, ila uwekezaji waarabu wapewe tu. ila kutuambia tusijenge bandari nyengine tutegemee ya kwao tu, ni ujinga gani huo?
 
Kwa uchache bandari zetu kavu ni mabomu. Tazama bandari kavu mpya inayoendeshwa na DP World Kigali 👇🏾

Halafu kuna wajuba wachache wenye chuki za kijinga wanajaribu kuzuwia maendeleo.

View attachment 2656975
Shida yako unaleta Siasa.

Nani amemkataa DP?....Yalee amasharti ndugu yangu hata mtu akija kwako fukuza kabisa.
 
Ni sawa tu na kufananisha DP world inayooperate London kwa mkataba wa waingereza na DP world inayotaka kuingia mkataba na Taifa Watanzania.

DP world Rwanda imekaa mezani na walio serious sio wafanya mizaha wa CCM, Barrick Gold ilipokutana na wafanya mizaha wa CCM ndio ikaitengeneza Acacia.

Tunachotofautiana Rwanda na Tanzania ni mmoja anaendekeza mizaha na mwingine yuko serious na future ya Taifa lake.
 
Back
Top Bottom