Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 21, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View attachment 3181677

View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Khaa!!
Huyu Baba mkavuuuu

Dikteta Mbowe
 
Ili uwe mwanasiasa mwenye mafanikio Africa HAKIKISHA una sifa tatu kati ya hizi ama uwe nazo ZOTE na yawezekana LISSU anayo moja ama HANA.

1; KUWA MNAFIKI WA VIWANGO VYA JUU,waambie watu yasyokuwa malengo yako huku ukiwahakikishia hayo ndio malengo yako.
2; KUWA KATILI WA VIWANGO VYA JUU ZAIDI,kumuua mwenzio ama kufanikisha kufa lisiwe jambo gumu kwako,mpeleke machinjioni akachinjwe.
3 ; KUWA MSHIKINA AMA MCHAWI MKUBWA NA ULIYEKUBUHU.
4;WAARIFU,VIONGOZI WA DINI WAWE WAFANIKISHAJI WA NIA YAKO HOVU.
Kama HUNA HIZO SIFA,KUJIITA MWANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA NI UZEZETA NA UNATUMIWA KAMA NGAZI TU YA KUPANDIA JUU WALE WENYE SIFA ZAO.

Nikiwa kijana wa miaka 18 nilibaini hayo na kwakuwa mimi sina hizo sifa mpaka uzee wangu huu SIJAWAHI KUANDISHWA WALA KUJIUNGA NA CHAMA CHOCHOTE CHA KISIASA.

Poleni mnaotumiwa,mliotumiwa na wanasiasa na naona LISSU hakuwahi kuyafahamu haya na hata wale waliouawa pale Arusha kwenye maandamano walikuwa hawajui sifa za wanasiasa.

Ongeza zingine taratibu.
 
Freeman Mbowe ataheshimika sana kama ataweka tamaa nyuma na kuachia kiti kwa heshima. Otherwise, Chama kitakosa legitimacy na moral authority ya kuwasema vibaya CCM

Siku zote tunapaswa kuyaishi tunaoyaongea na kuwahubiria wengine wafanye. Vipindi vinne vya uongozi totalling 20 good years inatosha kabisa na hizi kelele nyingine ni kelele za wenye njaa wanaofaidika na mfumo uliopo
Amuacgie kiti nani? Tundu Lissu mwenye risasi mwilini? Tuwe SERIOUS wakati mwingine
 
Hatumtaki. Akalee wajukuu zake. Jitu gani miaka 20 bado linataka kutawala.
 
Amuacgie kiti nani? Tundu Lissu mwenye risasi mwilini? Tuwe SERIOUS wakati mwingine
Kama haoni (au wewe pia hauoni) wa kumuachia after 21 years, CCM nayo itasema haioni wa kumuachia Nchi maana “wote ni mazwazwa na au wana risasi mwilini”

Tuwe serious indeed. Na usije na ngonjera kwamba kuongoza Nchi ni tofauti na kuongoza Chama..

Lakini hii haishangazi kwa kuwa ni hulka ya viongozi karibia wote wa hivi vyama vya upinzani. CHADEMA chini ya Mbowe sasa ni wazi kwamba haina tofauti na UDP, CUF na TLP. Viongozi ni wachumia tumbo tu
 
Pumzika kidogo tuwa angalie na wengine uwezo wao wewe ume fanya kazi kubwa sana
 
TUKUTANE KWA GROUND !
Ila kusiwepo na figisu figisu !
Je inawezekana kusiwepo na figisu figisu ??!

Kwa maana kama kutakuwepo na figisu figisu that means kumbe ni sawa tu hata Watemi wengine wakiwafanyia nyinyi figisu figisu kwenye mauchaguzi ya Vyama vingi !

Kama kutakuwa na figisu figisu kwenye uchaguzi wenu mtakuwa mmehalalisha kale kamsemo ka Waswahili kwamba-
Mwenye Nguvu Mpishe 😳🙄 !
Iko vile bandugu !
Kwahiyo hakikisheni hakuna figisu figisu hakuna kwenye uchaguzi wenu ili nanyi msije kufanyiwa mkaanza kulalamika !
Itakuwa ni “kijiti na boriti “ !
 
Leo ndio nimepata majibu ya wapi ulitoka ujasiri wa mke wa Mbowe na mwanae kujitokeza kwenye maandamano ya CHADEMA ya kupinga vitendo vya utekaji ya hivi karibuni.

Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Leo ndio nimepata majibu ya wapi ulitoka ujasiri wa mke wa Mbowe na mwanae kujitokeza kwenye maandamano ya CHADEMA ya kupinga vitendo vya utekaji ya hivi karibuni.

Muda ni mwalimu mzuri sana.
Chadema ni mali ya familia ya mbowe hawezi kurithisha mali yake na familia kwa Myaturu, pale pesa ipo, ila ndo mwisho wa upizani Tz kwasbabu Mbowe ataakishindwa uchaguzi hawezi kukubali CCM bado itaendelea kutawala angalau more 50yrs.
 
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 21, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View attachment 3181677

View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Ngoma mbichi kabisa hii
 
Back
Top Bottom