Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953

====

UPDATES;

=====

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es
Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.

Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake ,Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.

Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.

Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'

Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria.
Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.

Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .

Waraka wa Mbowe Kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi.
Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania.
Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.

Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Hivi huyu kachanganyikiwa eti tuendeleze mapambano. Kwanza hamsemi hii katiba ya sasa ina mapungufu gani. Je ni Tz wangapi wameisoma hii katiba. Hizi cheap politics tumechoka nazo nyie waroho wa madaraka
 
Kwa kazi hii aliyoianza Samia atakapoanza kutengwa kimataifa na kunyimwa misaada na nchi mbalimbali ataweza kuhimili vishindo vyake kama Magufuli alivyokuwa anafanya mambo yanapokuwa Magumu alikuwa anaingia mitaani na silaha za kivita kunyang'anya kodi kama jambazi? .
 
samia afanye udikteta tu lakini mashirika ya Kimataifa na Nchi za wafadhili zikiamua kutotoa mikopo na misaada kutokana na nchi kukosa demokrasi hapo ndiyo Watanzania watatia akili kichwani kwani ugumu wa maisha utaongezeka mara tatu ya ilivyo sasa na Serikali itakuwa haina jinsi bali kupitisha fagio la chuma Serikalini litakalosomba Wafanyakazi wengi sana.

hahahahahaha, jumuiya ya kimataifa na nchi wafadhili...wale wenzenu wapo kwa ajili ya maslahi yao wakihakikishiwa maslahi yao wanaweza hata kumuweka Mbowe kwenye kundi la Alqaeda na kushirikiana na hao hao CCM.....waulizeni wenzenu Muslim brotherhood baada El sis kuahidi kuilinda Israel na maslahi ya USA....hahahahahahahaha huu ndio ninaouita utoto..

ushajiuliza kwanini Paka na M7 wanafia madarakani na hawaguswi?... JPM ni kwa vile tu naye alikuwa jeuri mpaka kwenye maslahi yao japo ilikuwa 50/50....eti jumuiya ya kimataifa komaeni kudai mnachohitaji....
 
Hata mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC sasa wanaanza kuangazia hilo taasisi za haki za binadamu zote wameona uonevu mateso waliofanyiwa wananchi kule mwanza, hii inaenda kumletea chuki kubwa Mama na itaharibu mazuri machache aliyokuwa kaanza kuyafanya

Brother TL mapigwa risasi daylight pale Dom..akina Mbowe sio mara ya kwanza kukaa jela...hizi chaguzi miaka yote tunasema zinabakwa maana hata Lipumba alishawahi kushinda akaibiwa kura, Lyatonga NCCR pia, Dr Slaa pia, Mbowe, Lissu hawa wote walishashindaga uchaguzi, ushasikia kuna mtu kaenda ICC aka the hague au TZ kuwekewa vikwazo...
 
Tunasubiri kwa hamu kuona Mbowe akifunguliwa mashitaka ili nione alipanga kuua viongozi wepi wa serikali? Ili afaidike na nini? Aingie ikulu au? Wenzake sita wanaoshikiliwa gerezani ni kina nani?

Je, walishatimiza lengo lao la kuua baadhi ya hao viongozi wa serikali?

NB: Hizi ni tuhuma kubwa sana! Nadhani mara ya mwisho tuhuma kama hizi zilitokea wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere!
 
Kumbe mama ana roho mbaya kiasi hiki! Hivi hawa watu hawajui kuwa hapa tunapita, sote ni mchanga tu
 
Tunasubiri kwa hamu kuona Mbowe akifunguliwa mashitaka ili nione alipanga kuua viongozi wepi wa serikali? Ili afaidike na nini? Aingie ikulu au? Wenzake sita wanaoshikiliwa gerezani ni kina nani?...
Kisha ukishajua utafanya nini?
 
😭😭😭😭😭😭 Tanzania yangu inazidi kujipaka mavi kwenye uso wa dunia nani wa kuishauri??
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.

Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.

Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli

Ndiyo maana LISU alikuwa wa kwanza kusema Magufuli anaumwa na hatapona.
 
Rais ameapa kulinda Amani na utulivu wa nchi hii na endapo akitokea mtu au watu wanaleta au kutishia Amani ya nchi lazima wachukuliwe hatu za kisheria, haijalishi ni kiongozi wa kisiasa au kiongozi wa kidini...
Makosa yapi mtu kutekeleza haki yake ya katiba ndo iwe nongwa mfungeni mbona wakina Mandela wamekaa miaka 27 jela yeye sio wakwanza
 
Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.

Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.

Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli na uki connect dot utaelewa Tundu Lisu alijuaje kama Magufuli anaumwa?
Ni haya makundi ya ugaidi ndiyo yalikuwa yanawapa taarifa.View attachment 1863503
Ata mimi nilijua kuwa Magu mgonjwa,aya nikamateni basi. Tusiwe wajinga,Magu kafa kwa ujinga wake msitafute pa kufutia aibu.

Toa ushahidi beyond reasonable doubt sio kuongea tu kama headless chicken
 
Hilo ndo lilowaponza, mlishindwa kusoma alama za nyakati, hakuna mwananchi wa kawaida 2020 angeacha kumpigia kura JPM, hizo chuki na mitusi yenu mitandaoni kwa wachache mlonyooshwa mkajidanyanya na bado mnajidanganya ndo wananchi mlifail na mnafail sana.
Yuko wapi Sasa huyo aliyechaguliwa?
 
Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.

Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.

Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli na uki connect dot utaelewa Tundu Lisu alijuaje kama Magufuli anaumwa?
Ni haya makundi ya ugaidi ndiyo yalikuwa yanawapa taarifa.View attachment 1863503
Hawa viongozi wa serikali wanapotunga uongo wa kutisha kama huu wanalenga nini hasa?
 
na tunaomba Jeshi letu la polisi kwa kushirikiana wafanye uchunguzi wa kina na wa kitaalamu bila kufanya makosa wakamatwe wote amabao wapo ktk mtandao wa kuratibu na kupanga matukio ya kigaidi.wasibaki maana hao ni hatari sana kwa usalama wa Ncho yetu
 
Back
Top Bottom