Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi huyu kachanganyikiwa eti tuendeleze mapambano. Kwanza hamsemi hii katiba ya sasa ina mapungufu gani. Je ni Tz wangapi wameisoma hii katiba. Hizi cheap politics tumechoka nazo nyie waroho wa madarakaBaada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.
View attachment 1862953
====
UPDATES;
=====
TAARIFA KWA UMMA
JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"
Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es
Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.
Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake ,Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.
Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.
Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'
Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria.
Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.
Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .
Waraka wa Mbowe Kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi.
Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania.
Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.
Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”
Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
samia afanye udikteta tu lakini mashirika ya Kimataifa na Nchi za wafadhili zikiamua kutotoa mikopo na misaada kutokana na nchi kukosa demokrasi hapo ndiyo Watanzania watatia akili kichwani kwani ugumu wa maisha utaongezeka mara tatu ya ilivyo sasa na Serikali itakuwa haina jinsi bali kupitisha fagio la chuma Serikalini litakalosomba Wafanyakazi wengi sana.
Hata mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC sasa wanaanza kuangazia hilo taasisi za haki za binadamu zote wameona uonevu mateso waliofanyiwa wananchi kule mwanza, hii inaenda kumletea chuki kubwa Mama na itaharibu mazuri machache aliyokuwa kaanza kuyafanya
Kisha ukishajua utafanya nini?Tunasubiri kwa hamu kuona Mbowe akifunguliwa mashitaka ili nione alipanga kuua viongozi wepi wa serikali? Ili afaidike na nini? Aingie ikulu au? Wenzake sita wanaoshikiliwa gerezani ni kina nani?...
Makosa yapi mtu kutekeleza haki yake ya katiba ndo iwe nongwa mfungeni mbona wakina Mandela wamekaa miaka 27 jela yeye sio wakwanzaRais ameapa kulinda Amani na utulivu wa nchi hii na endapo akitokea mtu au watu wanaleta au kutishia Amani ya nchi lazima wachukuliwe hatu za kisheria, haijalishi ni kiongozi wa kisiasa au kiongozi wa kidini...
Ata mimi nilijua kuwa Magu mgonjwa,aya nikamateni basi. Tusiwe wajinga,Magu kafa kwa ujinga wake msitafute pa kufutia aibu.Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.
Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.
Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli na uki connect dot utaelewa Tundu Lisu alijuaje kama Magufuli anaumwa?
Ni haya makundi ya ugaidi ndiyo yalikuwa yanawapa taarifa.View attachment 1863503
Mbona polis hawajasema kwamba ameua watuMbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.
Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.
Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli
Yuko wapi Sasa huyo aliyechaguliwa?Hilo ndo lilowaponza, mlishindwa kusoma alama za nyakati, hakuna mwananchi wa kawaida 2020 angeacha kumpigia kura JPM, hizo chuki na mitusi yenu mitandaoni kwa wachache mlonyooshwa mkajidanyanya na bado mnajidanganya ndo wananchi mlifail na mnafail sana.
Hawa viongozi wa serikali wanapotunga uongo wa kutisha kama huu wanalenga nini hasa?Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.
Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.
Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli na uki connect dot utaelewa Tundu Lisu alijuaje kama Magufuli anaumwa?
Ni haya makundi ya ugaidi ndiyo yalikuwa yanawapa taarifa.View attachment 1863503