Hii movie kuhusu viongozi wa CHADEMA imeandaliwa kwa kiwango cha chini mno na inaabua maswali mengi kuliko majibu kuzidi hata ile ya kutekwa kwa MO.
Na kwakuwa jambo hili linaonekana kugusa hisia za watu wengi na kuvuka mipaka ya nchi huku shinikizo likiongezeka, sitashangaa wakati wiwote wakatafutwa watu wa kubebeshwa lawama na hao wanaweza kuwa ni Sirro na pengine hata Boss wa TISS
Inawezekana Mama asiwe na wazo la kubebesha mtu lawama kwa makosa yake, ila wanasiasa wenzake na ambao ni wakongwe ndani ya chama, wanaweza kumshauri afanye uamuzi wa kuwato watu mbuzi wa kafara ili kulinda image yake.
Tuhuma hizi ni nzito, ngumu kuzithibitisha na inaonekana walizi-underestimate huku dunia ikifuatilia, hivyo ni lazima wajisafishe na katika kujisafusha huko, Sirro ndio anaeweza kuwa wa kwanza kubebeshwa zigo la lawama kwa kuondolewa katika nafasi yake huku Boss wa TISS nae akikalia kuti kavu.
Tusubiri.