Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Kama kufa alishakufa. Hivyo hakuna jipya hata kidogo. Mbona hata yeye katoa watu wengi uhai bia sababu za msingi.
 
Unamcompare JPM na nan vile!!!???
 
Hata kama ana hizo tuhuma, timing ya kumkata ni mbovu, sasa hivi dunia inawaangalia.
Kwani dunia ikiangalia ndiyo nini? Muhalifu ni muhalifu tu. Na kila nchi ina wahalifu wake. Namusifu Kagame, puppets wamemujaribu pamoja na mabeberu wao kumujaribu aliwapa majibu powa. Angalia video hii. Mbona munaogopa dunia na Tanzania ni nchi mojawapo iko duniani? Tuondoleeni ujinga wa kikoloni.
 
Kama Mbowe ameua viongozi wa serikali,basi wakuu wote wa vyombo vya ulinzi wanapaswa kuwajibishwa na kuchukuliwa hatua Kali sana
 
Umeanza vibaya sentesi yako. Mbowe "hajakutwa" na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali, isipokuwa "anatuhumiwa". Polisi "wanatuhumu", hawaamui kesi. Mahakama ndiyo inayoamua baada ya kujiridhisha kuwa upande wa mashtaka imethibitisha tuhuma bila kuacha chembe ya shaka kwamba ni kweli anahusika na ugaidi na kuuwa viongozi wa serikali. Hivyo, kuwa mwangalifu jinsi unavyowalisha hoja yako.
 
Unashindwa kuwahoji wakina kikwete na genge lake unaenda kwa mbowe kwa access gani mbowe aliyonayo kuishinda intelligence ya nchi

Basi kama ni hivyo hatuna ulinzi nchi hii

Hata samia atauwawa muda wowote
Mkakati wa kuzima pacemaker ya Magufuli ulianza tar25/02/2021 Wakaanza kuichokonoa tar27/ 02/21
 
Mimi nadhani wametumia njia hii ya kumpa tuhuma nzito ili kupoza issue nzima ya katiba mpya. Maana ilianza kupamba moto sana. Ilianza kumfikia kila mtanzania. Kama wangeendelea vile, ingekua hatari huko mbele. Watawala wangetoa tu hiyo katiba
 
Nadhani ccm wanataka kuharibu kabisa uchumi wa TANZANIA sasa! Kama pamoja na hali mbaya ya uchumi na corona iliyopamba moto badala ya rais kuunganisha wananchi anagawa wananchi wake kama alivyofanya aliyepita, basi tutegemee hali mbaya zaidi ya uchumi Tanzania. Kwani wafanyi Biashara wa nje waliokimbia walitaka kurudi. Sasa wataanza kusita tena!!
Mbowe miaka yote amehubiri na kuishi non violence hata wakati serikali ikitumia violence nyingi dhidi yake yeye na viongozi katika chama chake. Yeye nyama tu zote aliendelea kushauri non violence! Iweje leo wamsingizie jambo la ajabu kama hilo??????
Nani ataamini wakati watz wengi sasa wanajua kuwa mfumo wa usalama wa taifa katika awamu ya tano na huenda hata sasa unaendelea na tabia ya kubambikizia watu kesi za uwongo kama ilivyothibitishwa na mahakama hapa karibuni!! Makonda alimbambikizia Mbowe kesi madawas ya kulevya na leo serikali hii imeleta jipya. Yote kwa kuwa serikali imekosa sababu za kisheria za kumkamata kwa ajili ya mikutano ya ndani ambayo imeruhusiwa na rais mwenyewe!!
Ni aibu kubwa Tanzania na kwa rais wetu tuliyemfurahia sana!! Shame on the government machinery! You embarrass us!!
 
Ndo yale yale ya magufuli yanaendelea sasa inamaana hiyo Corona iliyommaliza magufuli kaileta mbowe acha uzezeta.
 

Someni Biblia Takatifu.
Kirabu cha Nabii Yeremia.

YEREMIA 9: 23 - 24.

"BWANA ASEMA HIVI ,MWENYE HEKIMA ASIJISIFU KWA SABABU YA HEKIMA YAKE,WALA MWENYE NGUVU ASIJISIFU KWA SABABU YA NGUVU ZAKE ,WALA TAJIRI ASIJISIFU KWA SABABU YA UTAJIRI WAKE; BALI AJISIFUYE NA AJISIFU KWA SABABU HII, YA KWAMBA ANANIFAHAMU MIMI,NA KUNIJUA ,YA KUWA MIMI NI BWANA, NITENDAYE WEMA ,NA HUKUMU ,NA HAKI KATIKA NCHI; MAANA MIMI NAPENDEZWA NA MAMBO HAYO ,ASEMA BWANA."

Kila mtu atapita muda wake ukifika. Hata wangepata madaraka makubwa kiasi gani.
Wakaumbuke kusimamia na kutenda HAKI.

Kumuonea Mbowe sio jambo jema.
Dhulma iliyofanywa na makaburu kule Afrika kusini kwa kisingizio cha kujenga Nchi na miundo mbinu zake Leo dhulma hiyo inalighrimu sana taifa hilo.

Dhambi na dhulma inayofanywa Leo dhidi ya Mbowe na Chama chake zitakuja kuligharimu taifa miaka ijayo

Amani ni tunda la haki.
 
Hebu ondoa upumbavu wako hapa, eti taasisi za haki za binadamu wameona uonevu mateso waliofanyiwa watu wa mwanza! Tangu lini Mbowe wafuasi wake uchwara wakawa ni watu wa Mwanza? Ni kwanini mnalazimisha kuja kufanya vikao vyenu Mwanza? Mbona mnataka kutuchafulia sifa nzuri ya jiji na watu wa Mza! Chadema tambueni kabisa hamna chenu hapa! Tafuteni location nyingine mkafanye maigizo yenu!
 
Inashangaza sn,halafu watu si wajinga sikuhizi.Kumbambikia mtu kesi kijinga hivi ni ushamba.

Watakufa et hawa watu jamani,mbona hawajifunzi?

Watanzania sikuhizi maombi yao ni makali wakiamua kumshitakia Mungu
 
Pesa ya walipa kodi zinatumika hovyo kukandamiza demokrasia kwa njia haramu za kishetani, wametumia gharama kubwa kumsafirisha mbowe tokea mwanza hadi huko Dsm kwenda kusachi nyumbani kwake ni Aibu iliyoje
Pesa za tozo za miamala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…