Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unamcompare JPM na nan vile!!!???Siwaoni kabisa kabisa yaani nawa_zoom siwaoni yaani mpaka nataka kuwataja majina hapa hapa.
Walikuwa wanasifia kwa vimuemue style ya bimkubwa na kusema amekuja kuwafuta machozi kutokana na maumivu ya five years ago, sijui wako wapi asee!.
In 100 days ilikuwa ni shangwe na kusema tumeanza vizuri na tunaona machweo mujarabu, ila nilisema hata late president JPM in 100days mlimsifia kweli kweli although mnajua mlichokipata.
Jana nilisema viongozi wa kiafrika siku 100 hazina tija kumuweka kwenye mizania na kumpima tunapaswa kuvuta muda.
Pigia mstari ksbisa..Hahhaahhahaahahaha.
Mtumishi mwendawazimu sio?
Kwani dunia ikiangalia ndiyo nini? Muhalifu ni muhalifu tu. Na kila nchi ina wahalifu wake. Namusifu Kagame, puppets wamemujaribu pamoja na mabeberu wao kumujaribu aliwapa majibu powa. Angalia video hii. Mbona munaogopa dunia na Tanzania ni nchi mojawapo iko duniani? Tuondoleeni ujinga wa kikoloni.Hata kama ana hizo tuhuma, timing ya kumkata ni mbovu, sasa hivi dunia inawaangalia.
Alikuwa akichunguzwa. Uchunguzi huchukuwa muda murefu. Accept it and move on.Kwanini hakukamatwa tangu mwezi wa tatu?
Umeanza vibaya sentesi yako. Mbowe "hajakutwa" na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali, isipokuwa "anatuhumiwa". Polisi "wanatuhumu", hawaamui kesi. Mahakama ndiyo inayoamua baada ya kujiridhisha kuwa upande wa mashtaka imethibitisha tuhuma bila kuacha chembe ya shaka kwamba ni kweli anahusika na ugaidi na kuuwa viongozi wa serikali. Hivyo, kuwa mwangalifu jinsi unavyowalisha hoja yako.Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.
Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.
Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli na uki connect dot utaelewa Tundu Lisu alijuaje kama Magufuli anaumwa?
Lisu alikuwa anapewa na nani taarifa za kwamba Magufuli anaumwa na hatapona?
Bila shaka laptop za mbowe zilizokamatwa zimesema mengi kuhusu kundi la kigaidi.
Ni haya makundi ya ugaidi ndiyo yalikuwa yanawapa taarifa.View attachment 1863503
Kama kufa alishakufa. Hivyo hakuna jipya hata kidogo. Mbona hata yeye katoa watu wengi uhai bia sababu za msingi.
Mkakati wa kuzima pacemaker ya Magufuli ulianza tar25/02/2021 Wakaanza kuichokonoa tar27/ 02/21Unashindwa kuwahoji wakina kikwete na genge lake unaenda kwa mbowe kwa access gani mbowe aliyonayo kuishinda intelligence ya nchi
Basi kama ni hivyo hatuna ulinzi nchi hii
Hata samia atauwawa muda wowote
Kabisa mkuu. Aliumiza watu wengi sana. Pia alikuwa ni chanzo kikubwa cha kifo cha mama yake Kabendera.Tena majeraha ya Lissu ni evidence ya unyama wake..
Na charles mbowe alimuumiza nani?Kabisa mkuu. Aliumiza watu wengi sana. Pia alikuwa ni chanzo kikubwa cha kifo cha mama yake Kabendera.
Ndo yale yale ya magufuli yanaendelea sasa inamaana hiyo Corona iliyommaliza magufuli kaileta mbowe acha uzezeta.Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.
Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.
Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli na uki connect dot utaelewa Tundu Lisu alijuaje kama Magufuli anaumwa?
Lisu alikuwa anapewa na nani taarifa za kwamba Magufuli anaumwa na hatapona?
Bila shaka laptop za mbowe zilizokamatwa zimesema mengi kuhusu kundi la kigaidi.
Ni haya makundi ya ugaidi ndiyo yalikuwa yanawapa taarifa.View attachment 1863503
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.
View attachment 1862953
====
UPDATES;
=====
TAARIFA KWA UMMA
JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"
Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.
Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake, Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.
Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.
Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'
Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria. Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.
Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .
Waraka wa Mbowe kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi. Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania. Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.
Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”
Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
=====
UPDATE:
View attachment 1863559
View attachment 1863560
Hebu ondoa upumbavu wako hapa, eti taasisi za haki za binadamu wameona uonevu mateso waliofanyiwa watu wa mwanza! Tangu lini Mbowe wafuasi wake uchwara wakawa ni watu wa Mwanza? Ni kwanini mnalazimisha kuja kufanya vikao vyenu Mwanza? Mbona mnataka kutuchafulia sifa nzuri ya jiji na watu wa Mza! Chadema tambueni kabisa hamna chenu hapa! Tafuteni location nyingine mkafanye maigizo yenu!Hata mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC sasa wanaanza kuangazia hilo taasisi za haki za binadamu zote wameona uonevu mateso waliofanyiwa wananchi kule mwanza, hii inaenda kumletea chuki kubwa Mama na itaharibu mazuri machache aliyokuwa kaanza kuyafanya
Pesa za tozo za miamala?Pesa ya walipa kodi zinatumika hovyo kukandamiza demokrasia kwa njia haramu za kishetani, wametumia gharama kubwa kumsafirisha mbowe tokea mwanza hadi huko Dsm kwenda kusachi nyumbani kwake ni Aibu iliyoje