Twilumba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 12,576
- 14,522
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lilioandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) katika Ukumbi wa Kuringe - Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 08 Machi, 2023.
View attachment 2541597
Rais Samia akipokelewa na Viongozi wa Chadema kwenye uwanja ndege wa KIA baada ya kuwasili.Rais Samia amewasili ukumbini na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe. Mkutano huu umehudhuriwa pia na Viongozi wa kamati kuu ya Chadema, viongozi wa kanda na mabaraza, Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, viongozi wa dini, wageni wengine waalikwa pamoja na wanachama na wapenzi wa Chadema.
View attachment 2541670
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili ukumbini
CATHERINE RUGE, KATIBU WA BAWACHA
Amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano huo na amesema kuwa hawakumualika Rais kimakosa kwani ni mwanamke mwenzao.
Amejivunia kujenga baraza imara lenye ushawishi mkubwa nchini, amemkumbusha Rais kuwa wanawake ni jeshi kubwa na wapo Milioni 31 kwa mujibu wa Sensa iliyopita. Pamoja na wingi huu, hadhi ya wanawake nchini ni ndogo, wanaishi maisha duni. Kwenye mkutano huu pekee, wanawake 3234 wamehudhuria.
Amemshauri Rais Samia kutokuogopa kukatishwa tamaa na wale wasio itakia mema nchi hii ambao kwa kiasi kikubwa ni wanaume kwani mwanamke akiamua jambo lake hulifanya pasipo kurudi nyuma.
BAWACHA imetambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia akishirikiana na Mhe. Freeman Mbowe katika maridhiano na kutafuta katiba mpya kabla ya mwaka 2025. Ameomba jambo hili liendelee kufanyika kwa kasi kubwa ili matamanio ya watu yaweze kutimia.
Kuhusu Kuuliwa kwa watu na polisi, Mhe. Ruge amesema BAWACHA inalaaani vikali mauaji yanayofanywa na Polisi kwa raia wakiwa Mtaani na vituoni.
"Hatufurahishwi na mauaji yanayotokea katika maeneo mbalimbali yanayofanywa na jeshi la polisi hasa katika vituo vya polisi na maeneo mengine ya ukamataji. BAWACHA tutaendelea kutetea haki ya kuishi, haki ya uchaguzi, haki ya kupata ajira, haki ya kupata huduma bora za afya hasa za wanawake na watoto, haki hizi zote zimekuwa zinavunjwa kinyume cha Katiba" amesema Ruge
SHARIFFA SULEIMAN, MWENYEKITI BAWACHA
Ametaja mafaniko kadhaa yaliyochangiwa na BAWACHA kichama na katika ngazi ya Taifa, pia ameelezea mambo waliyofanyiwa wanawake kwenye chaguzi za mwaka 2019 na 2020 ambao amesema ulikuwa ni unyanyasi mkubwa uliofanywa kidikteta.
Kwa niaba ya BAWACHA, Mhe. Sharifa akimuona ametoa mambo manne kwa Rais akimuomba-
Kuhusu suala la Wabunge 19 linaloendelea Mahakamani, Mhe. Shariffa amemuomba Rais alitazame kwa undani na kulipatia majibu. Amewakaribisha wanachama waliokimbia nchi wajisikie nyumbani nankuwahakikishia kuwa zama za kutekana na kupotezana hazina nafasi kwa sasa.
- Kupunguza bei za vyakula na kudhibiti mfumuko wa bei
- Kuongeza kima cha chini cha mshahara
- Kuboresha sekta ya afya
- Kurejesha mchakato wa Katiba na tume huru ya uchaguzi, katiba itakayorudisha heshima ya nchi
JOHN MNYIKA, KATIBU MKUU CHADEMA
Akimkaribisha Mwenyekiti wa Chama chake, Mhe. Mnyika ametoa mapendekezo ya kuikumbusha serikali pamoja na vyama vyote vya kisiasa kuwa kila jambo wanalofanya liwe linazingatia maslahi na makatwa ya wananchi kwa kuwa hii ni nchi yao. Pia, amesema watanzania wanalia ugumu wa maisha na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Amemuomba Rais pamoja na Mhe. Mbowe katika safari ya maridhiano wanayoenda nayo kutokusahau mambo hayo mawilli.
Naomba nioneshwe sehemu Freeman Mbowe amesema "Rais Samia, CCM ilipora uchaguzi na kuumiza watu" kama heading ilivyo hapo juu!!